Jinsi ya kushika mpini shambani

Venus Star

JF-Expert Member
Dec 6, 2018
19,680
59,801
UTANGULIZI
MPINI-640x459.jpg

Kwetu hapa Tanzania kilimo ni uti wa mgongo. Hata duniani kote watu wanategemea mazao yatokanayo na kilimo. Kwetu hapa Tanzania tumekuwa na kilimo cha jembe la mkono kwa muda mrefu sana. Zamani wazazi wetu walikuwa wakiwafundisha vijana wao namna iliyo bora ya kushika mpini wakati wa kulima. Lakini kwa sasa wazazi na watu wazima hawawafundishi vijana wao namna ya kushika mpini pindi wanapokuwa shambani.
Hii imesababisha vijana wengi kuwa wazembe na kushindwa kujipatia vipato vyao kutokana na kilimo. Vijana wengi wanakuwa wanasaidiwa na vibarua kwenye mashamba yao kwa sababu hawana ujuzi wa kushika mpini ili waweze kulima.
Siku ya leo nimewiwa kuleta elimu ya ushikaji wa mpini kupitia mtandao wa kijamii ili kuelimisha baadhi ya watu ambao hawajui.
MKONO GANI UNATANGULIA KWENYE MPINI WAKATI WA KULIMA?
Hapa inategemea mtu na mtu. Kuna watu wengine mkono wenye nguvu ni mkono wa kulia lakini kuna watu wengine mkono wa kushoto ndio wenye nguvu.

Kama mkono wa kulia ndio wenye nguvu ni vyema ukatanguliza mkono wa kushoto kisha mkono wa kulia ukashika kwa nyuma.Mkono wa kushoto ukitangulia unakuwa kama pivot. Lakini kama wewe uwezo wako upo kwenye mkono wa kushoto ni vyema ukatanguliza mkono wa kulia kisha mkono wa kushoto ukashika kwa nyuma. Mkono kushika kwa nyuma maana yake huo mkono ndio wenye nguvu unaendesha namna ya ulimaji.

Lakini ni vyema kuanza kujifunza kutumia mikono yote. Hii itakusaidia wakati mkono mmoja umechoka kukaa nyuma unageuzia mkono mwingine ili kuupumuzisha mmoja.

Nitaendelea......
 
Mleta Uzi wewe una balaa Sana!hakuna kanuni za kushika mpini hapo inategemea ardhi na ardhi nyingine kavu Sana nyingine Zina unyevu Sasa mkulima atajiongeza mwenyewe
Kwenye ardhi kavu mkulima anatakiwa kutumia nguvu. Lakini kuna ardhi ya mfinyanzi pia ambapo udogo huwa unanata kwenye jembe. Kwahiyo ni muhimu sana kuwafundisha vijana wa sasa namna ya kushika mpini wakati wanalima kwenye ardhi tofauti tofauti.
 
Pia Kuna udongo tifutifu,una rutuba Sana hapo ukipiga jembe Mara mbilli tatu hutumii nguvu Ila utarajie kuota kwa mazao yaliyostawi vizurii kazi inabaki kupalilia
 
Pia Kuna udongo tifutifu,una rutuba Sana hapo ukipiga jembe Mara mbilli tatu hutumii nguvu Ila utarajie kuota kwa mazao yaliyostawi vizurii kazi inabaki kupalilia
Vijana wa siku hizi mazao yakiota tu wanakuwa wavivu wanakimbia na kulitelekeza shamba. Inambidi waelezwe kuwa hapa nchini kilimo ni uti wa mgongo.
 
Vijana wa siku hizi mazao yakiota tu wanakuwa wavivu wanakimbia na kulitelekeza shamba. Inambidi waelezwe kuwa hapa nchini kilimo ni uti wa mgongo.
Hivi tatizo Ni Nini?yaani wanalima vizuri tu,wanapanda mbegu nzuri tu,mazao yakichomoza tu wao mbiooo,,haya Ni matumizi mabaya ya ruzuku!
 
Hivi tatizo Ni Nini?yaani wanalima vizuri tu,wanapanda mbegu nzuri tu,mazao yakichomoza tu wao mbiooo,,haya Ni matumizi mabaya ya ruzuku!
Tatizo ni uzembe wa kupalilia na kuvuna mazao. Halafu jua likipiga kidogo tu vijana wanayaacha mashamba yao na kukimbilia mjini.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom