JK afunguka kuhusu kustaafu kwake

JK afunguka kuhusu kustaafu kwake

Well then, lets decide and judge: "We have scaled up on roads,on construction,on education,on health,and many other things" 1."We have scaled up on roads"- Kutoka kwenye barabara chache imara (maana mpaka leo zipo) kwenda kwenye barabara nyingi mpaka mitaani lakini mbovu zimedumu miezi 4! Quite a scalling up. Don't you think? 2."We have scaled up on Construction"- Sure! Kipindi cha Wengine kulikuwa na majengo machache. Sasa tuna maghorofa mpaka yanatishia usalama wa Ikulu na wao wako ok. Tunajua kuuza viwanja! Zamani mab
 
Kikwete's legacy after he retires will be the fragmentation of what was a homogenous nation by using religion as the yardstick in making senior government appointments!! Vasco Dagama ndio baba wa udini Tanzania; godfather wa wakina Ponda.

Atakumbukwa pia kama mtu aliyegeuza URAIS kama mali ya familia yake na pia patron wa majangili na wauza madawa ya kulevya.

who is this guy he deserves my ID
 
Kutoa Huduma za kijamii(elimu, afya miundombinu) ndio kazi ya Serikali hio haina mjadala sababu tunalipa kodi. Tunataka atueleze kuhusu wakulima, wafugaji, viwanda, ajira na mengine kama hayo kafanya nini?

Unajua watu wanashindwa kujua wajibu wa serekali kwa hiyo likifanyika jambo wanadhani ni fadhila.
 
Kikwete's legacy after he retires will be the fragmentation of what was a homogenous nation by using religion as the yardstick in making senior government appointments!! Vasco Dagama ndio baba wa udini Tanzania; godfather wa wakina Ponda.

Atakumbukwa pia kama mtu aliyegeuza URAIS kama mali ya familia yake na pia patron wa majangili na wauza madawa ya kulevya.

Aione Ritz THE BIG SHOW wabara kahtaan faby na wengineo
 
Last edited by a moderator:
Mnyonge mngeni lakini haki yake mpeni, miaka ya nyuma wala sio nyuma sana, kwenda sekondari ilikuwa ni ndoto achilia vyuoni, lakini sasa angalau watu wana fika nakupata elimu, barabara hakuna ubishi, japo wanasema ni zimejengwa na mikopo ya wahisani mie silijari hilo, wanasema elimu ni kiwango cha chini, lakini ni bora kuliko kuikosa,kama tatizo ni ajira vyuoni sasa wanafundisha ujasiriamali, unaweza kuanza na biashara ndogo lakini ukazalisha ajira yawengine hata kama ni m1 au wawili, yapo makosa yamefanyika lakini tushukuru kwa hayo mazuri, wapo viongozi walioingia kwa democrasia lakini wakang'ang'ania madaraka, tumshukuru jk kwa mazuri aliyotufanyia, na yale mabaya yawe changamoto kwa kiongozi ajaye, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni,
 
We Tahira unalazimika hata kama hutaki bara×2 huzioni? uhuru wa kujieleza si huu kwa mfano, na kuuita wewe tahira.

Ukweli ni kwamba,Baba wa Barabara ni Mkapa.Kikwete amekopa sana na tutalipa sana kufidia Madeni aliyotusababishia.Kama kweli kuna uhuru wa Kujieleza mpaka kutukana bila kuchukuliwa hatua,huo ni Udhaifu na sio Sifa za Uongozi Bora.
 
Tren ya mwakyembe.
daraja la kigamboni.
mabasi yaendayo kasi.
kasi ya utumaji na upokeaji fedha kwa mitandao ya simu( enzi zile ukitaka kutuma fedha uende posta lakin sasa hata ucku mambo poa).
Intanet kwenye simu. tunasoma magazeti mapema hata ukiwa kijijini
Umeme vijijini
Mabasi yaendayo kasi.
Fastjet mara 4 kwa siku. dar/ mbeya unagusa tu.
Tumemchapa m23 katulia. ngara kigoma tulii.

Hivi una akili kweli wewe ? Kwa hiyo Kikwete ndo kaleta Fastjet na M pesa ?
 
Mheshimiwa Rais wa JMT akiwa anahojiwa na mwandishi wa habari mwandamizi kutoka Nation media group aliulizwa swali je anategemewa utawala wake kukumbukwa kwa yapi ,Jk alijibu kama ifuatavyo:

Wanamama watalia sana na watamkumbuka sana. Mpaka manesi ni wakuu wa mikoa etc! Historia chafu !
 
Ukweli ni kwamba,Baba wa Barabara ni Mkapa.Kikwete amekopa sana na tutalipa sana kufidia Madeni aliyotusababishia.Kama kweli kuna uhuru wa Kujieleza mpaka kutukana bila kuchukuliwa hatua,huo ni Udhaifu na sio Sifa za Uongozi Bora.
.
Farudume heshima kwako mkuu, kwanza kukopa si tatizo kama anautumia mkopo vizuri kwa maendeleo ya nchi na sema akope tu hata deni la taifa lifikie 100trillion only.

Tuna raslimali kibao za kulipia huo mkopo. Deni la taifa litamfanya rais ajaye awajibike kulilipa na huku akilazimika kudumisha na kuboresha yale mazuri yaliyo achwa na Kikwete.

Pia deni la taifa litasaidia kuwa elewa wanaoutaka urais kama wanania ya kweli ya kuitumika nchi na wala si kujitajirisha? Maana yake hakika rais ajaye wa nchi hii atalazimika kulitumikia deni hata kama hataki kuwa tumikia wananchi.

Big up mh rais Kikwete ongeza deni kwa kuleta maendeleo na kumuachia mrithi wako mazingira ya kuwajibika, ama apende au asipende lazima atalilipa hili deni.

Au ni seme hivi sifa ya Nyerere ni mazingira aliyo ya acha, sifa ya Mwinyi inatokana na mazingira aliyo rithi kutoka kwa Nyerere. Sifa ya Nkapa inatokana na mazingira aliyoachiwa na Mwinyi. Sifa ya Kikwete inatokana na mazingira aliyo rithi kutoka kwa Nkapa.nk, nk.

Hili la kutukana ni mazingira niliyowekewa yalinilazimisha kujibu mapigo tuvumiliane tu.
 
Katika zile ajira milion moja,amenipa na mimi,ila miaka 10 ya JK nimeshuhudia uozo wa watendaji wake ambao wengi wana viburi,kebehi na dharau sana,nimeshuhudia ameingia kukiwa na kasi ya ujambaz na anaondoka kukiwa na kasi ya ujambaz mijini na vijijini,pia mfanyakaz kutokuwa na thaman ila mwanasiasa kuwa na thamani ya hali ya juu,chini ya JK nimeshuhudia rushwa ikitamalaki kwa kiasi kikubwa sana rushwa kubwa na ndogo,,,,,kwenye chaguz za kisiasa ikiwemo,pia nimeshuhudia taasisi ya urais makanjanja wakiitumia kwa deal mbalimbali like ile ya malaria ambayo watu waliililia sana,pia kaul za mipashooo za ile kurugenz yetu,,,maskin mpaka mzee wa watu akaitwa MNAFKI
 
Mimi nitamkumbuka kama rais muwazi zaidi kwa watu wake,mf.
1.Amekuwa wazi kuwa hajui kwa nini nchi yake ni masikini
2.Amekuwa wazi kuwa wanafunzi wanapata mimba kwa sababu ya kiherehere chao
3.Amekuwa wazi kuwa anawajua wauza madawa ya kulevya kwa majina
4.Amekuwa wazi kuwajua majangili na kiongozi wao aishie Arusha.
Mnyonge mnyongeni ila haki yake ya UWAZI mpeni!!!!
 
Pia amesema haya nanukuu, 'kwamba habari za kuchochea majeshi kufanya mapinduzi, habari za kuchochea vijana kuleta vurugu hatazivumilia, na kwamba chombo cha habari kitakachojielekeza kwenye habari za namna hiyo kitafungiwa.

“Wakiandika Rais Kikwete nchi imemshinda hainipi tabu, kwa kuwa najua nchi haijanishinda,” alisema Rais Kikwete huku akitoa mfano wa namna redio Mille Collines ya Rwanda ilivyochangia mauaji ya halaiki nchini humo.

Sasa inamaana hajamsikia Waziri wake Lukuvi na wale Wajumbe waliowengi wakitoa kauli za ubaguzi?Au akiwaCCM anaongea ni sawa ukiwa mpinzani then cha moto utakipata.Je hiyo ndiyo haki tunayoongela?
 
Kwa vile nilimtia mmko hadharani ndo maana waniita tahira? Ama??!!!

Kwa kuandika hivi na amini umejifunza kitu, siku nyingine utatafakari kabla ya kutukana wengine. Sasa hivi nimekupuuza najua umeelewa kwa kuumia hata kama hutaki kuukubali ukweli huo.
 
Mimi nitamkumbuka kama rais muwazi zaidi kwa watu wake,mf.
1.Amekuwa wazi kuwa hajui kwa nini nchi yake ni masikini
2.Amekuwa wazi kuwa wanafunzi wanapata mimba kwa sababu ya kiherehere chao
3.Amekuwa wazi kuwa anawajua wauza madawa ya kulevya kwa majina
4.Amekuwa wazi kuwajua majangili na kiongozi wao aishie Arusha.
Mnyonge mnyongeni ila haki yake ya UWAZI mpeni!!!!

Hamaanishi kuwa hajui, maana yake ni kuwa "haoni sababu ya msingi unayoweza ukamweleza mtu mwenye akili timamu kwa nini Tanzania ni maskini, na akakuelewa. Hata mimi mwenyewe sijui kwa nini sisi ni maskini. Kama wewe unajua, the meaning behind ni kwamba unajua sababu ambazo ni za msingi ambazo zinatufanya sisi tuendelee kuwa maskini, na kama sababu za msingi zipo, maana yake ni kwamba tunastahili kuwa maskini, na hatutakiwi kulaumiwa na mtu yeyote au kujilaumu sisi wenyewe. Nikupe mfano mdogo, uko na uwezo mzuri nyumbani kwako kimaisha halafu majambazi wakaja nyumbani kwako wakapora kila kitu na kukuacha maskini, baada ya hapo utakuwa una sababu ya msingi kabisa asilimia 100 ya kumweleza mtu kwa nini wewe ni maskini. Lakini kama ulikuwa na maisha mazuri ukaja ukaishiwa sababu ya ulevi wa pombe, je ukishakuwa maskini kwa staili hii, utakuwa na sababu yeyote kweli ya msingi ya kumweleza mtu kwa nini wewe ni maskini na akakueleewa? Unless ni chizi.

Nchi yetu Tanzania ni maskini kwa sababu ambazo hata mimi sizielewi na haitatokea siku nikaja nikazielewa, au labda pengine wewe unayezielewa utueleze ni zipi?
 
Huyu ni baba wa taifa wa miundo mbinu(bara×2) na uhuru wa kujielezea mengine mtaongezea. Hapa si hiari tuna lazimika kumpa hii sifa hata kama hututaki.
Semeni yote yake kuu ni Yeye kuwa mtalii duniani, kukithiri kwa mikataba mibovu na uchakachuaji uliokithiri, ubomoaji na ujenzi wa serikali bila kusahau kushuka kwa kiwango cha elimu mfululizo na kupandisha idadi ya wasiojua kusoma na kuandika toka 7% mwaka 2002 na kufikia 33% mwaka 2012.
 
Back
Top Bottom