Jinsi ya kupika chapati laini na zenye ladha nzuri

Mie huwa nakandia samli naichanganya na extra virgin olive oil kidogo na maji ya baridi. Ila wakati nazikaanda natumia mafuta kdg tu...ntakuekea chapati zangu lol uzione

nitajaribu recipe hii mie huwaga nazinunua kwenye mgahawa mmoja mwananyamala lakin sikuwah kujua recipe yake.
however samli kukandia chapati ni nzuri sana manake chapati zinakuwa laini na ladha nzuri sana.

kuna aina nyingine ya chapati nimezila jana zenyewe nazo ni nzuri sana na upish wake unatofauti kidogo na huu wa kawaida ngoja nijaribu kuizpika nikiweza nitawaletea recipe yake.
 
nitajaribu recipe hii mie huwaga nazinunua kwenye mgahawa mmoja mwananyamala lakin sikuwah kujua recipe yake.
however samli kukandia chapati ni nzuri sana manake chapati zinakuwa laini na ladha nzuri sana.

kuna aina nyingine ya chapati nimezila jana zenyewe nazo ni nzuri sana na upish wake unatofauti kidogo na huu wa kawaida ngoja nijaribu kuizpika nikiweza nitawaletea recipe yake.

Ok ahsante shukraan...
 
Chapati yachomwa haikaangwi. Nacheka na jibu la kongosho eti mfuniko wa sufuria akikupiga nao unatoka ngeu. Chapati ni mlo rahisi na mwepesi kuandaa ukifuata instructions. Mimi kila jumamosi napika chapati za kifungua kinywa jumapili asubuhi na mlo wa jioni siku ya jumatatu baada ya kazi.

chapati inakaangwa dada shallow frying
 
ahitaji
  • Unga wa ngano (plain flour 1/2 of kilo)
  • Siagi (butter vijiko 2 vya chakula)
  • Yai (egg 1)
  • Chumvi (1/2 ya kijiko cha chai)
  • Hiliki (ground cardamon 1/4 ya kijiko cha chai)
  • Maji ya uvuguvugu (warm water)
  • Mafuta (vegetable oil)


Matayarisho
Weka unga wa ngano katika bakuli la kukandia, kisha tia chumvi na hiliki na uchanganye kwanza, baada ya hapo tia siagi na uichanganye vizuri na unga mpaka ipotee. Baada ya hapo tia tena yai na uchanganye vizuri. Mchanganyiko ukishachanganyika vizuri sasa unaweza kutia maji ya uvuguvugu kidogo, kidogo huku ukiwa unauchanganya ili kupata donge. Baada ya hapo anza kukanda hilo donge mpaka mabuje yote yapotee na unga uwe mlaini, ambapo itakuchukua kama dakika 15. Baada ya hapo tawanyisha unga katika madonge ya wastani (yasiwe makubwa sana au madogo sana) Ukimaliza hapo, andaa kibao cha kusukumia chapati kwa kukitia unga kidogo ili chapati isinatie kwenye kibao. Sukuma donge moja la chapati mpaka liwe flat na kisha weka kijiko kimoja cha mafuta na usambaze. ukisha maliza ikunje (roll). Fanya hivyo kwa madonge yote yaliyobakia.
Baada ya hapo andaa chuma cha kuchomea (fry-pan) katika moto wa wastani. Kisha anza kusukuma chapati (ni vizuri ukaanza na zile ulizozikunja mwanzo ili kuzipa nafasi zile za mwisho ziweze kulainika) ukiwa unasukuma hakikisha zinakuwa flat (na zisiwe nene sana au nyembamba sana) Ukishamaliza hapo tia kwenye chuma cha kuchomea. Acha iive upande mmoja then igeuze upande wa pili. Tia mafuta ama kijiko kimoja kikubwa upande wa chini wa chapati na uanze kuukandamiza kwa juu uku ukiwa unaizungusha. fanya hivyo uku ukiwa unaigeuza kuiangalia kwa chini ili isiungue. ikishakuwa ya brown, geuza upande wa pili na urudie hivyohiyvo mpaka chapati iive. Rudia hii process kwa chapati zote zilizobakia.


Siri ya chapati kuwa laini ni kutia siagi au mafuta ya kutosha kipindi unazikanda na pia kuzikanda mpaka unga uwe laini.
 
Mahitaji

Unga kg 1 na robo

Chumvi kiasi

Samli vijiko 6 vya kulia......vijaze

Mafuta vijiko 5....


Maji ya baridi (yaliowekwa kwa friji).....

Namna ya kutaarisha.....


Weka unga katika bakuli mimina na chumvi changanya vizur


Pasha moto samli iache ipoe kidogo tu then mimina nusu ya hiyo samli katika unga.... nusu iliobaki weka

Changanya vizuri.....

Weka maji hadi utengeneze donge (usiwe maji mengi sana)....

Kanda hadi iwe laini (hii muhimu kwa ajili ya soft chapati).....

Kata maduara ukuubwa upendano then weka kwa nusu saa ilainike....

Sukuma chapati na weka mafuta 1/2 tablespoon alafu kunja na weka pembeni....


Wacha zilainike.....

Sukuma tena utengeneze duara

Kaanga chapati.....tumia 1 tablespoon kwa kila chapati

Tayar kwa kuliwa
 

Attachments

  • 20140718_191746.jpg
    20140718_191746.jpg
    137.2 KB · Views: 4,005
  • 20140718_200932.jpg
    20140718_200932.jpg
    177.4 KB · Views: 3,908

Similar Discussions

Back
Top Bottom