Jinsi wanawake wanavyopanga kulia msibani

Jinsi wanawake wanavyopanga kulia msibani

GAZETI

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2011
Posts
5,292
Reaction score
6,773
Siku moja tulikuwa na safari ya kusindikiza maiti kijiji Fulani, Pasipo Bahati
nilichelewa kwenye gari ambalo lilibeba wanaume. Nikalazimika kupanda
Landrover 110 pickup ukiacha dereva mimi ndiye pekee nilikuwa mwanaume
kwenye msafara huo.

Safari ilikuwa ya masaa kama matatu na nusu hivi, kuna sehemu tukafika
Mama mmoja akauliza:
"Tuanzi kwachi ukuta?"(Tuanzie wapi kulia?)
Mwingine akajibu:
"Apalaa pamnandi" (Palee kwenye Mti)
Watatu akasema:
"Apalaa mbali tukahwika karibu na kuchijiji navahaulila."
(Pale mbali tukifika karibu na kijijini nitawaambia)

Kweli baada ya kutembea dakika kadhaa tukafika mwanzo kabisa wa
kijiji ambapo yule aliyesema akaanza kuangusha kilio kikubwa ambacho
kilipokelewa na wenzake.

Hapo wanawake wa kijijini nao wakatupokea kwa vilio huku wakijigalagaza
chini.

Yaani badala ya kuhuzunika nilijikuta nacheka peke yangu.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ungewajoin kulia.
 
Ni sehemu ya maisha. Machozi yanaondoaga stress waache wanaoigiza waigize na wanaoguswa kweli waguswe.
 
Ni sehemu ya maisha. Machozi yanaondoaga stress waache wanaoigiza waigize na wanaoguswa kweli waguswe.
Sawa lakini hii ya kupanga kituo cha kuanzia kulia ilinisisimua asee!
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ungewajoin kulia.
Machozi yangu yako mbali mkuu, niliwahi kuvunjika mguu mpaka
unapona sikuwahi kutoa chozi.
 
Hii ni kweli huku bukoba tupanga kabisa wapi tuanzie kulia wala si jambo ka ajabu ..tunaita kuchula
 
Ukerewe nilishawah kuona wanawake wanajpaka pilipili machoni ili machozi yawatoke mengi na macho yawe mekundu sana,huko pia hupanga kulia pale anapokaribia kufika msibani
 
Ni kweli mkuu, wanaolia njia nzima na wale ndugu wa karibu na marehemu kiasi kwamba mkifika kijijini wengi sauti zinakua zimekata kabisa. Wasindikizaji wengine (wanawake) ni kama hua wana bofya tu switch ya kuanza kulia mnapokaribia kufika. Na hua wanalia kweli, sijui ni mbinu gani wanaitumia ila hua wanalia genuinely. Nahisi hua wanakumbuka matukio ya kusikitisha ya maishani mwao
 
Siku moja tulikuwa na safari ya kusindikiza maiti kijiji Fulani, Pasipo Bahati
nilichelewa kwenye gari ambalo lilibeba wanaume. Nikalazimika kupanda
Landrover 110 pickup ukiacha dereva mimi ndiye pekee nilikuwa mwanaume
kwenye msafara huo.

Safari ilikuwa ya masaa kama matatu na nusu hivi, kuna sehemu tukafika
Mama mmoja akauliza:
"Tuanzi kwachi ukuta?"(Tuanzie wapi kulia?)
Mwingine akajibu:
"Apalaa pamnandi" (Palee kwenye Mti)
Watatu akasema:
"Apalaa mbali tukahwika karibu na kuchijiji navahaulila."
(Pale mbali tukifika karibu na kijijini nitawaambia)

Kweli baada ya kutembea dakika kadhaa tukafika mwanzo kabisa wa
kijiji ambapo yule aliyesema akaanza kuangusha kilio kikubwa ambacho
kilipokelewa na wenzake.

Hapo wanawake wa kijijini nao wakatupokea kwa vilio huku wakijigalagaza
chini.

Yaani badala ya kuhuzunika nilijikuta nacheka peke yangu.


Haaaaaaa! siyo Mbeya hiyo wanajua kulia balaa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom