Jiwe laporomoka na kuua wanne Mwanza

Jiwe laporomoka na kuua wanne Mwanza

Rock City
ni rock city ya ukweli ila miundombinu sasaaaaa ndo kasheshe
Limefika funzo inabidi tuyaangaze yetu macho
 
Kuna member mmoja alikuja na thread yake hapa,alipofika Mwanza na kuyaona hayo mawe akatoa tahadhari lakini cha ajabu watu wa Mwanza wengi walimkejeli humuhumu.Mods irudisheni ile thread maana kinga ni bora kuliko tiba.Poleni sana wafiwa na R.I.P mliotangulia mbele za haki.
 
Yamebakia na Yale ya Nyakabungo kule ndo yatawaua kama nzige!
Just the matter of time.
 
acheni kuwaona wajinga.ni mazingira wamezaliwa na kuyakuta.kwani miaka yote serikali haiwaoni wamekosea kujenga milimani?
 
Vilio na simanzi jana vilitawala kwa wakazi wa maeneo ya Sinai-Mabatini, baada ya vifo vya watu wanne wa familia mbili tofauti, vilivyotokana na mvua iliyosababisha miamba mikubwa ya mawe kuporomoka na kuponda nyumba zao usiku wa manane.

Tukio hilo la kusikitisha limeripotiwa kutokea saa nane usiku kuamkia jana, wakati mvua iliyoambatana na upepo wa wastani ilipokuwa ikiendelea kunyesha, na kusababisha miamba hiyo mikubwa inayokadiriwa kufikia tani mbili kuporomoka na kuziponda nyumba hizo na kusababisha vifo hivyo na majeruhi wanne.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentino Mlowola, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari wakati wa mvua.

Mpekuzi ilifanikiwa kufika eneo la tukio na kushuhudia miamba hiyo ikiwa imeharibu nyumba, huku nyumba moja iliyojengwa kwa matofali ya tope ikiwa imeanguka na kubaki kifusi.

Nyumba zilizokumbwa na maafa hayo zinamilikiwa na watu waliotajwa kwa majina ya Joseph William na Lameck Ajiji, na kila moja watu wawili wamefariki kwa kukandamizwa na miamba hiyo.

Katika nyumba ya William iliyokuwa na watu watano, waliofariki wametajwa kuwa ni Kefa Joseph (15) na Emmanuel Joseph (12), wote wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbugani na majeruhi mmoja ambaye hakufahamika jina lake ambaye alikimbizwa hospitali.

Nyumba inayomilikiwa na Ajiji yenye watu watatu, waliofariki wametambuliwa kuwa ni mama wa nyumba hiyo, Kwinta Geko (24) na mumewe Samson Odinya.

Waliojeruhiwa ni mtoto Bety Samson (4) na Godfrey Joseph (14) mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mbugani.

Tukio hilo ni la pili kutokea katika eneo hilo la Sinai. Mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2009 baada ya miamba kuporomoka na kusababisha vifo vya watu wawili wa familia moja.

Tukio la jana lilivuta hisia tofauti kwa wakazi wa Jiji la Mwanza, huku wengine wakiangua vilio.

Mamia ya wananchi waliofika eneo hilo, walijitolea kwa kumpa fedha mtoto Bety aliyenusurika kufa kutokana na tukio hilo.

Mbunge wa Nyamagana jijini Mwanza, Ezekiel Wenje (Chadema), alifika eneo la tukio na kutoa pole kwa wananchi, ndugu jamaa na marafiki wa familia zilizoathirika na janga hilo, ambapo alionyesha kushtuka baada ya kuelezwa na wananchi kwamba hakuna kiongozi yeyote wa Serikali aliyefika eneo hilo.

Akizungumza kwa kutumia kipaza sauti mbele ya umati wa watu waliokuwa wamefurika katika eneo hilo la tukio, alisema: "Inashangaza sana kuona hata mkuu wa wilaya hajafika hapa. Nitawasiliana na viongozi wa Serikali na mchana nitarudi hapa tena."

Baadhi ya wananchi waliozungumza na Mwandishi katika eneo la tukio, waliiomba Serikali kuzuia wananchi kujenga karibu na miamba mikubwa, kwani kufanya hivyo itasaidia sana kuepusha maafa kama hayo.

"Kwa kweli tukio hili linasikitisha sana, na tunaomba viongozi wa serikali wasaidie wananchi kuwaondosha kwenye maeneo ya kwenye miamba," alisema mmoja wa wananchi hao ambaye pia ni balozi wa Shina Namba Tano, Mtaa wa Nyerere A, Jackson Kitundu.
 
kweli ID yako kiboko jina la USED COUNTRY NEW PEOPLE
ww unaweza kulala kwene Reli ukipaona salama? ww unaweza kupumzika kwenye kinywa cha mamba ukidhani hatakufunga?
Tafadhali usijenge kwenye maporomoko au mafuriko ukisema hakuna kitakachotokea
MUNGU kasema jilinde nami nitakulinda

hapo pekundu nnaomba kwenye msaafu au biblia unionyeshe haya maandiko!
 
ipo zaidi ya mistari 100 inayomaanisha hivyo na nimeiweka katika post # 35
Pia uwe unahudhuria mafundishao km ya kina Gwajima, Mzee wa UPAKO KAKOBE na hata wachugaji
Kwa hiyo tafsiri ya Neno kwa Neno
anza na hili WAULINDAO MJI BILA BWANA WAKESHA BURE
chochote ukifanyacho uwe na Imani na bwana atakuwa nawe
kama ni fundi mchundo, dereva abiria JILINDE KWANZA
sio unajenga kwenye maporomoko ukitegemea kulindwa au kwenda kuiba ukaanza kusali ni 30% kufanikiwa
 
picha zake zinatisha,kuna mmoja alifumuliwa kichwa
 
Hamuwezi kubishana na ukweli. Cku yako ikifika imefika. Vifo vingi hutokea in a mysterious way such that it is hard to explain why it couldnt have been prevented... Msitake tuamini kuwa nguvu za giza zimetumika kudondosha huo mwamba!

mark-twain-fooled.jpg
 
Kuna member mmoja alikuja na thread yake hapa,alipofika Mwanza na kuyaona hayo mawe akatoa tahadhari lakini cha ajabu watu wa Mwanza wengi walimkejeli humuhumu.Mods irudisheni ile thread maana kinga ni bora kuliko tiba.Poleni sana wafiwa na R.I.P mliotangulia mbele za haki.

nakumbuka huyo member alisema chumbani alipolala kulikuwa na bonge la jiwe basi hata usingizi akawa hapato....
 
Vilio na simanzi jana vilitawala kwa wakazi wa maeneo ya Sinai-Mabatini, baada ya vifo vya watu wanne wa familia mbili tofauti, vilivyotokana na mvua iliyosababisha miamba mikubwa ya mawe kuporomoka na kuponda nyumba zao usiku wa manane.

Tukio hilo la kusikitisha limeripotiwa kutokea saa nane usiku kuamkia jana, wakati mvua iliyoambatana na upepo wa wastani ilipokuwa ikiendelea kunyesha, na kusababisha miamba hiyo mikubwa inayokadiriwa kufikia tani mbili kuporomoka na kuziponda nyumba hizo na kusababisha vifo hivyo na majeruhi wanne.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentino Mlowola, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari wakati wa mvua.

Mpekuzi ilifanikiwa kufika eneo la tukio na kushuhudia miamba hiyo ikiwa imeharibu nyumba, huku nyumba moja iliyojengwa kwa matofali ya tope ikiwa imeanguka na kubaki kifusi.

Nyumba zilizokumbwa na maafa hayo zinamilikiwa na watu waliotajwa kwa majina ya Joseph William na Lameck Ajiji, na kila moja watu wawili wamefariki kwa kukandamizwa na miamba hiyo.

Katika nyumba ya William iliyokuwa na watu watano, waliofariki wametajwa kuwa ni Kefa Joseph (15) na Emmanuel Joseph (12), wote wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbugani na majeruhi mmoja ambaye hakufahamika jina lake ambaye alikimbizwa hospitali.

Nyumba inayomilikiwa na Ajiji yenye watu watatu, waliofariki wametambuliwa kuwa ni mama wa nyumba hiyo, Kwinta Geko (24) na mumewe Samson Odinya.

Waliojeruhiwa ni mtoto Bety Samson (4) na Godfrey Joseph (14) mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mbugani.

Tukio hilo ni la pili kutokea katika eneo hilo la Sinai. Mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2009 baada ya miamba kuporomoka na kusababisha vifo vya watu wawili wa familia moja.

Tukio la jana lilivuta hisia tofauti kwa wakazi wa Jiji la Mwanza, huku wengine wakiangua vilio.

Mamia ya wananchi waliofika eneo hilo, walijitolea kwa kumpa fedha mtoto Bety aliyenusurika kufa kutokana na tukio hilo.

Mbunge wa Nyamagana jijini Mwanza, Ezekiel Wenje (Chadema), alifika eneo la tukio na kutoa pole kwa wananchi, ndugu jamaa na marafiki wa familia zilizoathirika na janga hilo, ambapo alionyesha kushtuka baada ya kuelezwa na wananchi kwamba hakuna kiongozi yeyote wa Serikali aliyefika eneo hilo.

Akizungumza kwa kutumia kipaza sauti mbele ya umati wa watu waliokuwa wamefurika katika eneo hilo la tukio, alisema: "Inashangaza sana kuona hata mkuu wa wilaya hajafika hapa. Nitawasiliana na viongozi wa Serikali na mchana nitarudi hapa tena."

Baadhi ya wananchi waliozungumza na Mwandishi katika eneo la tukio, waliiomba Serikali kuzuia wananchi kujenga karibu na miamba mikubwa, kwani kufanya hivyo itasaidia sana kuepusha maafa kama hayo.

"Kwa kweli tukio hili linasikitisha sana, na tunaomba viongozi wa serikali wasaidie wananchi kuwaondosha kwenye maeneo ya kwenye miamba," alisema mmoja wa wananchi hao ambaye pia ni balozi wa Shina Namba Tano, Mtaa wa Nyerere A, Jackson Kitundu.
Poleni wakazi wa Mwanza.
 
ipo zaidi ya mistari 100 inayomaanisha hivyo na nimeiweka katika post # 35
Pia uwe unahudhuria mafundishao km ya kina Gwajima, Mzee wa UPAKO KAKOBE na hata wachugaji
Kwa hiyo tafsiri ya Neno kwa Neno
anza na hili WAULINDAO MJI BILA BWANA WAKESHA BURE
chochote ukifanyacho uwe na Imani na bwana atakuwa nawe
kama ni fundi mchundo, dereva abiria JILINDE KWANZA
sio unajenga kwenye maporomoko ukitegemea kulindwa au kwenda kuiba ukaanza kusali ni 30% kufanikiwa

Du!? Ya kweli haya!
 
nduguyangu haiko mbali ukipandisha ikulu ndgo, mtaa wa forest walk pale kwa Muhenne geti jeupe.. hapo pembeni kuna jumba la mzunu. uliziepo ! wasalimiee..

Mkuu kibanda chako kiko salama salimini... Ila Lile jiwe naona linatikisika likipulizwa upepo so fanya mpango wa kuhamisha ile nyumba otherwise hesabu maumivu
 
Lol, wapangaji wamegoma kuondoka, wasema watafiyemo humo'umo !! Sasa tutawaokowajee ?:help:
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom