Jiwe laporomoka na kuua wanne Mwanza

Jiwe laporomoka na kuua wanne Mwanza

Marire

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2012
Posts
12,333
Reaction score
5,314
Screen-Shot-2014-08-19-at-9.06.36-AM1.png


Heshima kwenu.

Kufuatia mvua zilizonyesha jana usiku maeneo ya SINAI Mwanza kuna jiwe limeporomoka na kuua watu wanne.
Kama tujuavyo watu wengi wamejenga kwenye milima na chini ya mawe yanayoninginia.
==================================


Watu watatu akiwemo mtoto mdogo wameumizwa vibaya mara baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba kwaa jiwe lililoporomoka kutoka mlimani jijini Mwanza.

Waliokumbwa na ajali hiyo ni Bw. Msalam Husein ambaye ni dereva (30) na mkewe Bi. Nadia Grecian ambaye ni mama wa nyumbani (25) pamoja na kichanga wao Asfati Mslam (aliyechini ya umri wa mwaka).

Tukio hilo limetokea leo hii majira ya saa 6:00 mchana katika nyumba wanayoishi kilima cha Sabato mtaa wa Ngara eneo la Mlimani B Kirumba jijini Mwanza ambapo pamoja na kwamba ni majira ya mchana watu hao mke na mume walikuwa wamejipumzisha kitandani, (yawezekana kutokana na hali ya hewa kwa mvua inayoendelea kunyesha leo tangu asubuhi hadi muda huu tunakupa taarifa) ndipo wakakutana na ajali hiyo.

Mtoto Asfati Mslam alifariki dunia jana majira ya saa 9 na dakika kadhaa za alasiri katika hospitali ya mkoa wa Mwanza, Sekou Toure alikokimbizwa yeye na wazazi wake mara baada ya kuumizwa vibaya kwa kuangukiwa na ukuta wa nyumba yao kupitia mawe yaliyoporomoka kutoka kwenye msingi wa nyumba iliyo eneo la juu mlimani jijini Mwanza. Mtoto Asfati Mslam amezikwa kwenye makaburi ya Waislamu ya Ngara Kirumba eneo la Mlimani B.

Chanzo: Michuzi

Screen-Shot-2014-08-19-at-9.04.53-AM.png


Screen-Shot-2014-08-19-at-9.05.00-AM.png

Screen-Shot-2014-08-19-at-9.05.07-AM.png


Screen-Shot-2014-08-19-at-9.05.16-AM.png


Screen-Shot-2014-08-19-at-9.05.46-AM.png
 
Poleni kwa msiba kakini kwa mwanza watu wengi wapo hatarini hasa kama kutatokea tetemeko la ardhi.
 
Ck yako ikifika imefika. Hayo mawe yamekuwako hivyo kwa mamilioni ya miaka ndio yaje kudondoka leo?
 
Pole sana mbwiga wangu, unapotolewa ushauri fikiria kwa kina then take action. Mnapenda kuishi kwa mazoea yanapotokea maafa lawama zote zinaenda kwa serikali, kumbe matokeo yake ni ukilaza wenu, ongea na wenzako wa mabondeni na maafa yanayo wakuta lakini bado ni ngumu kwao kuelewa somo, kalaga baho.
 
Ck yako ikifika imefika. Hayo mawe yamekuwako hivyo kwa mamilioni ya miaka ndio yaje kudondoka leo?

Mkuu hujui kuwa hata miamba kwa sababu ya mvua,jua,mda unavyoenda inakuwa inalika taratibu hivo kusababisha hatari zaidi! Siyo mara ya kwanza mawe kuporomoka Mwanza,nishawahi kukuta jingine limeporomoka maeneo ya Mahina na bahati nzuri halikufika kwenye makazi ya watu hivo halikuleta madhara.

Kusema siku ikifika imefika ni sawa lakini kwanini uifanye ifike kwa kupuuza hatari iliyopo wakati ukijua kabisa u-kwenye mazingira hatarishi! Walosema tahadhari i nzuri kuliko tiba wala hawakukosea mkuu.
 
Kweli wewe ni mbwiga.

Hivi unatambua kuwa yalikuwepo tangu awali kabla maeneo hayo kuchimbwa ama kubadilishwa uasili wake? Hivo kutokana na ongezeko la watu na mahitaji ya ardhi maeneo mengi yamechimbwa
 
Hivi unatambua kuwa yalikuwepo tangu awali kabla maeneo hayo kuchimbwa ama kubadilishwa uasili wake? Hivo kutokana na ongezeko la watu na mahitaji ya ardhi maeneo mengi yamechimbwa

Ulitaka kusema nini hapa!
 
Hamuwezi kubishana na ukweli. Cku yako ikifika imefika. Vifo vingi hutokea in a mysterious way such that it is hard to explain why it couldnt have been prevented... Msitake tuamini kuwa nguvu za giza zimetumika kudondosha huo mwamba!
 
Hamuwezi kubishana na ukweli. Cku yako ikifika imefika. Vifo vingi hutokea in a mysterious way such that it is hard to explain why it couldnt have been prevented... Msitake tuamini kuwa nguvu za giza zimetumika kudondosha huo mwamba!

Umri,elimu na mazingira ukiachilia mbali asili ya ubishi tu kwa baadhi ya watu vinaweza kuwa vigezo vya mtu kuwa mbishi tu hata kama hana pointi za kusapoti hoja yake.
 
Ck yako ikifika imefika. Hayo mawe yamekuwako hivyo kwa mamilioni ya miaka ndio yaje kudondoka leo?
kweli ID yako kiboko jina la USED COUNTRY NEW PEOPLE
ww unaweza kulala kwene Reli ukipaona salama? ww unaweza kupumzika kwenye kinywa cha mamba ukidhani hatakufunga?
Tafadhali usijenge kwenye maporomoko au mafuriko ukisema hakuna kitakachotokea
MUNGU kasema jilinde nami nitakulinda
 
Hivi unatambua kuwa yalikuwepo tangu awali kabla maeneo hayo kuchimbwa ama kubadilishwa uasili wake? Hivo kutokana na ongezeko la watu na mahitaji ya ardhi maeneo mengi yamechimbwa

Ni sawa lakini haina maana watu wabweteke bila tahadhari huku wakiona mabadiliko ya tabia ya nchi na athari zake kwa uhai. Wakifa waseme siku imefika ama uchawi kwa sababu hayo mawe tangu zamani yapo. Na isitoshe, mara ngapi mawe ya Mwanza yamewahi kuporomoka na mengine kuvingirikia ziwani?

Ni sawa na wa kongo wanaambiwa waache kula kima kwa kuwa sasa zina maambukizi ya ebola, wanabisha na kusema siyo kweli kwa kuwa wamekula vima miaka yote na hawakuwahi kupata hiyo ebola, na kuahidi kuendelea kula tu.


Sawa na masai anayesema wao kutembea na wanawake wengi ni jadi na hawakuwahi kupata ukimwi. "..Ukimwi iko huko mjini haiwesi fika kwenye boma setu.."
 
Wakome,wao ndio wameenda kuya disturb, mtu una akili timamu unajenga nyumba, juu kidogo kuna jiwe la tani mia mbili na kila siku unachimbua na kusababisha mmomoNYOKO
 
umri,elimu na mazingira vinaweza kuwa vigezo vya mtu kuwa mbishi tu hata kama hana pointi za kusapoti hoja yake.

Labda uongelee umri. Naamini kielimu mimi ni Professa kwako. Kimazingira, pia naamini mimi ni headmaster kwako. Nimeshazunguka nchi za mabara yote isipokuwa nchi moja tu inaitwa Greenland... Kwa hiyo unapaswa unipe fulll respect.
 
Hoja zinazoshauri kutojenga kwenye maeneo yasiyofaa kama mabondeni na kwenye uwezekano wa maporomoko ya mawe una busara kubwa. Nisichokielewa na sikubaliani nacho ni nadharia ya mungu kasema jilinde nitakulinda
Ni Mungu yupi huyo ? Maana kuna MUNGU na miungu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom