Jinsi ya kuboresha afya ya mbegu za kiume (sperms)

I am Groot

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
3,727
10,023
Utengenezaji wa mbegu za kiume katika kiwanda cha kutengenezea mbegu katika mwili wa mwanaume (mapumbu) huchukua muda mrefu kuliko wengi wanavyodhani.

Mfumo hutengeneza sperms kila siku, lakini mzunguko kamilifu wa sperm zilizokomaa kabisa unachukua kati ya siku 64 mpaka 74.

Wakati wa mlolongo wa uundwaji au utengenezaji wa sperms, kati ya mbegu zipatazo Millioni kadhaa hutengenezwa kwa siku, na 1,500 kwa kila sekunde.

Mwisho wa utekelezaji mbegu, Mwanaume anaweza kutengeneza mpaka kiwango cha sperms Bilion 8 tayari kwa matumizi. Na kwa kila ejaculation cell za mbegu ya kiume milioni 20 - 300 huachiwa kutoka pamoja na kilainishi maalumu (semen) kwa ajili ya kuzilinda.

JINSI YA KUBORESHA AFYA YA MBEGU ZA KIUME (SPERMS).
  • Fanya mazoezi ya mwili mara kwa mara.
  • Pata vitamin C & D ya kutosha kwa kila mlo.
  • Pata (Lycopene = matikiti, nyanya n.k { antioxidant products}) ya kutosha kila mara.
  • Acha/ punguza uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe
  • Punguza au acha kabisa upigaji puri/ masturbation.
  • Vaa nguo zisizobana sehemu za siri.

N.B: Ubora na wingi wa sperms unategemea na mfumo halisi wa maisha na ulaji wako.

Kula vizuri, kuwa mchangamfu na zuia tabia zinazoweza athiri afya yako kwa kadri uwezavyo.
 
Anhaa sasa pombe imefuata nini tena? Mbona walevi wana watoto.
Kunywa hukatazwi ila punguza. Huo ni uamuzi wa mtu. Unywaji pombe uliokithiri unapunguza kiwango cha testosterone ambayo inachangia kwa ukubwa uzalishaji wa mbegu za kiume.
 
Na ishu ya zero sperm inakuaje?
Hii inaweza tokana na tatizo katika mirija inayopitisha sperms labda kuwa imeziba, hormone imbalance, shida katika testicles na mengine mengi tu yaweza kuwa sababu. Vipimo zaidi vinahitajika.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom