JK amemsimamisha Jairo kupisha uchunguzi wa Bunge - PINDA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK amemsimamisha Jairo kupisha uchunguzi wa Bunge - PINDA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mathias Byabato, Aug 25, 2011.

 1. Mathias Byabato

  Mathias Byabato Verified User

  #1
  Aug 25, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 905
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Pinda amesema bungeni
   
 2. jcb

  jcb JF-Expert Member

  #2
  Aug 25, 2011
  Joined: Jul 6, 2010
  Messages: 281
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Raisi J K amemsimamisha kazi Bwana Jairo, Hii ni kauli iliyo tolewa na Waziri mkuu wakati akijibu swali la Mh. Mbowe asubuhi hii
   
 3. r

  reformer JF-Expert Member

  #3
  Aug 25, 2011
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 387
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Waziri mkuu akijibu swali la papo kwa papo toka kwa Mbowe amesema Rais amemrudisha Jairo kuendelea na likizo wakati kamati ya bunge itakayoundwa ikiendelea na uchunguzi.
  Hii ni movie nyingine ya kihindi..sijui itaishaje, let us wait and c!!!
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Aug 25, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Akijibu swali la Mh Mbowe kiongozi wa upinzani, wakati wa maswali ya papo kwa hapo, Waziri Mkuu Pinda amesema kuwa tayari Rais ameshakuwa hatua ya kumsimamisha kazi Ndugu Jairo wakati huu ambao kamati teule ya bunge inafanya uchunguzi.

  Source: TBC1 -bunge
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Aug 25, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,563
  Likes Received: 18,294
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,
  Rais Jakaya Kikwete, amemuweka pembeni swahiba wake David Jairo baada ya kurejea kazini kwa siku moja tuu!
   
 6. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #6
  Aug 25, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ktk maswali ya papo kwa papo, Pinda akimjibu Kiongozi wa kambi ya upinzani amesema, Jairo amerudishwa likizo ili kupisha uchunguzi wa kamati Bunge itakayokwenda kumchunguza hivi karibuni.
  Awali Mbowe aliuliza swali la kutaka kwanini Jairo asirudi likizo ili kupisha uchunguzi wa kamati teule.
   
 7. m

  migomo ya vyuo Member

  #7
  Aug 25, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wana jf napata taarifa ya ile filim ya jairo inaendelea baada ya mh. waziri mkuu mizengwe pinda kulijulisha bunge kwamba jairo amerudishwa likizo kupisha uchunguzi. wana jf hebu tujadili hii inatosha? kwanini wasiwapeleke likizo CAG,Katibu mkuu kiongozi,pamoja na waziri wa wizara husika? je si ndio muda muafaka wa kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais kwani amepingana na hawafanyi kazi kwa ushirikiano na waziri mkuu pamoja na bunge, kwanini waziri mkuu asijiuzulu? naomba kuwasilisha
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Aug 25, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,563
  Likes Received: 18,294
  Trophy Points: 280
  Hatimaye Rais Jakaya Kikwete amemtosa rasmi David Jairo ikiwa ni siku moja tuu baada ya Luhanjo kumrejesha kazini.
   
 9. SOKON 1

  SOKON 1 JF-Expert Member

  #9
  Aug 25, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,114
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Leo ktk kumuuliza waziri mkuu swali kwa serikali kutoa tamko kusimamishwa kwa kazi kwa Jairo ili kurahisisha kamati itakayoundwa na bunge kumchunguza.!
  Waziri mkuu akasema tayari Jairo kasimamishwa kazi toka jana.
  My take:
  Wale wote waliompokea kwa mbwembwe pamoja na Ngeleji wataweka sura zao wapi?
  Nawasilisha
   
 10. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #10
  Aug 25, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,857
  Likes Received: 4,533
  Trophy Points: 280
  Salaam wana JF!

  Katika muendelezo wa tamthilia ya Pesa za Jairo, waziri mkuu leo bungeni amesema kwamba utaratibu wa kumpeleka ndugu Jairo likizo ili kupisha uchunguzi wa kamati teule ya bunge umeanza kuratibiwa na muhishiwa rais.Waziri mkuu amesema hayo wakati akijibu swali la papo kwa hapo la kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni. Katika swali la msingi, ndugu Mbowe alimuuliza waziri mkuu kwamba, je, serikali haioni kwamba ni wakati muafaka kumrudisha ndugu Jairo likizo tena ili apishe uchunguzi wa kamati teule ya bunge?
  Katika swali la nyogenza ndugu Mbowe akamuuliza waziri mkuu kwamba, kutokana na majibu ya katibu mkuu kiongozi, ndugu Luhanjo kwamba utaratibu wa uwezeshaji wa bajeti katika wizara ni wa kawaida, je, waziri mkuu unataka kusema hii ndio sera ya serikali? (ndugu Mbowe alitoa mifano ya uwezeshaji huo kwa ofisi ya waziri mkuu na wizara ya Jairo) Hapo waziri mkuu akaleta porojo za siasa, kwamba hilo suala tuiachie kamati teule. Yaani anasahau kwamba hiyo kamati teule ni ya kuchunguza wizara moja tu!
   
 11. F

  Fareed JF-Expert Member

  #11
  Aug 25, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Waziri Mkuu Mizengo Pinda ametangaza Bungeni leo asubuhi kuwa Rais Jakaya Kikwete ameamua kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo, asimamishwe kazi tena kwa kwenda likizo ya malipo wakati kamati itakayoteuliwa na Bunge itakapokuwa inafanya uchunguzi wake. Pinda alisema hayo wakati akijibu suali la kiongozi wa upinzani Bungeni, Freeman Mbowe.
  Huu umekuwa mchezo wa kuigiza sasa. Ikulu hiyo hiyo si ndiyo iliagiza Jairo arudishwe kazini baada ya uchunguzi wa CAG kumsafisha? Na huu utaratibu wa viongozi kupelekwa likizo kupisha uchunguzi wa Bunge umeanza lini?

  Mbona kamati ya Mwakyembe ilipokuwa inachunguza kashfa ya Richmond kwa nini Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati na Madini nao hawakusimamishwa kazi kupisha uchunguzi?

  Serikali legelege ya Kikwete sasa inaendeshwa na Bunge!
   
 12. Mwache77

  Mwache77 Senior Member

  #12
  Aug 25, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  Hzo ndio habari tulikuwa tuna zisubiri kwa kutoka kwa mkuuuu wa kaya,safi sana.Tunasubiri tume ya bunge.
   
 13. W

  Wakwetu Senior Member

  #13
  Aug 25, 2011
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 157
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa waziri mkuu leo akiwa anajibu swali la Mh. Mbowe kuwa kwa nini jairo asisimamishwa wakati kamati itakayoundwa inafanya kazi amesema kuwa tayari rais amempa likizo tena bwana Jairo, kwa wananchi wa kawaida inaleta picha gani ukichukulia kuwa bwana Luhanjo alivyokuwa na makeke kumfagilia wakati anamrudisha kazini na mapokezi yaliyofanyika wizarani jana. Sina uhakika ila huenda alifanyiwa pati na fungu la wizara.
   
 14. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #14
  Aug 25, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hongera JK kwa kufanya maamuzi mazito, magumu na ya kiume. Sasa wapinzani wako sijui watapata wapi cha kuongea? Umethubutu, Umeweza sasa hebu SONGA MBELE!
   
 15. L

  LAT JF-Expert Member

  #15
  Aug 25, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  na wale wafanyakazi wa wizara ya nishati na madini waliosukuma gari lake nao wasimamishwe haraka sana
   
 16. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #16
  Aug 25, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,563
  Likes Received: 18,294
  Trophy Points: 280
  Waziri Mkuu. Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda, amelitangazia Bunge kuwa Rais Jakaya Kikwete ametengua uamuzi wa Katibu Mkuu Kiongozi, kumrejesha David Jairo kazini, hivyo Jairo kuendelea kuwa likizo ya malipo akisubiri matokeo ya kamati teule ya Bunge.

  Waziri Mkuu alikuwa akijibu swali la kiongozi wa upinzani bungeni Mhe. Freeman Mbowe aliyetaka Jairo awekwe pembeni kupisha uchunguzi wa kamati teule ya bunge.
   
 17. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #17
  Aug 25, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mkuu Jcb,
  Nadhani hajasimamishwa kazi amerudishwa likizo. Hii ni kwa sababu mbowe aliuliza kwanini Jairo asirudishwe likizo kupisha uchunguzi wa Bunge? Waziri mkuu akajibu, hilo limeshatekelezwa na Rais. Kwa hiyo, kilichotekelezwa ni kumrudisha likizo si kumsimamisha kazi. Na nadhani anaendelea kulipwa mshahara wake kama ilivyo kuwa awali. Sarakasi ya Serikali legelege inaendelea.
  Thax.
   
 18. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #18
  Aug 25, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hakuna kitu hapa
   
 19. m

  menny terry Senior Member

  #19
  Aug 25, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 187
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  hakuna kitu kama hicho waka hakitakaa kitokee.Pinda nae si ajiuzulu tu hayo mafao yake siatapata kama anavyopata lowasa! Ama kweli auwae kwa upanga atauliwa kwa upanga.pinda alimwaibisha Magufuli sasa yamemkuta.
   
 20. gmosha48

  gmosha48 JF-Expert Member

  #20
  Aug 25, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,955
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  You can't be serious! Kama ni kweli hii itakuwa ze commedy kama jamaa alivyodai mwanzoni.
   
Loading...