Jinsi tunavyoibiwa petrol station

[emoji15] mwisho wa siku ulirejeshewa kiasi cha petrol ulichoibiwa?
 
Total & Victoria basi wengine usiende
 
Asee mi wamenifilisi basi..
Mwaka wa tano huu ila kuanzia Leo ni dumu kwa kwenda mbele...

Hivi sheli wanakubali ushushe dumu ukiwa na gari hapo hapo?
Kama gari lako la petrol wadanganye ni la diesel, ila ww unahitaji petrol kuna gari la mshikaji nampelekea ngwese ndinga lake limebuma rodini.
 
Mimi gauge yangu Ya mafuta Ni digital, Unayosema Ni kweli kabisa,nimeshawekewa litre 8.6 muhudumu anakomaa kaweka litre 10, nikamwambia Kabla hajaanza kuweka mafuta nilikua na reserve Ya litre 10.2 kwahiyo baadaya Ya Kuongeza mafuta yake ilitakiwa gauge isome 20.2, nikaanza kumpa vitasa vya nguvu,shabashi wanatuibia sana hawa kima.
 
na ukikuta sheli yenye petrol iliyochakachuliwa pamoja na kidumu chako kujaa vizuri lazima gauge ishuke mda mfupi baada ya kutumia, wenye kujua mafuta mazuri pia mtuelekeze pa kuyapata
 

Kuelekea sinza ukitokea Shekilango kuna kituo cha Mafuta GBP, Ni muda umepita lakini nilipatwa na mkasa kama unavyoelezea hapa Ndugu, Nilikuwa na Gari Land cruiser VX V8 inatumia Diesel ,Jipya, na nilikuwa natokea Toyota Motors ambako baada ya taratibu zote nilikabidhiwa Gari langu na Nyaraka zikionyesha pia Mafuta yaliongezwa lita50. Na vipimo vya gari vilionyesha mafuta yapo chini ya Nusu tanki,Kwa kuwa nilikuwa nasafiri mchana huo nilipitia nyumbani nikachukua
Nguo chache na mkoba wa safari kwa ajili kazi, Napendelea kutumia mafuta ya BP tangu zamani hivyo nikaona nikiingia pale sinza itakuwa pia ni rahisi kutoka ingawa hakukuwa na foleni sana, Wakati naingia nilipokelewa kwa Bashasha sana na Dada wawili wakiwa na mlinzi mwenye silaha na nikaelekezwa pa kusimama , kwa kuwa mfuniko unafungulia ndani tayari Mhudumu alishaishika pipe ya kuweka mafuta na kuomba nifungue mfuniko..! Pembeni mlinzi nae kaniijia na kuanza kusemesha huku kasogelea mlango kwa karibu sana, kwa kuwa kioo kilikuwa wazi upande wangu na tena nilikuwa na fedha nyingi kidogo ikaniwia vigumu kuteremka kwa hofu ya yule mlinzi maana aliona wakati natenga zile fedha za kununulia mafuta, ghafla Muhudumu akaniuliza niweke lita ngapi? Nikamjibu Jaza kabisa Kichekesho cha Mwaka nikashangaa zimeingia Lita 142.7.. kama kwamba Gari lilikuwa halina mafuta kabisa , Ghafla mlinzi akatoka eneo lile na nikaletewa Risiti ya Madai, Kwa kuwa Nilitambua kuwa umefanyika mchezo mchafu kwa upole nilimwambia yule Muhudumu kilichotokea ingawa alihamaki kidogo lakini Body language yake haikuendana na sentesi zake, Na yule mlinzi alitegemea ubishi maana nilifikiria vitu vingi, Pampu inasoma 142.7 Litres, Ninapokwenda ni muhimu na nikipoteza muda najichelewesha,Nitabisha nini sasa, Nikafikiria hasara zinapata Watu wangapi? Nikamwambia yule Binti Naondoka lakini usitegemee nitarudi kujaza mafuta hapa tena na Rafiki zangu nikawaaambia, Yule Binti hakuwa mchangamfu tena kama mwanzo, Hivyo Niliingizwa mjini kwa kuiamini BRAND kumbe ovyo tu labda wabadilike.
TUWENI MAKINI UNAPOHITAJI KUONGEZA MAFUTA HAKIKISHA PAMPU INAANZA KUSOMA UPYA.
 
Kama gari lako la petrol wadanganye ni la diesel, ila ww unahitaji petrol kuna gari la mshikaji nampelekea ngwese ndinga lake limebuma rodini.
Mrejesho nimeenda na dumu mbili za Lita ishirini pale GBP ya mapambano kila Lita 20 nimeuziwa 370000, maajabu sasa nimeenda kujaza kwenye Gari nimestaajabu sana, kiufupi hawa watu ni wanatupiga

Note: kwenye dumu hujaziwi kwa kutumia mpira unakuta umeshaandaliwa yamefichwa chemba, so mnabadilishana madumu
 
na ukikuta sheli yenye petrol iliyochakachuliwa pamoja na kidumu chako kujaa vizuri lazima gauge ishuke mda mfupi baada ya kutumia, wenye kujua mafuta mazuri pia mtuelekeze pa kuyapata
Mi nimeelekezwa TOTAL pale Mlimani City... nimeanza kujaza pale, baada ya mwezi ntajua tuu
 
Thread 'Kasi ya ujenzi ya vituo vya kujazia mafuta ya magari inaendana na ubora, usafi na usalama wa mafuta yenyewe?' Kasi ya ujenzi ya vituo vya kujazia mafuta ya magari inaendana na ubora, usafi na usalama wa mafuta yenyewe?
 
Ongeza bidii kwenye kutafuta hela uache kuchunguza pamp
 
Ilinikuta hiyo picha ya ndege kibaha sita sahau halafu ilikuwa usiku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…