Venus Star
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 19,991
- 60,915
UTANGULIZI
Kwetu hapa Tanzania kilimo ni uti wa mgongo. Hata duniani kote watu wanategemea mazao yatokanayo na kilimo. Kwetu hapa Tanzania tumekuwa na kilimo cha jembe la mkono kwa muda mrefu sana. Zamani wazazi wetu walikuwa wakiwafundisha vijana wao namna iliyo bora ya kushika mpini wakati wa kulima. Lakini kwa sasa wazazi na watu wazima hawawafundishi vijana wao namna ya kushika mpini pindi wanapokuwa shambani.
Hii imesababisha vijana wengi kuwa wazembe na kushindwa kujipatia vipato vyao kutokana na kilimo. Vijana wengi wanakuwa wanasaidiwa na vibarua kwenye mashamba yao kwa sababu hawana ujuzi wa kushika mpini ili waweze kulima.
Siku ya leo nimewiwa kuleta elimu ya ushikaji wa mpini kupitia mtandao wa kijamii ili kuelimisha baadhi ya watu ambao hawajui.
MKONO GANI UNATANGULIA KWENYE MPINI WAKATI WA KULIMA?
Hapa inategemea mtu na mtu. Kuna watu wengine mkono wenye nguvu ni mkono wa kulia lakini kuna watu wengine mkono wa kushoto ndio wenye nguvu.
Kama mkono wa kulia ndio wenye nguvu ni vyema ukatanguliza mkono wa kushoto kisha mkono wa kulia ukashika kwa nyuma.Mkono wa kushoto ukitangulia unakuwa kama pivot. Lakini kama wewe uwezo wako upo kwenye mkono wa kushoto ni vyema ukatanguliza mkono wa kulia kisha mkono wa kushoto ukashika kwa nyuma. Mkono kushika kwa nyuma maana yake huo mkono ndio wenye nguvu unaendesha namna ya ulimaji.
Lakini ni vyema kuanza kujifunza kutumia mikono yote. Hii itakusaidia wakati mkono mmoja umechoka kukaa nyuma unageuzia mkono mwingine ili kuupumuzisha mmoja.
Nitaendelea......