agudev
Member
- Apr 5, 2016
- 76
- 122
Habari zenu wanaJF na hongereni na majukumu ya kuendeleza taifa hili.
Kama kichwa cha uzi kinavyojieleza, nimekuwa nikitatizwa na hili swali kichwani na nimejaribu kuuliza watu mbalimbali hasa Wakristo waliooa, majibu niliyopata mpaka sasa kusema kweli hayajaniridhisha kwani inaonekana watu huvaa pete mkono wa kushoto kwa vile kila mtu anafanya hivyo. Je uvaaji wa pete hii hauna maana yoyote?
Naangalia namna mkono wa kushoto unavyochukuliwa katika jamii zetu kama mkono usiofaa, mkono mchafu na mkono wa chooni, basi kama hili ni kweli iweje tuwe tunautumia mkono kuweka ishara ya uaminifu na upendo. Ndoa ni kiapo na kifungo chetu cha upendo na uaminifu na upendo mbele ya Mungu na mwenza wetu, ni ishara ya kukubali kujifunga maisha yetu na kuishi maisha ya nidhamu ya kujizua tamaa zetu za mwili, kujitoa kwa kushirikiana na mwenza wetu kuweza kujenga jambo lililo kubwa kuliko sisi ambalo ni familia. Ikiwa hivi vyote ni kweli, kwa nini basi tunaweka ishara inayowakilisha uzito wa maamuzi ya maisha yetu mkono ambao tunauchukulia kama mkono najisi?
Kawaida ni mwiko kabisa kutumia mkono wa kushoto kufanyia vitu muhimu; huruhusiwi kula kwa mkono wa kushoto, huruhusiwi kusali kwa mkono wa kushoto, huruhusiwi kumpa mtu kitu kwa mkono wa kushoto, kusalimia kwa mkono wa kushoto, kutoa sadaka kwa mkono wa kushoto n.k, ina maanisha ndoa ina thamani ndogo sana kuliko namna ya kula chakula, kutoa salamu n.k?