Jinsi wanausalama wa mtandaoni wanavyowapata watu

Jinsi wanausalama wa mtandaoni wanavyowapata watu

Akili fupi hii mie siye wa kutishwa wewe na utaahira wako fanya ubuku 7 wako kama ulidhani utanitisha mie basi umekula wachuya utasubiri sana.

Duh maneno hayo yako duh kumbe nawewe una maneno machafu hivi duh.. upinzani siwashangai endelea kuisoma namba hadinusage meno. Utajiju.. nipite hukoooo... sipendi akili chafu zenye maneno machafu maishani mwangu..Hapa kazi tu kama kawa.. hiyo buku saba kawaombe wakulipe kama unafikiri wananipatia mimi kuandika yangu humu.. lingine unaonyesha ni mtu kuoga sana kama maneno ya mleta mada yamekutingisha hivyo na unajua mwenyewe kwanini umeichukulia kama big issue kiasi hiki..
 
RAIA WA AFRIKA KUSINI APANDISHWA KIZIMBANI DAR KWA KUTOA VITISHO MITANDAONI
Monday, August 14, 2017 0 Comment Kitaifa


Raia mmoja wa Afrika Kusini, Menolaos Tsampos (61), leo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam akishtakiwa kwa makosa ya kutishia kwa mtandao, kuishi nchini kwa muda wa miaka minne bila kibali na kutumia paspoti yenye visa ya kugushi.

Mshtakiwa huyo aliyefikishwa katika mahakama hiyo leo kabla ya kusomewa mashtaka alitishia kuwapiga waandishi wa habari waliokuwa wakimpiga picha. Tsampos aliyekuwa chini ya ulinzi wa Polisi alikuwa akijaribu kurusha mateke na ngumi akijaribu kuwazuia waandishi wa habari wasimpige picha.

Mtuhumiwa huyo amesomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha ambapo amekana mashtaka yote na amerudishwa rumande hadi hapo upande wa mashtaka utakapothibitisha uhalali wa Visa yake na makazi yake ya kudumu.

Wakili wa serikali, Nassoro Katuga akisoma hati ya mashtaka hayo amedai kuwa, Juni 22, mwaka huu ndani Dar es Salaam, mshtakiwa kwa kutumia mfumo wa kompyuta, alimuandikia barua pepe Costa Gianna Koulos, yenye maneno ya vitisho kwa nia ya kumsababishia Koulos hisia za uoga.

Aidha, mahakama hiyo imeambiwa kwamba, Julai 20 mtuhumiwa huyo alimuandikia barua pepe nyingine Koulos yenye maneno ya vitisho na kumpa masaa 48 kumtaka wakae na kumaliza tofauti walizonazo vinginevyo atamfanyia kitu kibaya.
Katika shtaka jingine, Agosti 7 mwaka huu akiwa katika Kituo cha Polisi cha Kati, Tsampos alikutwa akiwa na pasi ya kusafiria yenye namba M00101612 ikiwa na visa ya kughushi.
Wakili Katuga ameendelea kudai kuwa mshtakiwa huyo mwenye pasi ya kusafiria namba 246184272, raia wa Afrika Kusini, Julai 6, mwaka huu alikamatwa akiishi nchini bila ya kuwa na kibali maalumu.
Mshtakiwa amekanusha kutenda makosa hayo na amerudishwa rumande baada ya mahakama kuutaka upande wa utetezi kufanya uchunguzi na kuhakikisha kama kweli mshtakiwa anaishi mbezi kama ana visa yake.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 16, mwaka huu.
Source: RAIA WA AFRIKA KUSINI APANDISHWA KIZIMBANI DAR KWA KUTOA VITISHO - ZOTE KALI | Blog
 
vipi kuhusu hawa wanaomba namba ya simu eti muwe mnashea aidia kwa wasapu. Inakuaje mtu humfahamu anakuomba namba ya simu mitandaoni muwe mnajadiliana mambo mbalimbali? Kuna wanaofuatilia thread au comment mwisho unaombwa namba ya simu kwa kusifiwa eti unajua kuchangia na kuchambua mijadala mitandaoni
kama nanii?
 
tutachat,tutataniana,tutaflirt hapa and everything ila namba yangu sijawahi fikiria kutoa...
na wala mazoea ya kujuana sana NO...coz i trust no one...
labda uniloge kutumia avatar yangu[emoji27]...ila no way hutaweza pia[emoji38]..i gat Jesus...
Hawa wanaojuana na kukutana nahisi ni wao hao hao "wasiojulikana" Mi huwa nashangaa jinsi wanavyofahamiana na kukutana mara kadhaa hasa Dar.Pia nimesikia mara kadhaa mtu anafika Mwanza na kuwaalika wana jf eti wafahamiane!Mambo yalivyo sasa hivi hata ukisema tu hadharani simpendi Rais hiyo kesi sidhani kama itakuwa na dhamana!Hata kama unamaanisha rais wa tff maana hadi ijulikane hivyo utakuwa umekaa jela muda wa kutosha.Kama tu kwenda kuchangia damu hospitali ni kosa la jinai,basi lazima watu wawe na hofu kubwa ya maisha yao.
 
Hawa wanaojuana na kukutana nahisi ni wao hao hao "wasiojulikana" Mi huwa nashangaa jinsi wanavyofahamiana na kukutana mara kadhaa hasa Dar.Pia nimesikia mara kadhaa mtu anafika Mwanza na kuwaalika wana jf eti wafahamiane!Mambo yalivyo sasa hivi hata ukisema tu hadharani simpendi Rais hiyo kesi sidhani kama itakuwa na dhamana!Hata kama unamaanisha rais wa tff maana hadi ijulikane hivyo utakuwa umekaa jela muda wa kutosha.Kama tu kwenda kuchangia damu hospitali ni kosa la jinai,basi lazima watu wawe na hofu kubwa ya maisha yao.
[emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] . . , mbavu zangu mkuu . . [emoji109]
 
Kwa njia hizo Watuwasiojulikana hawatapatikana Ngo
 
Back
Top Bottom