Jipe moyo Kafulila; Hongera NCCR-Mageuzi, Godbless Lema

mawazo yangu lile jimbo ni la mwenyewe kafulila so hata kama akienda chama chochoye atashinda 2 mi naona arudi kwa baba yake DR SLAA coz mtoto kwa baba hakui

ni mawazo 2
 
Nimependa hapo, hata kama unampenda vipi mkeo, huwezi kumsaidia kubeba mimba. Kafulila anampenda sana Zitto, anataka amsaidie kubeba mimba yake ya urais 2015. Kitu ambacho hakiwezekaniki. Safi sana kamanda LEMA
 
Naunga mkono maandiko ya Lema, sitashangai kuona watu wakimpinga Lema kwani uwezo wa kuelewa unatofautiana.
Pamoja na tofauti zetu katika kuelewa au kupingana ni vizuri ukapinga kwa vielelezo kuliko kuishia kulalamika tu au kusema UPUPU, leta ufahamu mbadala uujuao wewe ili nasi tuuone huo upupu....
 
i)Nidhamu bila UHURU ni UTUMWA. Kama tunaweza kuwaambia Rais, Waziri Mkuu, mawaziri, Spika wa Bunge, n.k. kwamba uongozi wao ni dhaifu, hadharani na mbele ya kadmnasi, viongozi wa vyama vya siasa wanapata wapi utukufu wa kujifanya kwamba hawawezi kusemwa nje ya vikao? Viongozi wa vyama vya siasa ni viongozi wa umma na hawawezi kuficha udhaifu wao katika mwamvuli wa nidhamu.

ii)Maamuzi ya chama cha siasa chochote makini lazima yazingatie maslahi mapana ya kisiasa na kijamii kwa sababu chama cha siasa sio kitengo cha mahakama. Mahakama ina haki na wajibu wa kuchukua maamuzi yeyote madamu yamezingatia sheria zilizopo kwa wakati huo hata kama maamuzi hayo ni ya ovyo.Jambo hili haliwezi kufanywa na chama cha siasa makini cha watu.
iii)Vyama vya siasa vipo kwa lengo la kukuza demokrasia. Msingi wa demokrasia ni UHURU WA KUTOA maoni. Kama vyama vya siasa vitatumika kuziba watu midomo kwa kisingizio cha kulinda nidhamu ya chama vitakuwa vinaua demokrasia.

iv) Siamini,na haitatokea niamni, kwamba kumkosoa kiongozi yeyote hadharani ni utomvu wa nidhamu.

NIdhamu ni jambo la msingi mahala popote pale. Uhuru usiyo kuwa na nidhamu si uhuru bali ni ujinga. Kukosoa serikali hadharani ni wajibu wa vyama vya upinzani ili serikali ipunguze makali kwa wananchi na uhuru huwo huwo usisababisha kukosekana kwa nidhamu ndani ya vyama. Utawezajemkuikosa serikali wakati umekosa nidhamu ndani ya chama chako? Nidhamu lazima ianze ndani kwako ndiyo utoke na kupaza sauti kwa wanaopindisha ukweli! Mimi binafsi sijafurahishwa kwa kafulila kuvuliwa uanachama wala sichekelei maamuzi hayo. Ila kwasababu ya kujenga msingi bora ni lazima nidhamu izingatiwe umaarufu usifanyike kama mtu mmoja ni zaidi ya taasisi.

MUNGU mpe kafulila moyo wa subiri awezekuzivuka changamoto hizzi. Na sikuhama chama chake bado ananafasi ya kutafakari juu ya watu wake na vijana wenzake.MARTIN LUTHER KING JR aliwahi kusema: nobody can give u freedo nobody can give u justice or rights or anything. You take it. Tafakari maneno haya kisha endeleza harakati
 
Mwalimu wangu hujanifundisha hivi, nakutegemea siku moja utoke nje ya CDM umshambulie kiongozi wako. Mimi nitamsema kiongozi hadharani as i have no access wewe upo kwenye kamati kuu mbona mengi huyapendi na still huyasemi? sasa kuna haja gani ya huwa na vikao? nonsense. tulio kariakoo tuseme walio ikulu wakisema tupo salama?

Kweli kabisa tupo pamoja hapa ila kama katiba yao inasema hivo ifanye hivo.

Hoja hii ndo ipo kwenye (i). acha sisi wa huku kariakoo na vilabuni tuseme lakini kama Pinda akimlalamikia JK au Zitto akimlalamikia Mbowe au Dr. Kitila akimlalamikia Dr. Slaa hapa JF tuna taasisi? unataka kusema nini Dr. Kitila? Ukipata nafasi ya kuonana na JK ni kwenda kunywa chai au you talk serious issues?

Nitafurahi sana ukiwa mjumbe wa CC chadema utoke kwenye kikao umlaumu chair au katibu kwa doings zao. Kama una access itumie acha kulalamika nje ya mfumo. Not neccessarily kila unapolalamika uwe sahihi. Ndo maana kuna vikao otherwise let close off mifumo tujikalie hivivi kila mtu awe na lwake na ikiwezekana labda tulipigie kura ili tujue direction. Ndo maana kule US wakitangaza misimamo through press huwa wanazungukwa kuonyesha umoja hapa Kafulila anaitisha press na Ruhuza anaitisha press yake. Sisi tufanyeje? Nidhamu ya kuheshimu mfumo uliopo ni muhimu.
 
GL unaposema kuwa masharti ya DC ili kupata misaada nikukosa utu hapo nimekuona kumbe na wewe utu huna.
Unapinga watu kufunga ndoa ya jinsia moja wakati wao huo ndo utu wao. Chama chenu kinaubili Demokrasia,je kuna Demokrasia bila kueshimu haki za binadam and minority rights? Hapa ndo tunasema wanasiasa wengi ni wanafiki zaidi kama wewe GL.
unapumliwa mgongoni? Oophsss! Mnaipeleka wapi hii sayari ninyi viumbe?
 
Wanasiasa wetu jamani yaani hata sielewi kabisa wamejifunza wapi siasa hizi.. Sasa huyu Lema maswala ya NCCR yanamhusu nini hadi kuingilia kati na kuchagua upande wakati hajui undani wa haya maswala na Pilipili asiyokula inamwasha nini?.. Ni kihelele kipi kilichomkumba Lema au ana beef na Kafulila?..

mkuu makosa ya G.Lema kutoa mawazo yake?
 
I have been on JF for sometime now and I have noticed a very disturbing pattern. Why is it when a an argument is being lost we result to abusive words or when someone has any opinion different from ours we insult them or shout them down. What happened to freedom of expression. It is this attitude of wanting to hear what suits us that breeds sycophants and makes our leaders lie to us. How exactly our we going to grow as a nation if the enlighten ones do not have basic respect other peoples opinion. This basic respect is the hallmark of civilized society

Kuhusu suala la Kafulila:nimesikitika sana kwa baadhi ya wanasiasa vijana kufurahia suala la kafulila ilihali mazingira ya kufukuzwa kwake yanajulikana.Ndani ya vyama vyetu vya siasa kuna tatizo la kutovumiliana hasa katika uhuru wa kutoa mawazo.Leo hii CCM na serikali yake wakiongelea kuhusu nyaraka za siri au the so called siri za jeshi tunalalamika.Ukirudi ndani ya vyama vyetu vya siasa kuna mdudu anayeitwa siri za vikao au siri za chama.Mara nyingi mbinu hizi hutumiwa na viongozi wasiojiamini na wasiopenda kuguswa.....hizi ni dalili za udikteta na zinasaliti harakati zote za kidemokrasia,

Pia nimegundua kuna kundi ambalo tunaunda la vijana wasio na weledi wa kuchanganua mambo.Tunaunda kundi la vijana wanaojipendekeza na kuzika uhuru wao wa mawazo ndani ya vyama vya siasa na katika medani za kitaifa.

Nitumie fursa hii kumpongeza ndugu Nape Nnauye kwa comment zake zenye mwelekeo chanya katika kuviasa vyama vya siasa kikiwamo chama chake (CCM) juu ya maamuzi yaliyokosa busara kwa viongozi wa vyama kufukuza wale wanaotofautiana nao kimtazama (ingawa ni wajibu wake kama kijana mwenye fikra huru).

Kitu cha ajabu na kushangaza naona baadhi ya vijana tena kutoka kambi ya upinzani wakitoa comments zilizozoeleka ndani ya chama cha mapinduzi juu ya hili sakata la NCCR-Mageuzi na Ndugu David kafulila.Naona dalili za kujenga taifa lenye upofu na ushabiki.tunaanza vibaya safari hii ya miaka mingine 50 ya uhuru na harakati za ukombozi wa pili(second liberation struggle).Ngwe ya pili ya miaka 50 imejikita zaidi katika mapambano ya fikra,nimeshaona dalili mbaya kwamba njiani tutapoteza wengi kama fikra nilizoziona hapa ndizo tunazozitegemea

baadhi ya wazee wakisaidiwa na vijana wasaliti wanashindwa katika vita hii ya mapambano ya fikra ndani na nje ya vyama vya siasa.unafiki wa vijana kama hawa ndio uliolifikisha taifa hili hapa lilipo miaka hii 50 baada ya uhuru.Naelewa sisi vijana tuna changamoto nyingi sana,tunastahili kujifunza kwa wazee(walio makini) ili tuweze kuchangia katika harakati hizi za ukombozi.Hatuwezi kufanya hivi kwa kuoneana wivu,unafiki na ushabiki kipofu.Vijana sampuli ya kafulila wataendelea kupata shida ndani ya vyama hivi unless radical measures zichukuliwe

David kafulila ni muda wa kutafakari na kuchukua hatua.Kilichotokea ni sehemu ya historia ya maisha yako ya kisiasa,uwezo wako ni mkubwa.Watanzania wanajua ni akina nani wanaopambana kwa dhati,wanaelewa ni akina nani wanaotafuta umaarufu binafsi kwa gharama za wengine.Mengine yote , i mean mapungufu yako kisiasa na kibinadamu ni kuyafanyia kazi.

NB: Let us decided on this forum not to dignify insults with any response no matter how tempting it might be.
 
Mwalimu wangu hujanifundisha hivi, nakutegemea siku moja utoke nje ya CDM umshambulie kiongozi wako. Mimi nitamsema kiongozi hadharani as i have no access wewe upo kwenye kamati kuu mbona mengi huyapendi na still huyasemi? sasa kuna haja gani ya huwa na vikao? nonsense. tulio kariakoo tuseme walio ikulu wakisema tupo salama?

Kweli kabisa tupo pamoja hapa ila kama katiba yao inasema hivo ifanye hivo.

Hoja hii ndo ipo kwenye (i). acha sisi wa huku kariakoo na vilabuni tuseme lakini kama Pinda akimlalamikia JK au Zitto akimlalamikia Mbowe au Dr. Kitila akimlalamikia Dr. Slaa hapa JF tuna taasisi? unataka kusema nini Dr. Kitila? Ukipata nafasi ya kuonana na JK ni kwenda kunywa chai au you talk serious issues?

Nitafurahi sana ukiwa mjumbe wa CC chadema utoke kwenye kikao umlaumu chair au katibu kwa doings zao. Kama una access itumie acha kulalamika nje ya mfumo. Not neccessarily kila unapolalamika uwe sahihi. Ndo maana kuna vikao otherwise let close off mifumo tujikalie hivivi kila mtu awe na lwake na ikiwezekana labda tulipigie kura ili tujue direction. Ndo maana kule US wakitangaza misimamo through press huwa wanazungukwa kuonyesha umoja hapa Kafulila anaitisha press na Ruhuza anaitisha press yake. Sisi tufanyeje? Nidhamu ya kuheshimu mfumo uliopo ni muhimu.

Selous, ukiwa mwanafunzi wa Social Psychology utakumbuka vizuri nilivyowafundisha ubaya wa 'group think' na 'conformity' jinsi zinavyofifisha uwezo wa kufikiri. Nami sijaongelea habari za kutukana kiongozi; naongelea habari za kumkosoa. Kumtukana kiongozi au mtu yeyote ni jambo la ovyo ndani au nje ya vikao. Mtu yeyote anayetukana anastahili kuchukuliwa hatua za nidhamu awe ametukana ndani au nje ya vikao. Lakini napinga kwa nguvu zangu zote watu kujijengea uimaya wa kutukuguswa hata pale wanapofanya madudu.

Nina bahati kwamba viongozi wangu katika chama changu siku zote wamekuwa wakisimamia misimamo ya chama tuliyoipitisha katika vikao vyetu. Ikitokea kiongozi wangu yeyote akafanya mambo ya kijinga barabarani au Kariakoo, kama alivyofanya huyu aliyesababisha Kafulila afukuzwe, nitampinga hukohuko barabarani/Kariakoo na wala sitasubiri vikao. Nawe nakuhimiza kumpinga kiongozi yeyote mjinga anayefanya ujinga wake barabarani au Kariakoo, na ufanye hivyo popote na wala usisubiri vikao kwa ajili hiyo!
 
Mbatia is a crap..i wounder why some of youth leaders especially frm opposition support wht Mbatia did 2 kafulila..i support Kafulila 4 what he believe,NCCR=CCM B(under Mbatia)
 
Ni kweli Biera.Hata hivyo kafulila alifanya kosa kumwangukia Mbatia.Haya ndiyo mambo anayotakiwa atafakari kwa kina.Kwa jinsi mimi ninavyoamini sioni mantiki ya alichofanya.Otherwise mambo haya yanafedhehesha kambi nzima ya upinzani kwa mapana na marefu,kwa kimo na katika mzunguko wake nyuzi 360
 
pasco ww ndio bure kabisa hufai hata ..wewe huna maoni yoyote unakashfu ya mbunge.
Kwani mbunge ni kamusi ya watu wote au yeye akisema wengine wote wawe kimya. Mimi hoja yangu kwenye suala hili ni hii. NCCR - Mageuzi wamekosea kumfukuza chama Kafulila njia sahihi ni ile waliyoitumia kwa Felix Mkosamali. Kwani adhabu zote ni ile ya kumfukuza chama Kafulila?

Tanzania tunaanza kujenga tabia ya viongozi wenye nafasi za kitaifa kutokupingwa. Kwenye vyama vyote vya siasa wenyeviti "hawagusiki" na tabia hii inakuzwa na vibaraka wa viongozi hao wanaotumia vyombo vya habari na mitandao jamii kuwachafua wale wenye mawazo tofauti na viongozi wanaowashabikia.

Kafulila kosa lake ni kusema Mbatia hafai na kuonana na Kikwete ni kufanya makosa. Kwangu mimi haya si makosa ya kumfukuza mtu chama na kusababisha kufanyika kwa uchaguzi mdogo ambao naamini NCCR hii haiweze kushinda hata kwa dawa na kwa tabia za Mbatia ufa kati ya CHADEMA na NCCR utazidi kuongezeka.

NCCR walipaswa kumvua Kafulila vyeo vyote vya kichama na kumweka kwenye uangalizi kwa kipindi fulani kabla ya kumruhusu kugomb ea vyeo vya kichama. Lakini kumvua uanachama ni ujuha uliopindukia na ushamba wa matumizi wa madaraka. Hivi vikao vinavyoitwa Halmashauri/Baraza Kuu vya hivi vyama vyetu vyenyewe havijitambui.

Wakati mwingine unaweza kujiuliza ilikuwaje Halmashauri Kuu ya TLP iliruhusu kutungwe Katiba inayompa madaraka Mwenyekiti wa chama kumfukuza mtu kwenye nafasi ya uongozi au uanachama bila ya kupitia kikao chochote. Ni madudu mangapi yanafanyika kwenye Halmashauri kuu ya CCM, ni mambo mangapi hayajadiliwi kina kwenye Baraza Kuu la CHADEMA ua CUF?

KAFULILA KAHUKUMIWA KWA NJIA HALALI LAKINI ADHABU ALIYOPEWA NI YA UONEVU!!

NIdhamu ni jambo la msingi mahala popote pale. Uhuru usiyo kuwa na nidhamu si uhuru bali ni ujinga. Kukosoa serikali hadharani ni wajibu wa vyama vya upinzani ili serikali ipunguze makali kwa wananchi na uhuru huwo huwo usisababisha kukosekana kwa nidhamu ndani ya vyama. Utawezajemkuikosa serikali wakati umekosa nidhamu ndani ya chama chako? Nidhamu lazima ianze ndani kwako ndiyo utoke na kupaza sauti kwa wanaopindisha ukweli! Mimi binafsi sijafurahishwa kwa kafulila kuvuliwa uanachama wala sichekelei maamuzi hayo. Ila kwasababu ya kujenga msingi bora ni lazima nidhamu izingatiwe umaarufu usifanyike kama mtu mmoja ni zaidi ya taasisi.

MUNGU mpe kafulila moyo wa subiri awezekuzivuka changamoto hizzi. Na sikuhama chama chake bado ananafasi ya kutafakari juu ya watu wake na vijana wenzake.MARTIN LUTHER KING JR aliwahi kusema: nobody can give u freedo nobody can give u justice or rights or anything. You take it. Tafakari maneno haya kisha endeleza harakati
\

Mkuu hapo kwenye Red napata shida kuelewa kidogo, ninavyojua kafulila hana chama tena kwasababu amevuliwa uanachama wa NCCR nadhani ana haki ya kwenda kokote anakotaka hata kuomba tena uanachama wa NCCR
 
Selous, ukiwa mwanafunzi wa Social Psychology utakumbuka vizuri nilivyowafundisha ubaya wa 'group think' na 'conformity' jinsi zinavyofifisha uwezo wa kufikiri. Nami sijaongelea habari za kutukana kiongozi; naongelea habari za kumkosoa. Kumtukana kiongozi au mtu yeyote ni jambo la ovyo ndani au nje ya vikao. Mtu yeyote anayetukana anastahili kuchukuliwa hatua za nidhamu awe ametukana ndani au nje ya vikao. Lakini napinga kwa nguvu zangu zote watu kujijengea uimaya wa kutukuguswa hata pale wanapofanya madudu.

Nina bahati kwamba viongozi wangu katika chama changu siku zote wamekuwa wakisimamia misimamo ya chama tuliyoipitisha katika vikao vyetu. Ikitokea kiongozi wangu yeyote akafanya mambo ya kijinga barabarani au Kariakoo, kama alivyofanya huyu aliyesababisha Kafulila afukuzwe, nitampinga hukohuko barabarani/Kariakoo na wala sitasubiri vikao. Nawe nakuhimiza kumpinga kiongozi yeyote mjinga anayefanya ujinga wake barabarani au Kariakoo, na ufanye hivyo popote na wala usisubiri vikao kwa ajili hiyo!

Mwalimu nakubaliana nawe kabisa.

Kumbuka David alikuwa anasema haya Mbatia ni CCM na ameshindwa kufanya siasa kiasi cha kusababisha NCCR Mageuzi kiwe chama cha Press Conference tu. Kwa nafasi yake, uzoefu wake kwenye siasa alishindwa kupress hii ndani ya vikao vya chama na akiwa na ushahidi? Kama angejitoa ukatibu mwenezi na nyadhifa zote sawa then akasema haya sawa. Na unakumbuka kilichompoka kazi huko CDM?

Inawezekana kabisa Mbatia sio mwenzetu ila anaweza kuondoka kabisa lakini sio kwa staili hii.
 
Kwani mbunge ni kamusi ya watu wote au yeye akisema wengine wote wawe kimya. Mimi hoja yangu kwenye suala hili ni hii. NCCR - Mageuzi wamekosea kumfukuza chama Kafulila njia sahihi ni ile waliyoitumia kwa Felix Mkosamali. Kwani adhabu zote ni ile ya kumfukuza chama Kafulila?

Tanzania tunaanza kujenga tabia ya viongozi wenye nafasi za kitaifa kutokupingwa. Kwenye vyama vyote vya siasa wenyeviti "hawagusiki" na tabia hii inakuzwa na vibaraka wa viongozi hao wanaotumia vyombo vya habari na mitandao jamii kuwachafua wale wenye mawazo tofauti na viongozi wanaowashabikia.

Kafulila kosa lake ni kusema Mbatia hafai na kuonana na Kikwete ni kufanya makosa. Kwangu mimi haya si makosa ya kumfukuza mtu chama na kusababisha kufanyika kwa uchaguzi mdogo ambao naamini NCCR hii haiweze kushinda hata kwa dawa na kwa tabia za Mbatia ufa kati ya CHADEMA na NCCR utazidi kuongezeka.

NCCR walipaswa kumvua Kafulila vyeo vyote vya kichama na kumweka kwenye uangalizi kwa kipindi fulani kabla ya kumruhusu kugomb ea vyeo vya kichama. Lakini kumvua uanachama ni ujuha uliopindukia na ushamba wa matumizi wa madaraka. Hivi vikao vinavyoitwa Halmashauri/Baraza Kuu vya hivi vyama vyetu vyenyewe havijitambui.

Wakati mwingine unaweza kujiuliza ilikuwaje Halmashauri Kuu ya TLP iliruhusu kutungwe Katiba inayompa madaraka Mwenyekiti wa chama kumfukuza mtu kwenye nafasi ya uongozi au uanachama bila ya kupitia kikao chochote. Ni madudu mangapi yanafanyika kwenye Halmashauri kuu ya CCM, ni mambo mangapi hayajadiliwi kina kwenye Baraza Kuu la CHADEMA ua CUF?

KAFULILA KAHUKUMIWA KWA NJIA HALALI LAKINI ADHABU ALIYOPEWA NI YA UONEVU!!

You have Nailed it...Kwenye Blue na Red !
 
Ni kweli Biera.Hata hivyo kafulila alifanya kosa kumwangukia Mbatia.Haya ndiyo mambo anayotakiwa atafakari kwa kina.Kwa jinsi mimi ninavyoamini sioni mantiki ya alichofanya.Otherwise mambo haya yanafedhehesha kambi nzima ya upinzani kwa mapana na marefu,kwa kimo na katika mzunguko wake nyuzi 360

kumwangukia Mbatia ndipo alipofanya kosa,mbona hakumuonya Kafulila kama ambavyo kafanya kwa Mkosamali?
 
Binadamu wanapenda kusikia au kuambiwa mazuri tu na pindi anapoambiwa ukweli anamchukia mtoa ukweli.Magamba.com ni matokeo wa huu mfumo wa kutotaka kusema ukweli..............
ukomavu katika jambo lolote ni kusimamia ukweli daima, kama ulisema hili ni jembe na ukapewa adhabu kwa kusema hivyo,

Mytake: Nini maana ya kuomba msamahaa baada ya hukumu kutoka:
  1. Umegundua kuwa ulikosea kusema Jembe?
  2. Na umekubali kuwa hilo siyo Jembe ni Shoka
kwa maana hiyo ulikuwa una testi kiberiti kama kilikuwa kimejaa?Ni vizuri kama aliona kuwa yale haliyoyasema halikuwa yupo sahihi hakukuwa na haja ya yeye kuomba msamaha coz alitafakari kabla hajasema.

Lema ameeleza ukweli ambao wengi wetu hatupendi kuusema zaidi ya kutoa sifa za kijinga.
 
I have been on JF for sometime now and I have noticed a very disturbing pattern. Why is it when a an argument is being lost we result to abusive words or when someone has any opinion different from ours we insult them or shout them down. What happened to freedom of expression. It is this attitude of wanting to hear what suits us that breeds sycophants and makes our leaders lie to us. How exactly our we going to grow as a nation if the enlighten ones do not have basic respect other peoples opinion. This basic respect is the hallmark of civilized society

Kuhusu suala la Kafulila:nimesikitika sana kwa baadhi ya wanasiasa vijana kufurahia suala la kafulila ilihali mazingira ya kufukuzwa kwake yanajulikana.Ndani ya vyama vyetu vya siasa kuna tatizo la kutovumiliana hasa katika uhuru wa kutoa mawazo.Leo hii CCM na serikali yake wakiongelea kuhusu nyaraka za siri au the so called siri za jeshi tunalalamika.Ukirudi ndani ya vyama vyetu vya siasa kuna mdudu anayeitwa siri za vikao au siri za chama.Mara nyingi mbinu hizi hutumiwa na viongozi wasiojiamini na wasiopenda kuguswa.....hizi ni dalili za udikteta na zinasaliti harakati zote za kidemokrasia,

Pia nimegundua kuna kundi ambalo tunaunda la vijana wasio na weledi wa kuchanganua mambo.Tunaunda kundi la vijana wanaojipendekeza na kuzika uhuru wao wa mawazo ndani ya vyama vya siasa na katika medani za kitaifa.

Nitumie fursa hii kumpongeza ndugu Nape Nnauye kwa comment zake zenye mwelekeo chanya katika kuviasa vyama vya siasa kikiwamo chama chake (CCM) juu ya maamuzi yaliyokosa busara kwa viongozi wa vyama kufukuza wale wanaotofautiana nao kimtazama (ingawa ni wajibu wake kama kijana mwenye fikra huru).

Kitu cha ajabu na kushangaza naona baadhi ya vijana tena kutoka kambi ya upinzani wakitoa comments zilizozoeleka ndani ya chama cha mapinduzi juu ya hili sakata la NCCR-Mageuzi na Ndugu David kafulila.Naona dalili za kujenga taifa lenye upofu na ushabiki.tunaanza vibaya safari hii ya miaka mingine 50 ya uhuru na harakati za ukombozi wa pili(second liberation struggle).Ngwe ya pili ya miaka 50 imejikita zaidi katika mapambano ya fikra,nimeshaona dalili mbaya kwamba njiani tutapoteza wengi kama fikra nilizoziona hapa ndizo tunazozitegemea

baadhi ya wazee wakisaidiwa na vijana wasaliti wanashindwa katika vita hii ya mapambano ya fikra ndani na nje ya vyama vya siasa.unafiki wa vijana kama hawa ndio uliolifikisha taifa hili hapa lilipo miaka hii 50 baada ya uhuru.Naelewa sisi vijana tuna changamoto nyingi sana,tunastahili kujifunza kwa wazee(walio makini) ili tuweze kuchangia katika harakati hizi za ukombozi.Hatuwezi kufanya hivi kwa kuoneana wivu,unafiki na ushabiki kipofu.Vijana sampuli ya kafulila wataendelea kupata shida ndani ya vyama hivi unless radical measures zichukuliwe

David kafulila ni muda wa kutafakari na kuchukua hatua.Kilichotokea ni sehemu ya historia ya maisha yako ya kisiasa,uwezo wako ni mkubwa.Watanzania wanajua ni akina nani wanaopambana kwa dhati,wanaelewa ni akina nani wanaotafuta umaarufu binafsi kwa gharama za wengine.Mengine yote , i mean mapungufu yako kisiasa na kibinadamu ni kuyafanyia kazi.

NB: Let us decided on this forum not to dignify insults with any response no matter how tempting it might be.

Ben,

Mimi sifurahii kwa namna yeyote ile Kafulila kuvuliwa uanachama au hata kupoteza ubunge. Nalilia my next generation kwa watu ambao ni wanasiasa na wakati huo huo hawazingatii mambo ya msingi na shida za watz. Naona tatizo hapa.
  1. Nidhamu kwenye mfumo wa taasisi. Kama ilivo huwezi kuanzisha mapambano nje ya utaratibu kutoa JK ikulu ukiwa kama Waziri wake hapana au mtz wa kawaida. Toka nje wa gari, kaa barabarani swaga mwendo. Ukishindwa toka barabarani katengeneze njia yako kufika huko. JK hafai haina maana Sita aanze harakati akiwa waziri. Atoke, akae pembeni kama Mwanachama au aje CDM. TUJIFUNZE KUTUMIA NAFASI na KUWAJIBIKA, sio uasi. Tunahitaji kujijenga kiutunu zenye utaifa.
  2. Kuna vijana hawawezi kusimamia wanachikiamini au hawawezi kufikiri kabla ya kuamua. mfano unachukua fomu ya kugombea halafu unajitoa unaungana na mwingine. Mfumo huu kuna wazee wazuri tu na vijana hovyo kabisa.
  3. utu na nidhamu havipimwi kwa thamani ya matokeo ila kwa thamani ya kufikiri kabla ya kuamua.
  4. ubaya wa mifumo yetu ndo athari zake hizi na vema kila shubiri tuipate tujirekebishe.
  5. Busara na hekima kwenye sheria? Kwanini tunalaumu hatua za EPA?
Kafulila alitakiwa ajue katiba yake, mfumo wa nccr na taifa, thamani yake kwenye chama na watz, awe na plan B, kilichomtoa CDM kilimfundisha nini, matatizo ya vijana wa kitz bila kusahau dhamira yake.
 
Back
Top Bottom