Jinsi ya kupata wazo la bidhaa ya kuuza mtandaoni ndani ya saa 24 tu...

RoadLofa

JF-Expert Member
Mar 22, 2017
1,347
2,957
JINSI YA KUPATA WAZO LA BIDHAA YA KUUZA MTANDAONI NDANI YA MASAA 24 TU

Er3ksfw1W0Bkrfq7j8t_CWRAeUezR3q0RK1BdfOd5zKV5HWSn0tMR6O4CsetHZI4wsvdUkyWdonTot1wd3QtA2GvO2yzuyhvdLA7Ug6SmxuTzcsRr5TwWKWPaNLD9fG7MUbfYnOcpe8y0irwgaEr9A


Najua uwa unasikia story za watu kupiga pesa mtandaoni yaani wanatumia smartphone au PC na internet kupiga mpunga na haujawahi kuwa mmoja kati yao na unatamani nawe upate bidhaa itakayokuwezesha kupiga pesa mtandaoni na haujajua jinsi ya kupata wazo ni bidhaa gani uingie nayo mtandaoni upige pesa basi fuatana nami ninachokwenda kuuelezea ni zaidi ya mchongo kwako…

Zifuatazo ni hatua 5 za kupata wazo la bidhaa ya kuuza mtandaoni ndani ya masaa 24👇

Usianze kutafuta kitu cha kuuza kwanza...HAPANA iyo itakuja baadae unachohitaji kutafuta kwanza ni soko lenye KIU,👇

hapo ndo watu wengi ufail na bidhaa zao kutokana na kutofanya tafiti kuna tatizo gani sokoni ila yeye anaanza na bidhaa kuzipeleka sokoni bila kujua soko linahitaji nini na lina kiu gani, basi ngoja mi nikwambie ni hivi siku zote anzia sokoni( marketing research) angalia kwanza soko linahitaji au kuna tatizo gani sokoni kisha nenda kaandae utatuzi wa ilo tatizo kisha na huakika utatusua,

Pia hakikisha bidhaa unayokuja nayo sokoni isiwe kwenye mfumo wa physical products ili kupunguza gharama na kisingizio cha sina capital ( capital yako hapa na PC yako au Smartphone na internet tu)bidhaa yako inatakiwa i iwe kwenye mfumo wa information product yaani unauza unique information zenye umuhimu wa kusolve tatizo fulani na watu wanaweza kuzinunua kwa mfano: kama sokoni umeona kuna tatizo la obesity na wewe una passion na mambo ya diet unaweza anza kuuza e-books na online courses za jinsi ya kupunguza uzito( weight loss) kupitia social media pages zako kwenye FB,, INSTA, Twitter na unawafanyia mentorship au coaching kisha wanakulipa sometimes unaweza penetrate na physical products kiasi ukawauzia pia, najua unajiuliza sasa ntaipataje iyo product ya kuuza mtandaoni 😀😀 fuatana nami ntakuonyesha kwenye hatua zinazofuata

Uza unachopenda 👇

,unatakiwa kufanya kitu unachopenda yaani kipo kwenye shauku yako ( passion) maana siku zote huwezi furahia kufanya kitu usichopenda na kitu unachokipenda utakijua tu yaani ukikifuatilia uchoki mfano kama hupendi kupika hauwezi fundisha watu kupika, mifano ya passion kwa mfano kama unapenda maswala ya fashion unaweza wauzia watu unique information kuhusu jinsi ya kupangilia mavazi , kwa mfano unapenda maswala ya diet unaweza wauzia watu unique information jinsi ya kupunguza uzito( weight loss) au kama unapenda maswala ya public speaking unaweza kuwauzia watu information za kuwafanya wawe public speakers nk mifano ipo mingi nadhani umenielewa jinsi ya kujua passion yako.

Weka nguvu kwenye shauku( passion) unayochangia na wale unaotaka kuwalenga,👇

unajua ukikifanya kitu unachokipenda uchoki na unakuwa na shauku sana ata wa kuchimba unique information za kuwaletea walengwa wako, na nina hakika ukifanya biashara katika soko lenye interest yako lazima utoboe tofauti na kufanya kitu usichopenda , kwa mfano kama unapenda sana kuogelea na ukaanza kuwafundisha watu jinsi ya kuogelea na hakika utakuwa na shauku kubwa ya kuwaelekeza uku unapiga pesa😀, hadi hapo naamini umeanza kuijua passion yako na ukiipata nakushauri ifanyie kitu kukuingizia pesa .

Sasa ni muda wa kuwa mtaalamu( expert)👇

,najua unajiuliza sasa ntakuwaje expert, amini kuwa expert wa kitu fulani ni rahisi sana sema inatakiwa juhudi ya maana kuchimba unique information kuhusu icho kitu, unaweza tumia siku chache kuanza kuwa expert wa kitu fulani, ni rahisi sana kuuza kwenye soko linalohitaji solution ya tatizo fulani na lipo tayari kupokea iyo solution , ivi unajua kinachowatenganisha expert na mtu wa kawaida ni nini?

Ni taarifa( informations) na ili uwe mtaalamu unatakiwa uwe na information za vitu fulani kuzidi mtu wa kawaida na ili kuwa mtaalamu yakupaswa kujifunza vitu vingi kupitia vitabu, online courses , YouTube, Google , watu na njia nyingine nyingi tu, sema unatakiwa kuhakikisha zinafanya kazi kama inavyotegemewa .

Tangaza utatuzi wa kile kinachowanyima usingizi watu( kama expert) katika soko lako ambacho umeshakisoma na kukielewa vyema, 👇

hapo sasa ukiwa tayari expert na upo vizuri kwenye niche yako kuliko mtu wa kawaida , ndo muda sasa wa kuwapelekea watu utaalamu wako(tumia social media accounts zako) na watakulipa pesa kupitia online courses zako, membership fee, subscription fees, mentorship, coaching, E-books

Ili kupata bidhaa ambayo itauza kama wazimu basi pitia umu👇
  • Chuja zile taarifa kuhusu tatizo lao kisha ziite SIRI
  • Chukua taarifa zile rahisi tu kuzitumia na zinaleta matokeo haraka
  • Halafu hakikisha taarifa za ayo matokeo ni ngumu kuaminika kwa walengwa kiasi kwamba yalete mshangao
P.S: SIRI izo zimeandaliwa kwa msaada wa mentor wangu Amos Nyanda ( Copywriter) Aliyenifundisha jinsi ya kugeuza maandishi kuwa PESA mtandaoni 🙏
 
Online hustle ni rahisi kuiwazia ila kufanikiwa ni pamoto
Mimi nilianza kama passion ila nimekuja kuanza kuona mafanikio baada ya miaka 6
Ni ku-fail , fail , fail, fail , fail , fail , fail , fail , fail , fail, fail , fail , fail , fail , fail , fail , fail, fail , fail , fail , fail Alafu MAFANIKIO

Cha msingi ni kumuweka MUNGU akupe bonge la idea
 
Online hustle ni rahisi kuiwazia ila kufanikiwa ni pamoto
Mimi nilianza kama passion ila nimekuja kuanza kuona mafanikio baada ya miaka 6
Ni ku-fail , fail , fail, fail , fail , fail , fail , fail , fail , fail, fail , fail , fail , fail , fail , fail , fail, fail , fail , fail , fail Alafu MAFANIKIO

Cha msingi ni kumuweka MUNGU akupe bonge la idea
Yes upo sahihi boss cha muhimu ni kuwa na consistency
 
Back
Top Bottom