Jinsi ya kupika pilau tamu la Nazi

Aaliyyah

JF-Expert Member
Mar 20, 2022
15,824
37,815
Natumaini mko poa,hongereni Kwa maandalizi ya sikukuu

Leo nimeandaa recipe ya pilau tamu la Nazi,karibun tujifunze

MAHITAJI
1)Mchele kilo moja.
2)Nyama iliyochemshwa Mimi nilitumia nusu
3)kitunguumaji,kata kata wastani
4)kitunguu swaumu kilichosagwa4)viaz mviringo vya wastani vitano.
5)pilaumasala
6)mafuta ya kupikia.
7)Tui la Nazi kulingana na mchele wako
8)iriki na binzari nyembamba,(Huwa natumia Ile halisi ili kuongeza ladha na harufu nzuri kwenye chakula)

JINSI YA KUPIKA
1)bandika sufuria jikoni weka mafuta ya kula kidogo sana kwaajili ya kukaanga kitunguu tu yakipata moto weka kitunguu maji kaanga kikianza kulegea na kubadilika rang weka kitunguu swaumu kaanga hadi viwe rangi ya brown

2) Weka pilau masala pamoja na binzari nyembamba na iriki changanya kidogo
Kisha weka Viazi na nyama

3) Changanya Kwa dakika 3 Kisha weka Tui la Nazi kiasi kulingana na mchele wako weka chumvi koroga uchanganye vizuri kisha acha Tui lichemke

4) Vikichemka weka mchele wako koroga uchanganye funika subiri ukauke

5) Ukishakauka punguza moto acha kidogo Kisha utageuza utaacha Tena kidogouive vizuri, pilau itakuwa tayari
Kinachofata ni kuandaa kachumbari na soda 😄😍😍

Karibuni Kwa nyongeza na maoni

IMG_20231101_214134.jpg

IMG_20231101_214336~2.jpg
 
Mother ndo mpishi wangu Bora wa muda wote, hata apika chumvi nahisi itakuwa tamu tu.

Halafu mi vya hivyo sijui kupika, Labda Hawa majirani zangu wapike Nile tu🤓
Mimi mamaang amebaki shabiki tu nikiwepo kilakitu nipike Kuna siku akanambia sitaki fulani apike hata sielewi 😂😂😂anaweka kilakitu lakn wapi🤣🤣

Hao majirani nipe namba zao niwaambie kitu🤣🤣
 
Mimi mamaang amebaki shabiki tu nikiwepo kilakitu nipike Kuna siku akanambia sitaki fulani apike hata sielewi 😂😂😂anaweka kilakitu lakn wapi🤣🤣

Hao majirani nipe namba zao niwaambie kitu🤣🤣
The best moment naipataga Niki enda home aisee 🤓.
Ni kukaa mezani kusubiri maajabu ya mpishi😂.

Usije nigombanisha na majirani zangu, akati wao wa kishua, mi jobless pro max tu 😂
 
Natumaini mko poa,hongereni Kwa maandalizi ya sikukuu
Leo nimeandaa recipe ya pilau tamu la Nazi,karibun tujifunze
MAHITAJI
1)Mchele kilo moja. 2)Nyama iliyochemshwa Mimi nilitumia nusu 3)kitunguumaji,kata kata wastani 4)kitunguu swaumu kilichosagwa4)viaz mviringo vya wastani vitano. 5)pilaumasala
6)mafuta ya kupikia. 8)Tui la Nazi kulingana na mchele wako 7)iriki na binzari nyembamba,(Huwa natumia Ile halisi ili kuongeza ladha na harufu nzuri kwenye chakula)

JINSI YA KUPIKA
1)bandika sufuria jikoni weka mafuta ya kula kidogo sana kwaajili ya kukaanga kitunguu tu yakipata moto weka kitunguu maji kaanga kikianza kulegea na kubadilika rang weka kitunguu swaumu kaanga hadi viwe rangi ya brown

2)weka pilau masala pamoja na binzari nyembamba na iriki changanya kidogo
Kisha weka Viazi na nyama

3)changanya Kwa dakika 3 Kisha weka Tui la Nazi kiasi kulingana na mchele wako weka chumvi koroga uchanganye vizuri kisha acha Tui lichemke

4) vikichemka weka mchele wako koroga uchanganye funika subiri ukauke

5)ukishakauka punguza moto acha kidogo Kisha utageuza utaacha Tena kidogouive vizuri, pilau itakuwa tayari
Kinachofata ni kuandaa kachumbari na soda 😄😍😍

Karibuni Kwa nyongeza na maoni

View attachment 2948308
View attachment 2948310
Absolutely delectable!

Kwa vile sijui kupika pilau, chicken biryani is the next best thing I’ll settle for…

IMG_6162.jpeg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom