Jinsi ndoto yangu ilivyoanza kusuasua

kenkule

Member
Dec 1, 2017
37
28
Natumai mu wazima ndg wana JF!

Mimi ni kijana niliyezaliwa miaka ishirini na sita iliyopita (26). Ni kijana wa nne kwenye familia ya watoto tano, nilizaliwa moja ya mkoa unaopatikana kasikazini mashariki mwa ziwa Victoria . Nilianza shule ya msingi mwaka 2001 mkoan humo kwenye moja ya shule ya serikali baada ya kukaa mda mrefu nikiwa nachunga ng'ombe maake nmetokea kwenye familia ya mfugaji na mkulima vilevile. Kutokana na shughuli hizo basi ilinilazimu kuanza darasa la kwanza nikiwa na umri wa miaka 9.

Niliingia shulen hapo nikiwa mwenye furaha na bashasha kwani nilkuwa nawataman watoto wa rika langu walionitangulia kuanza chekechekea japo tulikutana nao darasa la kwanza kwan Mimi niliruka chekechekea na kuanza moja kwa moja darasa la kwanza.

Nilikuwa na hamasa kubwa sana ya kusoma ingawa kiumri bado nilkuwa mtoto, hamasa ya kupenda kusoma iliongezeka siku hadi siku, nikiwa na miezi michache tu toka nijiunge darasa la kwanza nilkuwa nishaweza kuhesabu na kuandika kwa ustadi kuzidi wanafunzi wenzangu darasa zima , nilkuwa mchangamfu sana kitendo kilichopelekea mwalimu wa darasa kunipenda sana hadi kufikia kuwa na urafiki na wazazi wangu.

Maendeleo yangu kishule yalistawi siku hadi siku na kila mwalimu alobahatika kupewa kipindi darasani kwetu hakuchelewa kunifahamu kutokana na uchangamfu wangu nilkuwa nao na uwezo mkubwa wa kunasa mambo ya darasani kwa haraka sana.

Uchangamfu wangu na hamasa ya kupenda shule ulinifanya nipendwe na walimu wangu sambamba na wanafunzi wenzangu shuleni apo, mitihani ya kujipima uwezo nilkuwa naonesha uwezo mkubwa sana kuanzia nikiwa darasa la kwanza kw ani toka nianze nilishawahi kushuka nafas moja tu na kuwa mtu wa pili nikiwa darasa la tatu, madarasa yote yaliyobakia niliongoza mihula yote!

Mwaka 2007 nilihitimu darasa la saba na kwenda mkoa mwingine wa jirani ambapo alikuwepo mzazi wangu(mama), aliondoka mwaka 2004 nikiwa darasa la nne (ni stori ndefu)

2007 mwezi wa kumi na mbili nilifika kwa mama kumsalimia mahala alipokuwa nikiwa na mdogo wangu w a mwisho yaan anayenifuata, alitupokea kwa furaha sana maana ni miaka takribani mitatu ulikuwa ishapita bila kuonana Naye, tulikula,tukanywa na kushiba huku tukifurahi na mama yetu. Tuliendelea kukaa apo kwa siku kadhaa huku mama akiendelea kujishughulisha na biashara yake ya kuuza dagaa, week chache baada ya kufika pale mama alinitafutia tuition yaani pre-form one kwan alijua nitafaulu kwenda kidato cha kwanza kutokana na uwezo nilkuwa nao.

Matokeo ya kujiunga na kidato cha kwanza yalitoka na hatimae kati ya wanafunzi kumi na tano waliofaulu nilikuemo na nikiwa na alama nzr zaid kuliko wenzangu, basi tukaendelea kusubiri mda wa kujiunga ufike huku mama akiendelea na shughuli zake nami nikiendelea na tuition, mda ukawadia na usajili ukawa umeshaanza , mama nakuwa na hali nzr kiuchumi ya kuweza kuninunulia baadhi ya vitu ili nikajiunge na kidato cha kwanza ,ilibidi tuanze kufanya mawasiliano na mzee wangu kupitia simu ya mjomba maana mda ule wenye simu walikuwa wachache , nikaongea na mzee kwenye simu kumuelezea kinachoendelea ili aweze kunishika mkono lkn hakuonesha umoja kwani alinijibu kwa ukali kwamba hayamhusu.

Mama aliendelea kupambana huku na kule kwa ndg na jamaa hadi akafanikiwa kupata mahitaji mhimu yanayohitajika na ada japo kidogo.

Baada ya hapo tukaanza safari ya kurudi nyumban Mimi na mdogo wangu hiyo 2018 miez ya mwnzon kwan na yeye alikuwa ndo anaingia darasa la sita, tulifika nyumbani na baba aligomba sana ilifikia hatua akataka kutufukuza lakini bibi akaingilia kati hatimaye yakaisha.Nikaanza shule japo kwa kuchelwa kwan lakini nilijitahidi kufatilia waliosoma wenzangu na vile nilivosoma tuition hatimae tukawa sambamba nao, mda wa kufanya mitihan uliwadia tukafanya nikawa kwenye top ten , mwaka uliofata tukaingia form two na mtihani wa kwanz nikawa wa pili kiukweli nilifurahi sana maana nilihisi narudi kwenye enzi za shule ya msing na matokeo yalinipa hamasa ya kuendelea kusoma kwa bidii.Kipindi hiki tayari nilkuwa nimehama nyumbani na kwenda kuishi kwa binamu yangu kutokana na umbali wa shule pamoja na huduma hafifu niliyokuwa naipata nyumbani ,mdogo wangu naye alikaa kwa mjomba wangu kumalizia darasa la saba.

Jambo la kushukuru mungu ni kwamba matokeo yangu yaliendea kuwa mazuri kwani mtihani wa mock wa kidato cha pili nilifaulu kwa wasatani wa B nikiwa mtu wa pili darasani , na mtihani wa taifa nikapata B nikiwa wa pili , Tukafunga shule form two kusubiria matokeo baada ya kumaliza mtihani November , nikaa kwa binamu yangu huku nikimsaidia shughuli za hapa na pale kama kulima nk mpkaa shule ilipofunguliwa January 2009 nikaanza kwenda japo matokeo yetu yalikuwa bado hayajatoka ila tuliendelea kusoma huku tukisubiri ,baadae yakatoka na wastan wa B yakanipa ruhusa ya kuingia kidato cha nne!

Niliendelea kusoma kwa bidii kama mwanzo usiku na mchana. Mdogo wangu alihitimu darasa la saba 2009 September na kurudi kwa mama mwanza , Apa nilisahau kitu ,ipo hivi ndg zangu watatu yaan ukinitoa Mimi na mdogo wangu walimaliza la saba na wawili kati ya hao ni wa kike mda huo walikuwa washaolewa wapi kwa waume zao ,mmoja aliyebaki ni kaka yangu mkubwa ambaye aliekea mwanza 2003 Mara baada ya kumaliza la saba na kwenda kuvua samaki akiwa kama mvuvi kibarua.

Tuendelee, mdogo wangu kamaliza la saba yupo kwa mama ,kaka yupo visiwan na dada wapo kwa waume zao ,Mimi Niko kw binamu nimeingia kidato cha tatu 2009 , siku moja nikiwa nimelala nilisikia mwili kupooza na kukosa nguvu kabisaa huku kifua kikibana mithili ya mtu mwenye TB , ilinikamata homa kali usiku huo nikakohoa huku nikijisikia uchungu kwenye koromeo na kuhisi ubongo unatoka , niliendelea kukohoa kwa mfulilizo week kama tatu hivi huku nikiwa sina nguvu za kwenda darasani kwan niliugulia ndan binamu alinipeleka hospital nikachomwa sindano na kupewa dawa za kutumia nyumbani ,nikarudi nyumbani huku nikiwa na doz , nikaanza kutumia doz na mda ulivozidi kwenda nikajisikia ahueni kwenye upande wa kukohoa japo kichwa kiliendelea kuuma kwa sana.


Baada ya homa kukata nikaanza kwenda shule lkn kichwa kilikuwa kinauma na wakati mwingine naskia kama kuna mdudu anapita ndani kwa ndani, kuwasha had natamani nipitishe mkono sjui wapi nijikune kwa ndani humo maake muwasho nilkuwa nausikia kwa Ndan ya ubo go na siyo nje.

Baasi kikaendlea hivo na me nikaendelea kwenda darasani kwa maumivu makali maana shule nilkuwa naipenda na pili nilitamani kusoma kwa hali yoyote ile nije nisaidie familia yangu, kadri siku zikivizid kwendq maumivu yalizid ikabidi nimtafute mama nimtaarifu ili anipe msaada , akaniambia nimtafute mjomba anipeleke hospitali ya wilaya ,siku moja ya jumamosi nikaenda kwa mjomba ambaye aliishi kijij cha jirani nikamueleza tatizo akaniambia nilale kwake kesho yake anipeleke hospital,nikalala kesho yake tukaenda nikafanyiwa vipimo wakanipa dawa tukarudi nikaenda kwendlea na shule, maumivu bado hayakuwahi kupungua hata Mara baada ya kupewa vidonge.

Nilkaa pale shule huku hali ikiendlea kuwa tete kwani ilifika mda macho yakawa hayaoni vizuri naona kama kuna giza ama ukungu ukungu mbele yangu hats nakumbuka kuna siku mwalimu wa geographia alikuja kufundisha nikawa simuoni lkn namsikia anacho kiongea , kuinama kuandika ilikuwa ni taabu maake nilihic ubongo unatoka kila nikijaribu kuinama.

Siku chache nikampigia mama kwa Mara ya pili kumpa taarifa ya kwamba mambo bado yanazidi kuw a mabaya kwangu maana hata kuona sion vizuri, akaniambia ikifika siku ya jumamos niende kwa mjomba wangu (huyu ni mwingine tofaut na yule wa kwNza) ,basi lipofika siku nikaenda nikamuelezea akanipa dawa moja ya kienyeji nikawa navuta kama mtu anavyovuta ugolo baadae nikatulia kwa mda ndo akaja akniukiza unajisikiaje nikamwambia bado nasikia kinagonga.akasema okey nitakutafutia nyingine.


Nikarudi jioni shule kwani kuna kazi tulikuwa tumepewa na mwalimu wa hesabu ilibidi nirudi kufanya


Mwezi wa nne ukiwa umekaribia shule ikapokea taarifa kutoka kwa afisa wa afya kwamba choo kimejaa hivo hatutaweza kuendlea kukaa maeneo yale hadi shule ipate choo kingine ndo iliamuriwa shule kufungwa , baada ya kumaliza mambo ya ufungaji wa shule nilichukuwa begi langu la nguo nikaaga binamu nikaanza safar ya kwenda kwa shangazi amabye alkuwa anaishi mjini , nilifika kwake jioni nikalala ,kesho yake nikamuomba simu nikafanya mawasiliano na mama na kumwamibia hali halisi ya maendeleo ya afya yangu , akaniahidi kunitumia nauli ili niende alipokuwa, akawa amenjtumia nauli kesho yake nikapanda bus huku na begi la shule na nguo chache kuelekea mwanza , nilifika akaniangalia akatokwa na chozi kwani nilkuwa nimekonda sana.

Basi nikamueleza nilivoanza kuugua ,siku ya kwanz akanipeleka sekoutoure moja ya hospitali ya mkoa wa mwanza nikafanyiwa vipimo majibu yakatoka wakanipa dawa na miwani ya kuvaa kutokana na tatizo langu la macho na kichwa ,tualrudi nyumban ,nikaanza kutumia dawa huku akinitafutia shule ya kusoma wakati naendele na matibabu.


Alitokea mchungaji mmoja kwa jina anitwa Amon wa T.A.G akaja nyumban pale kwa mama kwan mama alikuwa nasali kanisan kwake , mama akaanza muelezea tatizo langu akaanza kuniombea na kuniambia kila siku jioni niwe naenda kwake anionbee pia alimuahidi mama kunitafutia shule ya kujishikiza kwa wakati ule , nikawa nahudhuria maombi kila siku jioni na mchungaji akapata shule moja ambayo alikuwa anafundisha masomo ya dini kila jumatano mchana yaan vile vilind vya dini(casfeta,TYCS nk) nadhani wengi wenu mnavikumbuka,alipofanikiwa kupata akarudi nyumban kumwambia mama akaninunulia nguo na daftar kwan kule sikuondoka na nguo za shule wala daftaar.


Nikaanza shule huku tatizo la kichwa likiwa pale pale na time hii kusoma mpaka nifunge kitambaa kichwsni ndo noweze kusoma, niliendelea hivo hivo ,kusali ,kutumia dawa na kusoma kuanzia mwishoni mwa April kufikia may tukaanza kujiandaa na terminal exams ,apa niliwaza sana maana nilkuwa nyuma sana lkn mungu si athumani nilipata kuwa na wastani wa B na kushika nafasi ya nne.Apa mkuu alitokea kuanza kuwa karibu na Mimi kwani mkuu alikuwa na upendo wa hali ya juu kwa wanafunzi hususan wale wanaonesha nia , tukafunga shule mwez wa sita mama akanipeleka bugando kupigwa x-ray , tulipofika tukakuta watu ni wengi afu taratibu ni ndefu mapaka uje upate huduma ,ndo akatokea mtu mmoja kuja kuniona waliokuw wanafahamina na mama akamuuliz kuhusu tatizo langu nikajieleza ndo akamshauri mama ajaribu kuangalia na kwa waganga wa kienyeji, ikafika jion tukarud nyumban ,asbh yake mama akaniambia nijiandae kuna mahala atanipeleka.



Kiufupi,alinipeleka kwa mganga wa kienyeji huko kisiwani ukrewe nikatibiwa likizo yote ya mwenzi wa sita bila kupata ahueni yyte nikarudi tena shulen baada ya kufungua nikaendelea kusoma hivo, kiukweli mda huu kichwa kiliniuma sana adi nilitamani kujinyonga tu maana sikuoni raha ya kuishi tena!


Nikasoma huku kila nikipata hata likizo ya week ama mpumziko ninaenda kupata dawa hospitalini na kubadili waganga mbalimbali ,nikienda kigoma hola,rukwa hola,musoma hola nikarudi tena bugando hola , apa nikaanza sasa kuizoe ile hali kwamba ndo kilema changu , nilirudi shule safar hii tunaingia form four ,mkuu akajitolea kunifuatilia uhamisho maana alinipenda sana kutokana na nidhamu na utulivu niliokuwa nao pale shule pia alinionea huruma sana jinsi nmeteseka, basi nikarudi kuendelea na masomo na mkuu akafanikisha uhamisho aketa nikasajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha nne pale shulen kwake ,mda ukafika nikafanya mtihani matokeo yakatoka tukawa tumefulu wanafhnzi wanne kwenda advance.

2012 nikachaguliwa kujiunga na kidato cha tano mkoani kagera ,nikaenda nikasoma huku kichwa kikiendelea kuuma vilevile lkn kufhnga kitambaa ndo kitu kilichokuwa kinaniwezesha kuhimili na kuanza kusoma kwan bila hivo nisingeliweza PCM

Mungu wetu ni mkuu nikamaliza 2014 nikachagukisa JKT mlale kwa miezi mitatu apa kuna siku niliugua usiku kidogo nife ila kutokana na uakribu wa askari wa pale kikosini nilipata hiduma mapema, niliruhusiwa kufanya kazi za kawaida dogidogo kama usafi na kuchota majin kulingana na tatizo langu nilikokuwa nalo.


Matokeo yakatoka nikawa nimefauli kuingia chuo kikuuu , tukamaliza mafunzo tukafanya na applications za chuo nikachaguliwa kujiunga na moja ya vyuo vikuu apa nchin kwa course ya electrical engineering ,nikaanza 2014 mwaka wa kwanza tatizo likawa limeanza kuzid kwani kuna mda nilkuwa nasikisia kizunguzungu hadi inanibidi nikae chini kwa mda ndo niendelee na safar yangu,nikakomaa hivo hivo hadi nikamailiza mwaka wa nne 2018 , yaan mwaka huu na nmefanikiwa kugraduate japo kwa ufauku wa kawaida ,nipo nyumban bado tatizo liko pale pale naogopa kuaply kazi maake kusema ukweli ufanisi wangu utakuwa ni mdogo kazini kwani kichwa kinauma usiku na mchana na tukizingatia ya kwamba kazi inahitaji utulivu wa hali ya juu, Mimi nachoomba mwenyezi mungu na ndg zangu ni uzima na kupona kurudi katika hali ya kawaida nimeteseka kwa mda mrefu sana


Ahsante sana
 
Mkuu pole sana, jana nilikutana na dogo mmoja hapa mitaa flani mbeya, alikuja ofisini akaniomba simu awasiliane na mama yake huko musoma, baada ya kuwasiliana nae akaanza kunieleza tatizo kama lako hivyo hivyo japo yeye hajasoma na hivyo amajikuta akishindwa kuendelea na kazi zake alizokuwa anafanya. Sikuwa na nafasi ya kuongea nae sana kutikana na kazi niliyokuwa nafanya, na leo sijamuona kutokea. Kwa ushauri wangu ni kuwa hilo tatizo liangalie kwa macho manne kutokana na sababu uliyosema pale juu kuwa ulipotoka kwa mama baba alikugombeza sana.

Pole sana
 
nakushauri mpigie huyu kaka hapa nakupa namba yake,,ni nabii wa kiroho Mtumishi wa Mungu..Ana maono ya ndani na namfahamu sana namba yake 0713344025 nina imani utapona,,ana maombezi mazito na yenye mnufaa
 
Pole Sana mkuu je umejaribu kwenda tena hospital? Ushauri wangu ungefanya kipimo cha MRI, ungeweza kujua tatizo nini nakujua ,nakuombea upone
Nitajaribu japo kwa sasa kiuchumi hatuko vzr ,chuo nilipewa mkopo kwa asilimia karibu zote! Ila nitajitahidi kufanya kazi yyte nitakayoweza nikipata hela niende tena nikafanye vipimo!
 
stori inasikitisha adi inafika stage tunashindwa kutoa ushauri tunaishia kusema pole

any way usimuache mungu hata kama unakutana na majaribu gani kwa imani yote yanawezekana muhimu imani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom