Jiwe laporomoka na kuua wanne Mwanza

Jiwe laporomoka na kuua wanne Mwanza

Labda uongelee umri. Naamini kielimu mimi ni Professa kwako. Kimazingira, pia naamini mimi ni headmaster kwako. Nimeshazunguka nchi za mabara yote isipokuwa nchi moja tu inaitwa Greenland... Kwa hiyo unapaswa unipe fulll respect.

Sawa kabisa Prof.and full respect to you. Ebu turudi kwenye mada sasa ni kweli unaamini mawe haya ya Mwanza yaliyopandiliana hayawezi poromoka?
 
Yote sawa lakini la Mungu kasema umechapia. Usimsingizie, Hajawahi kusema hivyo. Leta andiko.

Za week end lakini?

kweli ID yako kiboko jina la USED COUNTRY NEW PEOPLE
ww unaweza kulala kwene Reli ukipaona salama? ww unaweza kupumzika kwenye kinywa cha mamba ukidhani hatakufunga?
Tafadhali usijenge kwenye maporomoko au mafuriko ukisema hakuna kitakachotokea
MUNGU kasema jilinde nami nitakulinda
 
Mkuu hujui kuwa hata miamba kwa sababu ya mvua,jua,mda unavyoenda inakuwa inalika taratibu hivo kusababisha hatari zaidi! Siyo mara ya kwanza mawe kuporomoka Mwanza,nishawahi kukuta jingine limeporomoka maeneo ya Mahina na bahati nzuri halikufika kwenye makazi ya watu hivo halikuleta madhara.

Kusema siku ikifika imefika ni sawa lakini kwanini uifanye ifike kwa kupuuza hatari iliyopo wakati ukijua kabisa u-kwenye mazingira hatarishi! Walosema tahadhari i nzuri kuliko tiba wala hawakukosea mkuu.

Mkuu tatizo la mawe kuleta madhara Mwanza alijaanza leo wala jana. Nakumbuka nikiwa Form I Mwanza kuna mzee mmoja wa Kikurya alikuwa anachimba jiwe ili atengeneze uwanja wa kujenga nyumba pale juu kidogo ya shule ya msingi Mkuyuni (wakati ule ikiitwa Igogo shule ya msingi). Alikwenda upande wa juu na kujaribu kulisukuma lakini alikusogea, ikabidi arudi upande wa chini kuchimba tena kumbe lilikuwa limeishakuwa tayari kupomoromoka. Liliporomoka na yule bwana alichoweza kufanya ni kukimbiza kichwa lakini kuanzia kiunoni mpaka miguu vyote vilifunikwa na jiwe.

Asante kwa kazi nzuri ya fire brigade waliokuja na vifaa na jeki na kamba zilizosaidia kuliinua jiwe. Mzee alikatwa miguu yote miwili.

RIP waliokufa kwa kuporomokewa na mawe.

Tiba
 
Katika hali ya kusikitisha,Leo usiku mvua iliyonyesha jijini mwanza ikiambatana na upepo mkali imesababisha watu WANNE kufa baada ya mawe yaliyokuwa karibu na nyumba kuporomoka na kuwakandamiza ndani ya nyumba.

Tukio hilo limetokea eneo la Mabatini mwanza.

Kazi ya Mungu Haina makosa.
 
Labda uongelee umri. Naamini kielimu mimi ni Professa kwako. Kimazingira, pia naamini mimi ni headmaster kwako. Nimeshazunguka nchi za mabara yote isipokuwa nchi moja tu inaitwa Greenland... Kwa hiyo unapaswa unipe fulll respect.

Mkuu, inaelekea Jiografia unaifahamu sana, hivi umeishi miaka mingapi pale?
 
Heshima kwenu.

Kufuatia mvua zilizonyesha jana usiku maeneo ya SINAI Mwanza kuna jiwe limeporomoka na kuua watu wanne.
Kama tujuavyo watu wengi wamejenga kwenye milima na chini ya mawe yanayoninginia.
Poleni sana jamani
 
Katika hali ya kusikitisha,Leo usiku mvua iliyonyesha jijini mwanza ikiambatana na upepo mkali imesababisha watu WANNE kufa baada ya mawe yaliyokuwa karibu na nyumba kuporomoka na kuwakandamiza ndani ya nyumba.

Tukio hilo limetokea eneo la Mabatini mwanza.

Kazi ya Mungu Haina makosa.

Mbona nimesikia kuwa ni maeneo ya Kirumba au matukio mawili tofauti!

R.I.P. Marehemu wa maporomoko.
 
Tena ni mwezi uliopita tu kulikuwa na uzi kuhusu mwanza na ujenzi juu/chini/pembeni/katikati/ya majabali.Baadhi ya wadau hasa wa mwanza walibisha na kushupaza mishipa ya shingo kama wala pilipili kichaa.Haya ndo matokeo yake.Mbeleni inaweaza kuwa very delicate kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.TAHADHARI ICHUKULIWE NA WANAOISHI HUMO,KWANI MWANZA INA MAENEO MAKUBWA kama igombe,kisesa,usagara mpaka misungwi,eneo baada ya kuvuka kamanga feri,maeneo baada ya air port n.k
 
Tanzania wengi tunaishi kwa neema tu.., sehemu nyingi sana Mwanza siku ikitokea tetemeko au kama ule udongo ulivyofunika watu kule Kampala (wengi tutakufa..)

By the way hata ndugu zetu wa kule Kilimanjaro nadhani ule mlima volcano yake ni dormant kuna siku au time yoyote inaweza ikafurukuta
 
Tabby huki Kitabu ni kikubwa sana ukianza kufuatilia kila nukta hasa ya neno jilinde utachapia mengi kwani gawa wenzetu kukesha kwenye milima ya mawe bila BWANA WATAKESHA BURE
1 Samweli 30 soma Daud alivyowapiga Waameleki

Kaa ufahamu kuwa Vita vyote vya zamani MUNGU aliwalinda wapiganaji wake na mifano mingi

  • ZABURI 31;19 - 20 Jinsi gani ulivyo mwingi wema wako,uluowawekea wale wanaokucha! wanaokimbilia usalama kwako wawapa mema binadamu wote wakiona 20. Wawaficha mahali salama katika ulinzi wako mbali na ubishi wa adui zao.
  • Zaburi 23 Mpendeni Mwenyezi Mungu enyi watakatifu wake wote. Mwenyezi Mungu huwalinda watu watakatifu, lakini huwaadhibu kabisa wenye kiburi wanavyostahili
  • Zauri 24 Muwe hodari na kupiga moyo konde enyi nyote mnaomtumainia Mwenyezi Mungu

Hebu waambie hao watu wa Milimani huko Mwanza wasijenge chini ya jiwe litakaloporomoka wakitarajia KULINDWA
 
wana jf msaada naombeni mwenye picha za tukio lala jiwe lililo uwa watu wanne mwanza
 
Nikama utabiri uliotimia
hivi majuzi familia ilikubwa na mkasa Wa aina yake pale jiwe lilipo toka mlimani na kufunika nyumba ndani yake kukiwa na baba mama na watoo
Waokozi walibaki kinywa wazi wasijue la kufanya kwani jiwe ni kuuubwa miundombinu hakuna ilikuwezesha mashine ya kusukumia jiwe hilo kuwa kupita
na kufanya ulipuaji ndo hataaari zaidi
poleeeeni wana Mabatini poleni Mwanza poleni wafiwa Kwa ajali ya kuangukiwa na jiwe
 
Walifariki wangapi?
Majeruhi jee?
Picha lini!

Bwana Ametwaa,jina la Bwana lihimidiwe.
 
Poleni sana wafiwa wote. Hili janga ni la kusikitisha sana maana pale mabatini eneo la tukio hakuna miundo mbinu kama alivyisema mtoa mada. Mpaka sasa sijapata taarifa kuwa jiwe lilitolewa ama namna gani. Inatia huruma sana. Mwenyezi Mungu amjalie mtoto aliyenusurika aendelee kuishi na awe na afya njema. May their soul R.I.P.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom