Jinsi ya kupika ubuyu wa Zanzibar

lissa david

Member
Mar 3, 2017
45
12
Wana jamvi,

Naomba mnisaidie kunielekeza jinsi ya kupika ubuyu wa Zanzibar ule unao kuwa mlaini maana mimi nilijaribu lakini unatoka mgumu hauwi mlaini na wenye unga, nifanye nini?.

=========

Jinsi ya kupika Ubuyu

Mahitaji.

1. Sukari vikombe 2
2. Maji vikombe 2
3. Nusu kikombe unga wa ubuyu
4. Vikombe 4 ubuyu wenyewe
5. 1/4 pili pili ya unga
6. 1/4 tsp chumvi
7. 1/4 tsp iliki ya unga
8. Rangi nyekundu au yeyote ile utakavyopenda.

Namna ya kufanya.
1. Katika sufuria,weka maji na sukari na chumvi na pili pili ya unga na Rangi na iliki. Moto uwe juu kiasi na changanya vyote hivyo vipike vizuri.

2. Wakati vitu vinaanza kujipika utakuta rojo linatoa mapovu. Endelea tu kukoroga acha rojo lipikike vizuri. Baada ya hapo mapovu yakianza kutulia inamaanisha kua rojo limeanza kua zito.

3. Sasa hapo chota kidogo katika mwiko na test kwa vidole kama rojo linanata ua halinati. Rojo linatakiwa linate ndio linakua limeiva. Lisinate San kiasi tu.

4. Kisha mimina ubuyu wa kokwa na changanya vizuri kabisa katika rojo. Endelea kupika vizuri kama dakika 2 hivi. Kisha mimina unga wa ubuyu na changanya vizuri tena.

5. Endelea kupika mpaka unaona sukari inaanza kuganda na kung'aa na kushika vizuri katika ubuyu. Hapo sasa zima jiko na mimina ubuyu katika sinia kubwa na acha ubuyu upoe.

Ukishapoa ubuyu tayari kuliwa.
 
Wana jamvi naomba mnisaidie kunielekeza jinsi ya kupika ubuyu WA Zanzibar ule unao kuwa mlain maana mm nilijaribu lakin unatoka mgumu hauwi mlain na wenye unga.nifanye nn
Wakati wa kupika hakikisha unaweka ubani na udi.
 
kwann unasema siji kujua maisha we mungu au nabii
Hahahaaaaaa....
Hizo ni siri za kibiashara ndugu yangu ni vigumu kuzijua... sio ww tu unaye tamani kujua, hata mm natamani pia lakini sintoweza...
Mm nilikuwa zanzibar, hata ukienda pale wanapo tengeneza huwezi kuona unavyo tengenezwa..
 
Ha

haya
 
vanila inabid niweke kwenye Yale maj ambayo yanachemkia au nikiweka ubuyu
Afu sikia ubuyu hupiki kama ugali fanya hivi chemsha maji pembeni baada ya kuchemka yatie sukari (sukari kali ndo nzuri zaidi) vanilla na radha (kama utapenda) baada ya mchanganyiko wako kuiva ipua hayo maji sasa Chukua beseni au sufuria chini weka ubuyu wako ndani ya beseni Anza kumimina hiyo juice yako kidogo kidogo huku ukiuchanaganya kwa mikono safi
Ila hakikisha pembeni una Unga wa ubuyu ulio changanywa na mchanganyiko huohuo
Baada ya ubuyu wako kuchanganyika vizuri (usiwe rojo) Anza kumiminia ule unga kwa juu ili uwe mkavu mkavu na kutoa ule ubichi alafu uanike upoe ukisha poa ule ugumu hutouona tena Mkuu

Endelea na ujasiliamali nimeuza sana kipindi nipo chuo
 
Asa

asant Sana mpendwa umenipa elimu pana sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom