Jinsi vibaka walivyopeperusha ndoto zangu

Jinsi vibaka walivyopeperusha ndoto zangu

gidlameck

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2016
Posts
618
Reaction score
532
Habarini wana jukwaa kiufupi namshukuru mungu maana bila yeye nisingekuwepo kabisa nakumbuka mwezi wa sita nilipata kibarua mkoani singida cha ujenzi nilianza kazi japo mazingira yalikuwa magumu lkn nilikomaa na nilimuomba mungu pia na baada ya mwezi nikafanikiwa kukabidhi kazi wakati wote wa kazi nilimwambia boss anitunzie hela Mpaka nitakapomaliza ndio anilipe nashukuru mungu nilifanikiwa kumaliza na nikalipwa halali yangu moja kwa moja nikaanza mikakati ya kununua kuku wa kienyeji kwa lengo la kuja kuuza dar kweli mungu alinipa wepesi nikanunua mzigo wa laki sita jpl ya week iliopita nikaanza safari ya kurudi dar na nikiwa na furaha tele kwani nyumba niliokuwa naishi hapo kimara korgwe ilikuwa kwenye order ya kuvunjwa hivyo nikawa na matumaini nikiuza tu natafuta chumba haraka lkn ndoto zilikatizwa na vibaka pale mikese morogoro kwani jamaa walidandia gari wakashusha mzigo kwenye bamsi wakasepa sio siri niliugua gafla kwa kweli hii dunia imejaa watu dhalimu wasiotumia nguvu zao kutafuta walaaniwe maisha yao yote wamefanya nimepungua kilo gafla hapa naomba mungu anipe wepesi
 
Pole sana, ila basi ulilopanda halikuwa na lock kwenye buti siku nyingne uwe makini na uchaguzi wa mabasi ya usalama ukiwa na mzigo kama huo.
 
Nimepoa ila tahadhari mnaosafiri hasa usiku Kama unatoka mkoani ukikaribia morogoro bora ukakaa nyuma kabisa kwenye mzigo japo hawa jamaa wanaweza hata kukuua lkn wakiona mtu kidogo wanaogopa pia kama kuna mtu ana kazi hasa kupaua blundering anistue ili nijikimu na huu mji wenye raha za bandia
 
Mkuu kwanza pole sana kwa majanga yaliyokukuta,mola akupe moyo wa subra Sana'a.


Pili naomba nidokeze kwa sasa kuku wanaenda kwa Bei gani,maana nahutaji kuingia katika hyo biashara na target area NI hapo singida
 
Back
Top Bottom