Jinsi ya kuwa na uwezo wa kutunza siri zako, kama huna siri elewa huna maisha

BAKIIF Islamic

JF-Expert Member
Jul 11, 2021
594
1,827
Ndugu Msomaji wa makala za BAKIIF.
Bila shaka unampenda MUNGU Sana, tunaamini hivyo japo hufuati amri zake, lipo kusudi la Mungu kutaka kukusaidia jambo Fulani ikiwa uko tayari katika yote jiepushe na mafundisho yasiyokuwa ya ki-MUNGU.

Siri ni mipango iliyo ndani ya moyo wa mtu juu ya hatima ya maisha yake, kila jambo unalolipanga ndani ya Moyo wako fahamu hiyo ndiyo siri yako, hakuna mtu awezaye kufahamu mipango iliyo ndani ya mtu bila kuambiwa, watu wengi wamevuruga maisha yao bila ya kujuwa sababu ni ipi.

Kuna watu wamefukuzwa kazi na wengine wameshushwa vyeo kwa sababu ya kutoa siri zao wengine wameharibu biashara wengine masomo wengine uchumba wengine ndoa zao zimevunjika kabisa, kwasababu ya kutoa siri. Sasa Mungu ametupatia nafasi hii tujifunze ili tupate maarifa ya kutunza siri zetu.

Kumcha-Mwenyezi MUNGU ni kumtumaini Mungu kwa kila jambo lako na kuyashika maagizo yake yote na kuyatenda ndipo atakupatia maarifa na hekima ya hatima ya maisha yako, ila utapodharau mafundisho ya MUNGU hayatakusaidia popote kwa kalolote.

Kwakuwa maandiko yametufundisha kuwa siri hukaa moyoni mwa mwanadamu basi shughuli kubwa kumbe inafanyikia moyoni mwa binaadamu, hivyo kumbe ili ufanikiwe unatakiwa kujuwa namna ya kutunza siri zilizo moyoni mwako.

Na kwa hivyo unatakiwa kuulinda Moyo wako maana ndiko mipango yote inafanyikia na ndiyo sehemu salama ambayo hakuna mtu awezaye kujuwa unapanga nini juu ya maisha yako, kila mtu ana mipango mingi au kidogo juu ya hatima ya maisha yake ila Mipango mingi haijakamilika sababu ya kutoa siri ya mipango yako kabla hata haijakamilika.

Siri yako ndiyo mafanikio yako yote, Siri yako ndiyo mipango yako yote, Siri yako ndiyo Maisha yako yote, Siri yako ndiyo uzima wako wote.

Kufanikiwa au kuinuliwa na Mungu kunatokana na wewe kutotoa siri yako kwa Mtu yeyote Yule, awe Rafiki au mchumba, mke, Mume, Baba au Mama usikubali kutoa siri zako au kuwaambia ambia watu mipango ya moyoni Mwako.

Yapo madhara unayoweza kuyapata kama utatoa siri yako kwakuwa watu wengi wanataka kujuwa siri yako ili wappate njia ya kukuingia.

Kwakuwa siri zote ndiyo mipango yetu yote ya moyoni unatakiwa kuwa makini na kujihadhari sana na wale watu wote wa karibu yako, kwa mfano wazazi, mke au mume, mtoto wako, mchumba, mfanyakazi mwezako, mfanyabiashara mwezako, Rafiki yako wa karibu usiwaamini kupita kiasi na kuanza kuwaambia siri zako zote.

Kwetu sisi waislamu MUNGU aliliweka bayana swala hili mapema kabisa alisema kwamba
''Enyi mlioamini! Hakika miongoni mwa wake zenu na watoto wenu ni maadui kwenu, basi tahadharini nao. Na mkisamehe na mkapuuza na mkayafutilia mbali, basi hakika MUNGU ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu'' (At-Taghaabun: 14)

Pia MUNGU alimsema kwamba
''Na jueni kwamba mali zenu na watoto wenu ni jaribio, na kwamba kwa MUNGU uko ujira adhimu.
(Al-Anfaal: 28)

Sasa tuendelee na mada yetu ya kutunza siri
Ujua ndugu, MUNGU mwenyewe kuna vitu amevifanya kuwa siri, hakuna kiumbe chochote kinacho fahamu siri hizo, baadhi ya siri za MUNGU walipewa mitume na manabii. Na hadi leo kifo kimekuwa ni siri kubwa anaye ifahamu ni MUNGU pekee, hakuna kiumbe chochote kinacho fahamu siri ya kufa kwake itakuwa lini.

Siri ni jambo muhimu ndio maana hata mitihani mashuleni na vyuoni imefanywa kuwa ni siri tena inasimamiwa na ulinzi mkali.

Kumbe kuna mambo ambayo hatuyajui hatujayajuwa na hatutayajuwa kutoka kwa Mungu Hadi ametaka tuyajuwe Siri ya Bwana iko kwao wamchao, Naye atawajulisha agano lake. Kwahiyo kumbe hata kuyajuwa mambo ya Mungu ni lazima uwe mchaji wake ili aweze kukupatia siri ambazo hajaambia wengine.

Usikubali kusema siri zako kwa Mwanadamu yeyote Yule Hata kama ni kiongozi wako mahali pa kazi au biashara au Rafiki mlioshibana kushibana ni maneno tu hayo huyo huyo unayesema mmeshibana ndiye adui yako mkubwa.

Kutokubali kufunguwa Mlango wako hovyo hovyo, yaani kinywa chako kiwe na ukiasi na kichaguwe maneno ya kuongea na yakutoongea, ukilinda mdomo wako vizuri kwakuto toa siri zako kutomchokoza Mungu kwa kinywa chako Moyoni mwako kutakuwa salama na siri zako zitakuwa salama zote na hatima ya maisha yako itakuwa tofauti sana na wengine utajishangaa wewe na wengine watakushangaa pia, sasa weka kitanzi kinywani mwako kwanzia sasa juu ya siri zako.

Kinywa chako kinauwezo wa kuusababishia Mwili wako matatizo usipikuwa makini nao, pia kila mwanadamu Mungu amempa malaika waawili (Rakib" na "Atid.) kwa kuwa naye wakati wote anapotenda matendo mema ya Mungu ukimkosea huyu malaika umemkosea Mungu mwenyewe, na Mungu ataharibu kazi ya mikono yako chunga sana kinywa chako.

Inawezekana umenuniana na jirani yako kwasababu ya kinywa chako au umenuniana na mkeo au mmeo au mtoto kwa sababu ya kinywa chako tu, juwa kwamba humkomoi mtu bali unamkasirisha Malaika wa Mungu na MUNGU mwenyewe.

Kama unaona huelewani na watu kwasababu yakinywa chako tafuta msaada kwa Mwenyezi MUNGU akuongoze ili uwe salama vinginevyo ni hatari sana kutumia kinywa vibaya.

BAKIIF ISLAMIC
+255755351262
Ubungo municipal, Kimara
Dar es Salaam, Tanzania.
 
Inshallah sheikh tumekuelewa " siri ndo ufunguo Wa mafanikio
 
Back
Top Bottom