Jinsi ya kuacha kuvuta sigara (A Guide to Quitting Smoking)

Wapendwa Za Mchana.

Mwenzenu kijana wangu amejiingiza kwenye uraibu wa sigara. Kwanza nilikuwa nahisi baadae nimekuja kujua ni kweli.

Tafadhali mwenye kujua dawa ili aache anifahamishe.

Ahsanteni
Amekuambia kama yupo tayari kuacha ? Au unamtafutia dawa halafu mnamfunga kamba na kumnywesha kilazima?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muelimishe madhara ya sigara ukiambatanisha na picha za madhara waliyopata wavuta sigara kama..saratani yakoo...saratani ya mapafu...wagonjwa wa kifua kikuu...nk... hapo atakuelewa...lakini kama ni wewe ndo unavuta alafu unasema mwanao...ujumbe utakuwa umekufikia
Asipoelewa, aende naye tour hospitali akaone watu wanaoteseka kutokana na madhara waliyoyapata kupitia uvutaji wa sigara,naamini akili itamkaa sawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha huruma za kijinga we mwambie achague 1 kati yakuvuta fegi au kuondoka hapo home boy simple 2 lkn nais we mshua mwnyewe ndo unasmoke.
 
Habari wakuu leo leo napenda kuwapa dawa ya kuacha kuvuta sigara kama we n mvutaji na unahitaji kuacha, Nenda dukan kanunue sigara tano(5) unazozitumia zitoe ile tumbaku iliyoko ndani na uiloweke kweny kikombe chenye maji safi lowela kwa usk mzima kisha asubuh yake kunywa hayo maji kwa mkupuo yan bila kusubilisha ukimaliza tulia kama nusu saa arf vuta sigara kama utaimaliza utakuw Tayari umeishapona N.B sio sumu jamani ni salama na ni tiba kweli asanten san nasubilia marejesho kwa watako fanya
 
Habari wakuu leo leo napenda kuwapa dawa ya kuacha kuvuta sigara kama we n mvutaji na unahitaji kuacha, Nenda dukan kanunue sigara tano(5) unazozitumia zitoe ile tumbaku iliyoko ndani na uiloweke kweny kikombe chenye maji safi lowela kwa usk mzima kisha asubuh yake kunywa hayo maji kwa mkupuo yan bila kusubilisha ukimaliza tulia kama nusu saa arf vuta sigara kama utaimaliza utakuw Tayari umeishapona N.B sio sumu jamani ni salama na ni tiba kweli asanten san nasubilia marejesho kwa watako fanya
Mhhh
 
Nimeanza kuvuta sigara nikiwa na umri wa miaka 15. Imekuwa ni kipindi kirefu sasa nimehangaika kujizuia kuacha bila mafanikio na nimejaribu kutumia kila aina ya dawa za tiba asili na za kizungu bila mafanikio.

Imefika mahali kila nikijizuia kuacha nikaa muda mrefu bila kuvuta:

- Najihisi kama mgonjwa yaani kichwa kuwa kizito nakuwa kama sijitambui.

- Baada ya kula najisikia kuchefu chefu.

- Nikishituka usingizini usiku wa manane bila kuvuta sigara basi siwezi tena kupata usingizi mpaka kunakucha nahangaika sana, ila nikivuta 2 naendelea kupata usingizi.

Nina kila sababu ya kuacha ila nashindwa na kuna mabadiliko hata ya kimwili nayaona kabisa hii ni athari ya sigara:

- Kukosa pumzi wakati wa mazoezi ata kukimbia 2 kidogo kufua kuwaka moto.

- Meno yamebadilika rangi kuwa ya kahawia yamepoteza rangi halisi.

- Mwili kulegea baada ya kuvuta.

- Kumkera mke wangu (matumizi ya mdomo kwa sisi watu wazima) hata kiafya inamuathiri pia

Nisaidieni wakuu nina nia kabisa ya kuacha kilevi hiki.

Natanguliza shukrani.
1583051623951.png


MICHANGO ILIYOTOLEWA NA WADAU:
Ukiashaujua kwamba kila kitu binadamu anachokifanya kinaanzia kweny mawazo yake bc ni rahisi kuacha sigara japo mwanzo arosto itakutesa. kwanza fanya hivi jaribu kila unapohisi unatamani kuvuta sigara jaribu kuyahamisha mawazo yako kufikiri vitu vingine (kujisahaulisha) au kucheki movie au kupiga story na marafiki wasiovuta sigara ili wa sikushawishi

Na kingine toa vitu vyote vitavyokufanya utamani kuvuta sigara kama viberiti ,vipisi vya sigara , vifungashio vyake na vinginevyo na kubwa zaid jitahidi kulaa pilipili nyingi kweny vyakula vyako hii itakusaidia kupunguza hamu ya kuvutaa sigara ukiwa umemaliza kulaa.

Ukijaribu kuzingatia hay naona inawez kukusaidia ndani ya wiki au wiki mbili ilaa hii ya kusema punguza kidogo watu wengi haiwasaidii .NAMALIZIA kuacha sigara ni vita kama vita vingine ila ni ni vita kati ya mawazo yako na tamaa za mwili usichukulie lelemama Amua leo na Utaacha

Sent using Jamii Forums mobile app
===
Bro!kama una nia kweli kuacha sigara ni simple sana. Fanya hivi kila siku unapovuta sigara popote utakapokua majivu na kile kishungu vihifadhi sehemu safi may be kwenye mfuko au gazeti safi.Then ukirudi nyumbani andaa glass yako ya maji safi ya kunywa kisha weka vile vishungi na majivu ya sigara kisha funika.

Fanya zoezi hili kwa wiki moja,maji ni yale yale glass moja yafunike vizuri.Baada ya wiki moja chukua chujio yachuje yale maji vizuri kisha yanywe.Kitakachofuata baada ya muda utatapika sana.Baada ya kutapika hiyo ndio itakua tiba yako maana hata moshi wa sigara hutata kuipata tena ile harufu yake.Kila la heri kaka.
===
Sigara ina nicotine, a very addictive substance. Kuiacha inahitaji mkakati maalumu.Mimi nilifanikiwa kuacha kwa kujitrain mwenyewe.Fanya yafuatayo:
1_Punguza idadi ya sigara unazovuta kwa siku.Mfano kama ulikuwa unavuta packet moja kwa siku, puguza hadi sigara 15,10 hadi 5 kwa siku.
2_Jinyime kuvuta sigara usiku ,kama ulikuwa unaamka katkati ya usingizi na kuvuta,acha.
3_Jiepushe na marafiki wavutaji.Ukiwa nao watavuruga mpango wako
4_Endelea kupunguza idadi ya sigara hadi kufika moja kwa siku.
5_Unaweza sasa kuvuka siku nzima bila kuvuta.Ukifika hatua hii,jaribu kuruka hadi siku tatu bila kuvuta,lakini endeleakuhakikisha sigara ni moja tu kwa siku.Ukiweza kufikisha wiki bila kuvuta unaweza kuacha sasa.
Mpango huu niliubuni mwenyewe na ulinisaidia sana kuacha mpaka sasa sivuti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom