Mbowe, Lissu wafundeni wafuasi Falsafa ya Chama

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,867
35,874
Mada kama hizi huelekezwa kwenye vile vyama vyenye ule wito mtakatifu wa ukombozi.

"Ikiwapendeza waheshimiwa, waungwana kabisa:"

Falsafa ya chama ni jambo la msingi zaidi katika chama chochote. Falsafa hutoa utambulisho halisi wa chama. Ikaweza kutofautisha baina ya vyama. Ikazaa imani za chama.

"Ya kuwa chama kinasimamia nini? Kwanini hii ni CHADEMA siyo CCM. Kwanini hii ni CUF siyo ACT? Tofauti haiwezi kuwa majina. Inapaswa kuwa wazi ili wafuasi wakajua kamili kama walipo ni sahihi."

Watazipigania vipi kwa moyo wao wote, sera au agenda za chama kama falsafa ya chama haijulikani?

Falsafa za vyama zitaweka wazi misimamo ya vyama kuhusu mambo yote yakiwamo yaliyo tata na ikaondoa mikanganyiko isiyokuwa na tija.

"Kwa mfano, nini misimamo ya chama kuhusu Katiba Mpya, vita vya Ukraine, HAMAS, Gaza, Palestina, nk?"

Misimamo rasmi ya chama ni "binding." Mfuasi hawezi kuwa na msimamo tofauti na wa chama huku akijinasibu hadharani kuongea kwa niaba ya chama.

Tunapiga hatua, mdogo mdogo tutafika tu:

I. Mbowe, Lissu chukueni hatua kurejesha nidhamu kwenye chama

II. Mbowe, Lissu nidhamu inaporejea wafundeni wafuasi heshima
 
Kuwafundisha wafuasi falsafa ya chama sio jambo litakalochukua muda mrefu sana? anyway, kwanza is it practicable?

Hujaonesha ni njia zipi zitakazotumika kufundisha hizo falsafa, jambo ambalo pia naona limeacha gap kwenye mada yako.

Lakini pia, huoni haya mambo ya kifalsafa wakati mwingine huingiliana na mitazamo/ maisha binafsi ya watu, hivyo unaweza kuta jambo fulani ambalo kwako ni baya, kwa mwenzio wa chama chako linaweza kuwa la kawaida?

Kwa mfano, mambo kama hayo ya LBTQ japo kwa upana wake jamii yetu haikubaliani na hilo jambo kwa kiwango kikubwa, lakini pia ukweli ni kwamba, watu hao wapo kwenye jamii yetu.

Sasa kwa muktadha huo, huoni kama hao kina Lissu kufanya hii kazi uliyowapa wanaweza kuwa wanatengeneza tatizo lingine kwa wanachama wao, wanaweza kuanza kuwagawa kwa matabaka, kwasababu kwa akili yangu, mtu yeyote anaruhusiwa kujiunga na chama chochote cha siasa ilimradi afuate sheria husika, bila kujali mrengo wake kijamii?

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Kuwafundisha wafuasi falsafa ya chama sio jambo litakalo chukua muda mrefu sana?

Hujaonesha ni njia zipi zitakazotumika kufundisha hizo falsafa, jambo ambalo pia naona limeacha gap kwenye mada yako.

Lakini pia, huoni haya mambo ya kifalsafa wakati mwingine huingiliana na mitazamo binafsi ya watu, hivyo unaweza kuta jambo fulani ambalo kwako ni baya, kwa mwenzio wa chama chako linaweza kuwa la kawaida?

Kwa mfano, mambo kama hayo ya LBTQ japo kwa upana wake jamii yetu haikubaliani na hilo jambo kwa kiwango kikubwa, lakini pia ukweli ni kwamba, watu hao wapo kwenye jamii yetu.

Sasa kwa muktadha huo, huoni kama hao kina Lissu kufanya hii kazi uliyowapa wanaweza kuwa wanatengeneza tatizo lingine kwa wanachama wao, wanaweza kuanza kuwagawa kwa matabaka, kwasababu kwa akili yangu, mtu yeyote anaruhusiwa kujiunga na chama chochote cha siasa ilimradi afuate sheria husika bila kujali mrengo wake kijamii?

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app

Mkuu tofautisha kufundisha na kufunda:

1. Falsafa ya chama haiwezi kuwa siri kwani ndiyo ulio utambulisho wake kamili.

2. Wafuasi katika chama ni kwa mujibu wa falsafa yenye kuzaa Imani na misimamo ya chama.

3. Wafuasi hawawezi kuwa wa kuvizia tukiogopa hili au lile linaweza kumkwaza fulani.

4. Asiye kubaliana na falsafa za chama huyo ni wa kufukuzwa unceremoniously kama wale wabunge wa yobo.

5. Misimamo ya chama kuhusu LGBTQ, HAMAS, Ukraine nk haiwezi kutegemea upepo.

6. Kutegemea upepo hakuta tufikisha popote.

7. Wafuasi wasioijua au kuiamini falsafa ya chama watakipigania vipi chama chao kwa moyo wao wote?

8. Kutokuwa na falsafa ya wazi labda kama unataka kusema chama kikose misimamo.

9. Wafuasi wasiokubaliana na misimamo ya chama ni heri wasiwamo chamani.
 
Mkuu tofautisha kufundisha na kufunda:

1. Falsafa ya chama haiwezi kuwa siri kwani ndiyo ulioutambulisho wake kamili.

2. Wafuasi katika chama ni kwa mujibu wa falsafa yenye kuzaa Imani na misimamo ya chama.

3. Wafuasi hawawezi kuwa wa kuvizia tukiogopa hili au lile linaweza kumkwaza fulani.

4. Asiyekubaliana na falsafa za chama huyo ni wa kufukuzwa unceremoniously kama wale wabunge wa yobo.

4. Misimamo ya chama kuhusu LGBTQ, HAMAS, Ukraine nk haiwezi kutegemea upepo.

5. Kutegemea upepo hakutatufikisha popote.

6. Wafuasi wasioijua au kuiamini falsafa ya chama watakipigania vipi chama chao kwa moyo wao wote?

7. Kutokuwa na falsafa ya wazi labda kama unataka kusema chama kikose misimamo.

8. Wafuasi wasiokubaliana na misimamo ya chama ni heri wasiwamo chamani.
Naona unazidi kuniacha njia panda.

Hivi hauoni kama falsafa ya chama kwa kuzingatia hayo mambo uliyoorodhesha, inaweza kutofautiana na sheria za nchi zinazomtaka mtu kujiunga na chama chochote cha siasa, bila kujali rangi yake, jinsia, dini na mengineyo?

Au kwa maana nyingine niseme, huoni huu mtazamo wako ni kama udikteta fulani? kwasababu naona unaenda kuwataka kina Lissu waanze kuwatenga baadhi ya members wa society yetu, huku ukijua fika nao wana haki sawa kama raia wengine wa hii nchi, kwasababu tu falsafa za Chadema zitaenda kinyume na hali zao kijamii?

Tena zaidi, naona unakosea sana pale unapoyahusisha makundi yenye misimamo mikali kwenye kujenga hoja yako, hayo makundi mara nyingi yana mitazamo ya kidikteta, ndio maana nawe umejikuta una mitazamo ya aina hiyo hapa kwenye andiko lako bila kujua.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Naona unazidi kuniacha njia panda.

Hivi hauoni kama falsafa ya chama kwa kuzingatia hayo mambo uliyoorodhesha, inaweza kutofautiana na sheria za nchi zinazomtaka mtu kujiunga na chama chochote cha siasa bila kujali rangi yake, jinsia, dini na mengineyo?

Au kwa maana nyingine niseme, huoni huu mtazamo wako ni kama udikteta fulani? kwasababu naona unaenda kuwataka kina Lissu waanze kuwatenga baadhi ya members wa society yetu, huku ukijua fika nao wana haki sawa kama raia wengine wa hii nchi, kwasababu tu falsafa za Chadema zitaenda kinyume na hali zao kijamii?

Tena zaidi, naona unakosea sana pale unapoyahusisha makundi yenye misimamo mikali kwenye kujenga hoja yako, hayo makundi mara nyingi yana mitazamo ya kidikteta, ndio maana nawe umejikuta una mitazamo ya aina hiyo hapa kwenye andiko lako bila kujua.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Anataka na CHADEMA wawe wajinga kama wana CCM kila anachosema Mwenyekiti kazi yao ni kushangilia bila kuhoji chochote
 
Naona unazidi kuniacha njia panda.

Hivi hauoni kama falsafa ya chama kwa kuzingatia hayo mambo uliyoorodhesha, inaweza kutofautiana na sheria za nchi zinazomtaka mtu kujiunga na chama chochote cha siasa bila kujali rangi yake, jinsia, dini na mengineyo...

Au kwa maana nyingine niseme, huoni huu mtazamo wako ni kama udikteta fulani? kwasababu naona unaenda kuwataka kina Lissu waanze kuwatenga baadhi ya members wa society yetu, huku ukijua fika nao wana haki sawa kama raia wengine wa hii nchi?

Tena zaidi, naona unakosea sana pale unapoyahusisha makundi yenye misimamo mikali kwenye kujenga hoja yako, hayo makundi mara nyingi yana mitazamo ya kidikteta, ndio maana nawe umejikuta una mitazamo ya aina hiyo hapa bila kujua.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app

Usichokiona ni kuwa falsafa ndiyo msingi wa chama. Falsafa huzaa imani na hivyo misimamo ya chama:

1. Tunajiunga kwenye vyama kufuata imani na misimamo ya vyama itokanayo na falsafa ya chama husika.

2. Hatujiungi kwenye vyama Kwa lazima ya sheria za nchi.

3. Tunavutiwa na imani na misimamo ya chama si kwa msukumo wa sheria.

4. Msimamo na imani za chama ni "binding" na ndiyo maana hizo huwapo kimaandishi.

5. Msimamo na imani za chama huwezi kuziita udikteta na ndiyo maana chama kinayo haki kumfukuza mtu kama alivyo na haki ya kuondoka kama hakubaliani na Imani na misimamo ya chama.

6. Msimamo wa chama kuhusu jambo lolote hauwezi kuwa siri kwa mujibu wa Imani au falsafa yake.

7. Vyama haviwezi kukaa kiujanja ujanja, kiwizi wizi, kimachale machale au kuwapo bila misimamo.

8. Chama bila msimamo kwenye jambo ni zogo.
 
Cc: Pascal Mayalla kwa mwongozo wako tafadhali, ikikupendeza.
Hapa ulitakiwa kuandika hivi;

Tunajiunga kwenye vyama, kwa kufuata imani na misimamo ya vyama, tukiongozwa na sheria za nchi, hapa ndio ningekuelewa.

Au kwa namna nyingine nikwambie useme hivi, tunajiunga kwenye vyama kwa kutii sheria, naamini hizo ndio zinatupa ruhusa ya kujiunga, kisha baada ya hapo ndio unaangalia chama kile kinachokufaa.

Naandika hivyo nikiamini kwamba, hakuna jambo linalofanyika siku zote bila muongozo wa sheria, tunazifuata sheria ndio maana mambo yapo kama yalivyo, kinyume na hapo ndio ingekuwa zogo.

Hivyo basi, hata mara moja hutakiwi kuiweka sheria nyuma ya jambo lolote, kuna mifano mingi nayoweza kukupa kuthibitisha hili.

Mfano wa jana tu, baada ya kina Mdee na wenzake kuvuliwa uanachama Chadema, kilichofuata ni kwa pande zote mbili kuzirudia sheria na kutazama zinasema nini ili kujitafutia ulinzi. Hapo ndipo kikaitishwa kikao cha KK na baadae baraza kuu, huku wakina Mdee nao wakisema sheria hazikufuatwa ipasavyo, na matokeo yake ndio kesi kufunguliwa mahakamani.

Hapo kwenye namba nne ukumbuke hiyo misimamo na imani za chama unayosema iko "binding" ndio sheria zenyewe, zinazowaongoza wanachama wake kufuata taratibu walizojiwekea chamani, ndio maana wakienda kinyume nazo, majanga huwakuta.

Hapa ndio utanielewa vizuri nilipokwambia pale juu sheria ndio zinatuongoza kwenye kila jambo tunalofanya, na kama ule mfano niliokupa hapo juu unavyosema.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Hapa ulitakiwa kuandika hivi;

Tunajiunga kwenye vyama, kwa kufuata imani na misimamo ya vyama, tukiongozwa na sheria za nchi, hapa ndio ningekuelewa.

Kunitaka niandike miye utakavyo ili ndipo ukapate kuelewa nadhani hiyo ni kuvuka mipaka:

1. Kwani una maana vinginevyo utaamua kukaza ubongo tu?

2. Kwamba basi kabla ya kuandika niwe nakuuliza niandikaje ili ukawe tayari kuelewa?

Naandika hivyo nikiamini kwamba, hakuna jambo linalofanyika siku zote bila muongozo wa sheria, tunazifuata sheria ndio maana mambo yapo kama yalivyo, kinyume na hapo ndio ingekuwa zogo.

Hivyo basi, hata mara moja hutakiwi kuiweka sheria nyuma ya jambo lolote, kuna mifano mingi nayoweza kukupa kuthibitisha hili.

Raia wanayo haki ya kujiunga na chama chochote cha siasa kilichosajiliwa. Haipo sheria ya namna ya kujiunga inayompa mtu fursa ya kulazimisha yake kwenye chama chochote anapoona akajiunge.

Kwenye chama tunafuata yaliyopo na sana sana kuchangia panapo nafasi. Twajiunga kama wageni. Hatuendi kushurutisha au kulazimisha. Ndiyo maana mtu anaweza kuondoka au kufukuzwa, ila hawezi kukifukuza chama!

Mfano wa jana tu, baada ya kina Mdee na wenzake kuvuliwa uanachama Chadema, kilichofuata ni kwa pande zote mbili kuzirudia sheria na kutazama zinasema nini ili kujitafutia ulinzi. Hapo ndipo kikaitishwa kikao cha KK na baadae baraza kuu, huku wakina Mdee nao wakisema sheria hazikufuatwa ipasavyo, na matokeo yake ndio kesi kufunguliwa mahakamani.

Linganisha vizuri kuwahusu wabunge hao hapa kuona ni kwa nini mgogoro huu upo, kwanini hawa wanafukuzwa, kwanini wanang'ang'ania na kwa nini hawakifukuzi chama.

"Wamekiuka imani na misimamo ya chama."

Halipo tatizo jingine. Wanazo njia mbili tu hata kama wakatambike. Kuikubali wabaki au kuikataa waelekee kunakowafaa zaidi.

Misimamo na imani ni za chama si zao. Zao wanaweza kukaa nazo tu mwenye haja nazo atawafuata majumbani kwao.

Hapo kwenye namba nne ukumbuke hiyo misimamo na imani za chama unayosema iko "binding" ndio sheria zenyewe, zinazowaongoza wanachama wake kufuata taratibu walizojiwekea chamani.

Tofautisha sheria za chama kwa upande mmoja na imani na misimamo ya chama kwa upande mwingine.

"Kwamba mwanachama anatakiwa kuwa mwadilifu; ni sheria, si imani wala msimamo wa chama."

Kwamba binadamu wote ni sawa; hii ni imani na msimamo wa chama kuhusu binadamu.

Hatuwezi kuwa na kigugumizi kuhusu Imani wala misimamo ya chama kutokea katika msingi (falsafa).

Hapa ndio utanielewa vizuri nilipokwambia pale juu sheria ndio zinatuongoza kwenye kila jambo tunalofanya, kama ule mfano niliokupa hapo juu unavyosema.

Ushauri wa bure tulia, kaa chini kama vipi na maji unywe; u tafakari:

1. Imani za chama haziwezi kuwa siri.

2. Misimamo ya chama kwenye mambo yote haiwezi kuwa siri.

3. Ni udhaifu wa wazi kuishi kinafiki, kimachale machale, kiwizi wizi, nk na hasa panapo utata.

4. Hapo namba #3 jiulize nini msimamo wa serikali kuhusu Ukraine, Gaza, HAMAS, au Palestina au LGBTQ? Kimachale machale siyo?

5. Hiyo #4 ndiyo inayoitwa opportunism kazini.

6. Vyama opportunists havifuzu kwenye wale wenye ule wito mtakatifu.
 
Kunitaka niandike miye utakavyo ili ndipo ukapate kuelewa nadhani hiyo ni kuvuka mipaka:

1. Kwani una maana vinginevyo utaamua kukaza ubongo tu?

2. Kwamba basi kabla ya kuandika niwe nakuuliza niandikaje ili ukawe tayari kuelewa?

Raia wanayo haki ya kujiunga na chama chochote cha siasa kilichosajiliwa. Haipo sheria ya namna ya kujiunga inayompa mtu fursa ya kulazimisha yake kwenye chama chochote anapoona akajiunge.

Kwenye chama tunafuata yaliyopo na sana sana kuchangia panapo nafasi. Twajiunga kama wageni. Hatuendi kushurutisha au kulazimisha. Ndiyo maana mtu anaweza kuondoka au kufukuzwa, ila hawezi kukifukuza chama!

Linganisha vizuri kuwahusu wabunge hao hapa kuona ni kwa nini mgogoro huu upo, kwanini hawa wanafukuzwa, kwanini wanang'ang'ania na kwa nini hawakifukuzi chama.

"Wamekiuka imani na misimamo ya chama."

Halipo tatizo jingine. Wanazo njia mbili tu hata kama wakatambike. Kuikubali wabaki au kuikataa waelekee kunakowafaa zaidi.

Misimamo na imani ni za chama si zao. Zao wanaweza kukaa nazo tu mwenye haja nazo atawafuata majumbani kwao.

Tofautisha sheria za chama jwa upande mmoja na imani na misimamo ya chama kwa upande mwingine.

"Kwamba mwanachama anatakiwa kuwa mwadilifu; ni sheria, si imani wala msimamo wa chama."

Kwamba binadamu wote ni sawa; hii ni imani na msimamo wa chama kuhusu binadamu.

Hatuwezi kuwa na kigugumizi kuhusu Imani wala misimamo ya chama kutokea katika msingi (falsafa).

Ushauri wa bure tulia, kaa chini kama vipi na maji unywe; u tafakari:

1. Imani za chama haziwezi kuwa siri.

2. Misimamo ya chama kwenye mambo yote haiwezi kuwa siri.

3. Ni udhaifu wa wazi kuishi kinafiki, kimachale machale, kiwizi wizi, nk na hasa panapo utata.

4. Hapo namba #3 jiulize nini msimamo wa serikali kuhusu Ukraine, Gaza, HAMAS, au Palestina au LGBTQ? Kimachale machale siyo?

5. Hiyo #4 ndiyo inayoitwa opportunism kazini.

6. Vyama opportunists havifuzu kwenye wale wenye ule wito mtakatifu.
- Nimekutaka uandike nilivyokwambia sio kwa kukushurutisha, naamini ni ili kile unachosimamia kilete maana, au kama unataka kibaki kama kilivyo, basi ndio tutakesha hapa.

- Sawa, haipo sheria inayomlazimisha mtu kujiunga na chama chochote, bali ipo sheria inayomtaka mtu kujiunga bila kulazimisha yake, kwa maana hiyo hata kama mtu alikuwa na misimamo yake kabla, lakini bila ya uwepo wa sheria husika inayomtaka kufanya hivyo, huo msimamo wake ungebaki hewani tu.

- Kuhusu kulinganisha ya wabunge kufukuzwa na wao kun'gan'gania, nilichofanya kwenye huo mfano ni kukuonesha umuhimu wa sheria unavyotuongoza kwenye mambo yetu.

Hii ni hata kama mtu alikuwa na misimamo na imani yake mwanzo inayoendana na ile ya chama alichopo, wale walitakiwa kufuata taratibu za chama chao, wakakiuka, majanga yakawafika, wakakimbilia sheria, ndio maana kwangu sheria ndio muongozo, sio imani na misimamo ya chama au mwanachama.

- Nimeshakuonesha vile hiyo imani na misimamo ya chama unayoipigania inavyoweza kwenda kinyume na sheria za nchi, nikakupa ule mfano wa LBTQ, kulazimisha hivi vitu huku ukijua wanachama wako wana mitazamo na uhuru wao wa mambo yao private, ndio nikakuita una mtazamo wa kidikteta wenye viashiria vya kuwatenga watu.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
- Nimekutaka uandike nilivyoakwambia sio kwa kukushurutisha, naamini ni ile kile unachosimamia kilete maana, au kama unataka kibaki kama kilivyo, basi ndio tutakesha hapa.

Haya ni kwa mawazo yako ambayo si lazima yawe sahihi. Tambua tofauti ya chama cha siasa na cha mpira kama Simba au Yanga:

1. Ulisikia mwanachama wa Simba au Yanga kafukuzwa?

2. Nini tofauti ya Simba, Yanga, Man U au Arsenal?

3. Nini tofauti ya CCM na Chadema?

4. Kwanini ACT, CUF au CHAUMA?

- Sawa, haipo sheria inayomlazimisha mtu kujiunga na chama chochote, bali ipo sheria inayomtaka mtu kujiunga bila kulazimisha yake, kwa maana hiyo hata kama mtu alikuwa na misimamo yake kabla, lakini bila ya uwepo wa sheria husika inayomtaka kufanya hivyo, huo msimamo wake ungebaki hewani tu.

Kwamba?

"..... bali ipo sheria inayomtaka mtu kujiunga bila kulazimisha yake."

Haipo sheria hii pia. Kilichopo ni kuwa kila mtu anayo haki ya kujiunga na chama chochote kilicho sajiliwa.

Utakapojiunga utakuta vyama ambavyo kama binadamu ni hai vina falsafa yenye kuzaa imani, sera na misimamo tofauti. Ni kwa kuzingatia haya vyama hutofautiana na hivyo "options" za wapi uende huwepo.

Tofautisha hapa na Simba au Yanga ambako majina, rangi, mahaba au ushabiki ndivyo huamua mtu ajiunge wapi.

Uhai wa chama ni katika falsafa, Imani, sera na misimamo yake. Bila hayo chama ni mfu. Matokeo yake ndiyo yale ya kukosa misimamo, kujipanga kuelekea chaguzi bila kujali juzi tuliamua nini, nk.

- Kuhusu kulinganisha ya wabunge kufukuzwa na wao kun'gan'gania, nilichofanya kwenye huo mfano ni kukuonesha umuhimu wa sheria unavyotuongoza kwenye mambo yetu.

Hii ni hata kama mtu alikuwa na misimamo na imani yake mwanzo inayoendana na ile ya chama alichopo, wale walitakiwa kufuata taratibu za chama chao, wakakiuka, majanga yakawafika, wakakimbilia sheria, ndio maana kwangu sheria ndio muongozo, sio imani na misimamo ya chama au mwanachama.

Mgogoro wa wabunge hawa na chama ni kukiukwa Kwa msimamo wa chama wa kutoshiriki kwenye bunge batili kwa niaba ya chama.

Mengine yote ni mbwembwe tu labda katika kujaribu kuurefusha msamiati.

- Nimeshakuonesha vile hiyo imani na misimamo ya chama unayoipigania inavyoweza kwenda kinyume na sheria za nchi, nikakupa ule mfano wa LBTQ, kulazimisha hivi vitu huku ukijua wanachama wako wana mitazamo na uhuru wao wa mambo yao private, ndio nikakuita una mtazamo wa kidikteta wenye viashiria vya kuwatenga watu.

Mkuu vyama hivi vina usajili ambapo manifesto zao na makabrasha lukuki hukabidhiwa kwa msajili Kwa tathmini kabla ya usajili.

Falsafa na imani za chama ni documented. Misimamo kwenye yatokanayo ni kwa mujibu wa falsafa na imani.

Imani na misimamo ya chama kama zilivyo za watu, inaratibiwa na dola. Kulikoni kuongelea visivyoweza kuwepo kwani kama chama ni halali kitakuwa kina imani na misimamo iliyo halali?

Misimamo na imani za chama kuhusu lolote haziwezi kuwa siri au kutokuwapo bali kwa chama mfu.

Angalizo:

Ndiyo maana CCM ni wahuni kwa sababu CCM hii siyo ile ya Nyerere na hawa waliomo aina ya Bashite, Joni na wenzao ni wasaka fursa tu.

Hawa wasingekuwa na nafasi kwenye CCM ya Nyerere.
 
Haya ni kwa mawazo yako ambayo si lazima yawe sahihi. Tambua tofauti ya chama cha siasa na cha mpira kama Simba au Yanga:

1. Ulisikia mwanachama wa Simba au Yanga kafukuzwa?

2. Nini tofauti ya Simba, Yanga, Man U au Arsenal?

3. Nini tofauti ya CCM na Chadema?

4. Kwanini ACT, CUF au CHAUMA?

Kwamba?

bali ipo sheria inayomtaka mtu kujiunga bila kulazimisha yake.

Haipo sheria hii pia. Kilichopo ni kuwa kila mtu anayo haki ya kujiunga na chama chochote kilicho sajiliwa.

Utakapojiunga utakuta vyama ambavyo kama binadamu ni hai vina falsafa yenye kuzaa imani, sera na misimamo tofauti. Ni kwa kuzingatia haya vyama hutofautiana na hivyo "options" za wapi uende huwepo.

Tofautisha hapa na Simba au Yanga ambako majina, rangi, mahaba au ushabiki ndivyo huamua mtu ajiunge wapi.

Uhai wa chama ni katika falsafa, Imani, sera na misimamo yake. Bila hayo chama ni mfu. Matokeo yake ndiyo yale ya kukosa misimamo, kujipanga kuelekea chaguzi bila kujali juzi tuliamua nini, nk.

Mgogoro wa wabunge hawa na chama ni kukiukwa Kwa msimamo wa chama wa kutoshiriki kwenye bunge batili kwa niaba ya chama.

Mengine yote ni mbwembwe tu labda katika kujaribu kuurefusha msamiati.

Mkuu vyama hivi vina usajili ambapo manifesto zao na makabrasha lukuki hukabidhiwa kwa msajili Kwa tathmini kabla ya usajili.

Falsafa na imani za chama ni documented. Misimamo kwenye yatokanayo ni kwa mujibu wa falsafa na imani.

Imani na misimamo ya chama kama zilivyo za watu, inaratibiwa na dola. Kulikoni kuongelea visivyoweza kuwepo kwani kama chama ni halali kitakuwa kina imani na misimamo iliyo halali?

Misimamo na imani za chama kuhusu lolote haziwezi kuwa siri au kutokuwapo bali kwa chama mfu.

Angalizo:

Ndiyo maana CCM ni wahuni kwa sababu CCM hii siyo ile ya Nyerere na hawa waliomo aina ya Bashite, Joni na wenzao ni wasaka fursa tu.

Hawa wasingekuwa na nafasi kwenye CCM ya Nyerere.
Sasa unaposema haipo hiyo sheria naona unazidi kupotea njia, sheria ipo inayomtaka yeyote kujiunga na chama chochote apendacho na hatakiwi kutengwa kwa kuhusisha rangi, kabila, dini yake au vinginevyo.

Kutoka hapo sasa, ndio mtu huyo ataangalia chama kile anachoona kinamfaa kwa kuzingatia hizo imani na misimamo yako unayoipigania, ambayo kwangu bado napingana nayo kwasababu kuna wakati inaweza kukiuka haki za makundi mengine kama hao LBTQ niliokutajia.

Mimi naona tuishie hapa tuwaachie na wengine waje kuweka mawazo yao, right?

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Sasa unaposema haipo hiyo sheria naona unazidi kupotea njia, sheria ipo inayomtaka yeyote kujiunga na chama chochote apendacho na hatakiwi kutengwa kwa kuhusisha rangi, kabila, dini yake au vinginevyo.

Hapa sasa ni sawa. Linganisha kamili na kile ulichokuwa umeandika awali.

Kutoka hapo sasa, ndio mtu huyo ataangalia chama kile anachoona kinamfaa kwa kuzingatia hizo imani na misimamo yako unayoipigania,

Hili sipiganii. Vyama vya siasa siyo vyama mpira. Hapa ndipo ambapo wafuasi wanaweza kuwa tayari kuipigania Imani na misimamo yao ikibidi hata kuifia.

ambayo kwangu bado napingana nayo kwasababu kuna wakati inaweza kukiuka haki za makundi mengine kama hao LBTQ niliokutajia, mimi naona tuishie hapa tuwaachie na wengine waje kuweka mawazo yao, right?

1. Haya ya siasa za kimachale machale, kiwizi wizi, kiujanja ujanja, nk, haisaidii.

2. Imani au msimamo wa nchi, chama au mtu kuyahusu haiwezi kuwa jinai.

3. Ni tatizo la msingi sana tuna vyama wafu vyenye imani na misimamo isiyojulikana.

4. Ndiyo maana safari ya ukombozi kwa mwendo huu haiwezi kuwa na mafanikio leo au hata kesho.
 
Hapa sasa ni sawa. Linganisha kamili na kile ulichokuwa umeandika awali.

Hili sipiganii. Vyama vya siasa siyo vyama mpira. Hapa ndipo ambapo wafuasi wanaweza kuwa tayari kuipigania Imani na misimamo yao ikibidi hata kuifia.

1. Haya ya siasa za kimachale machale, kiwizi wizi, kiujanja ujanja, nk, haisaidii.

2. Imani au msimamo wa nchi, chama au mtu kuyahusu haiwezi kuwa jinai.

3. Ni tatizo la msingi sana tuna vyama wafu vyenye imani na misimamo isiyojulikana.

4. Ndiyo maana safari ya ukombozi kwa mwendo huu haiwezi kuwa na mafanikio leo au hata kesho.
Kwa dhana hiyo, kwangu naona siasa za kimachale machale kama unavyoziita haziepukiki, kwasababu wakati mwingine siasa ni kama upepo, hazipo static, unaweza kujikuta unamfungia mtu vioo sasa hivi, ajabu ukashangaa kesho unamuhitaji kuunganisha nguvu.

- Hivyo unaposema tuna vyama vya wafu unakosea, huu ni uhalisia ambao lazima kuuishi, huwezi kuwa chama cha siasa ukajichagulia wenye tabia za kufanana nawe, na kuwatenga wengine, mbele itakugharimu, au kama lengo lako sio kukamata dola.

Naamini ndio maana hata wewe mwenyewe huwa ni muumini wa kutokukumbuka makosa ya wengine wakati wa kupigania jambo, mfano kwenye Katiba Mpya, umekuwa ukisisitiza sana hilo, sasa huoni ule mtazamo wako wa mwanzo unapingana na hili la "msimamo na imani" unalosisitiza hivi sasa?

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Kwa dhana hiyo, kwangu naona siasa za kimachale machale kama unavyoziita haziepukiki, kwasababu wakati mwingine siasa ni kama upepo, hazipo static, unaweza kujikuta unamfungia mtu vioo sasa hivi, ajabu ukashangaa kesho unamuhitaji kuunganisha nguvu.

1. Siasa za kimachale machale ni za kinafiki, hazikubaliki na hazina tija:

2. Mtu asiyeamini kwenye mnachopigania anaweza kujitoa vipi kamili kwa mapambano?

3. Hapa ndipo kama taifa tulipo feli; hatujui tunataka au hatutaki nini na kwa nini.

4. Bila kuyajua haya tunapigana vita tulivyoshindwa.

- Hivyo unaposema tuna vyama vya wafu unakosea, huu ni uhalisia ambao lazima kuuishi, huwezi kuwa chama cha siasa ukajichagulia wenye tabia za kufanana nawe, na kuwatenga wengine, mbele itakugharimu, au kama lengo lako sio kukamata dola.

1. Bila watu kujua haki; iwe umeme, maji, bei ya mafuta, nauli, katiba, nk hupiganiwa na kwa nini, kitu gani nani atahoji wapi?

2. Sidhani Lissu kuwa anaweza kuwa na msimamo duni kama huu wako.

3. Pana haja ya kumtaka kufafanua mambo mengi zaidi kumbe, kwa mtaji huu.

4. Kwa hakika kumbe kiza chaweza kuwa ni kinene zaidi nadhani, kwa mwendo huu.

Naamini ndio maana hata wewe mwenyewe huwa ni muumini wa kutokukumbuka makosa ya wengine wakati wa kupigania jambo, mfano kwenye Katiba Mpya, umekuwa ukisisitiza sana hilo, sasa huoni ule mtazamo wako wa mwanzo unapingana na hili la "msimamo na imani" unalosisitiza hivi sasa?

1. Mimi ni muumini kindaki ndaki wa kutokumbuka makosa ya watu.

2. Falsafa ya chama haihusu makosa ya watu bali misingi ya chama.

3. Kwamba chama kinasimamia nini; kuwa kinapigania usawa na haki? Kinaamini kwenye uhuru? nk. Nk.

4. Wapi kinapingana na nini nilichosema au kuandika popote?
 
1. Siasa za kimachale machale ni za kinafiki, hazikubaliki na hazina tija:

2. Mtu asiyeamini kwenye mnachopigania anaweza kujitoa vipi kamili kwa mapambano?

3. Hapa ndipo kama taifa tulipo feli; hatujui tunataka au hatutaki nini na kwa nini.

4. Bila kuyajua haya tunapigana vita tulivyoshindwa.

1. Bila watu kujua haki iwe umeme, maji, bei ya mafuta, nauli, katiba, nk hupiganiwa na kwa nini, kitu gani nani atahohi wapi?

2. Sidhani Lissu kuwa anaweza kuwa na msimamo duni kama huu.

3. Pana haja ya kumtaka kufafanua mambo mengi zaidi Kwa mtaji huu.

4. Kwa hakika kiza chaweza kuwa ni kinene zaidi Kwa mwendo huu.

1. Mimi ni muumini kindaki ndaki wa kutokumbuka makosa ya watu.

2. Falsafa ya chama haihusu makosa ya watu bali misingi ya chama.

3. Kwamba chama kinasimamia nini; kuwa kinapigania usawa na haki? Kinaamini kwenye uhuru? nk. Nk.

4. Wapi kinapingana na nini nilichosema au kuandika popote?
Aisee sikuelewi kabisa, hapa unatetea siasa za makundi kujitenga kwa wenye msimamo unaofanana, pale unadai wewe ni muumini wa kusahau makosa ya wengine, mwenyewe unajielewa kweli?!

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Falsafa inatoka wapi ? Kwa viongozi..., Wanachama, Wafuasi au Mkusanyiko wa hao wote ? Au ni Ideology fulani ambayo watu wenye msimamo kama huo sawa wanakutana na ku-form Mkusanyiko wao ?

Nadhani kuna Core Values ambazo watu wanaenda kule na haziwezi kubadilika..., hayo mengine hata ndani ya Katiba Mpya; Vita n.k. sio lazima watu wawe na msimamo sawa... (People are Different) but the Core values ndio zilizopelekea hao watu waende huko in the first place (These should Never Change).... Ingawa in this day and age Vyama ni Platform ya Kupata kura ili kwenda Kula
 
1. Wapi usipopaelewa ndugu?

2. Kujitenga na tusiokuwa na falsafa, Imani, malengo au misimamo inayofanana nao kwa nini ni tatizo kwako?

3. Kwamba huna taabu hata kiongozi wetu kwenye madai yetu ni Bashite, Samia au Msukuma wa CCM huko?

4. Kwa nini unadhani kusamehe makosa ya mtu ya nyuma aliyoachana nayo leo, ni sawa na kuwa na mbumbumbu anayeendelea kulisukuma gari nyuma, wengine tunapolisukuma kwenda mbele?

5. Hapa kwenye kushindwa kufahamu umuhimu wa kuwa na falsafa, Imani na misimamo ya chama inayofahamika, unajielewa kweli?

6. Clip hiyo ya Nyerere (Rip) ina maana yoyote kwako?
 
Falsafa inatoka wapi ? Kwa viongozi..., Wanachama, Wafuasi au Mkusanyiko wa hao wote ? Au ni Ideology fulani ambayo watu wenye msimamo kama huo sawa wanakutana na ku-form Mkusanyiko wao ?

1. Falsafa inatoka kwa waanzilishi.

2. Vyama huundwa kwa sababu fulani.

3. Vya kisiasa vikiwa na malengo ya kisiasa kwa misingi au mqlengo fulani.

4. Democrats au Republicans, Greens, liberals, conservatives, nk, si majina ni falsafa zao zinazo zaa imani na misimamo tofauti.

5. Tofautisha misimamo ya mtu mmoja mmoja na misimamo ya chama ambayo ni entity hai.

6. Chama hakiwezi kukosa imani au msimamo kwenye jambo lolote.

7. Kutegemeana na falsafa ya chama Imani zake na misimamo yake kwenye lolote haiwezi kuwa by accident.

8. Chama ni mkusanyiko wa watu wenye imani moja; ndiyo maana CCM na CDM ni mafuta na maji.

9. Ukiwa chamani na imani na msimamo tofauti na wa chama unafuzu kunyimwa dhamana ya chama.

10. Indeed hata ukiondoka ni sawa. Chamani ukitofautiana na misingi ya chama unapoteza sifa.

Nadhani kuna Core Values ambazo watu wanaenda kule na haziwezi kubadilika..., hayo mengine hata ndani ya Katiba Mpya; Vita n.k. sio lazima watu wawe na msimamo sawa... (People are Different) but the Core values ndio zilizopelekea hao watu waende huko in the first place (These should Never Change).... Ingawa in this day and age Vyama ni Platform ya Kupata kura ili kwenda Kula

1. Msikie Nyerere kwa mfano:

Chini ya falsafa ya CCM wakati huo ubaguzi ni haramu. Imani hiyo na msimamo thabiti tokea kwenye falsafa. Hilo halina mjadala.

2. Kwamba wewe ni mbaguzi? Si mwenzetu bila kujali lingine lolote. Unaweza kuwapo ila uko wrong place, hufuzu kupewa dhamana ya chama.

3. Kwamba tunaamini kwenye uhuru:

IMG_1567.jpg

1. Huamini kwenye uhuru na demokrasia? Si mwenzetu. Wewe huwezi kuwa kiongozi wetu. Hauna thamani kwetu. Hufuzu kupewa dhamana chamani.

2. Beberu hutaka kujua misimamo ya wagombea kwenye mambo nyeti na ya msingi yakiwamo: utoaji mimba, LGBTQ, vita nk. Yote hayo tamo kwenye Imani na misimamo tokea kwenye falsafa zao.

3. Una msimamo na Imani tofauti za chama? Si mwenzetu, unaweza kuwepo ila hufuzu kupewa dhamana ya chama.

4. Tafsiri kamili kuwa uko mahali sipo. Utachagua mwenyewe kusuka au kunyoa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom