Jinsi tunavyoendelea kuliwa kupitia BoT!

FP, IPTL is being liquidated lakini kinachoniacha gizani mimi ni hayo mengine kuhusiana na hiyo akaunti na huo mkwanja

Mpita njia,

Nilivyoelewa mimi,hiyo Escow Acounti ilifunguliwa BOT ikiwa chini ya udhibiti wa RITA (Kama Liquidator).

Huo mkwanja 138bil ni madeni ambayo IPTL inawadai wateja wake...hopeful tanesco....lakini kati ya hayo medeni, kuna mengine yana mgogoro na mengine hayana mgogoro.....yale yenye mgogoro malipo yake yanatakiwa kulipiwa kupitia Escrow account wakati yale ambayo ni clean yanalipwa kwenye account ya IPTL!

Mimi maswali yangu on this ni kama kny post yangu hapo juu tu!
 
Mkuu, mdeni mkubwa wa IPTL ni tanesco (sidhani kama kuna mdeni mwingine). Mihela hiyo ni jumuiko la malipo ya capacity cahrges ambazo serikali iligoma kulipa baada ya kugudua ujanja wa IPTL. Kimkataba nadhani serikali ilitakiwa kuweka fedha hizo katika hiyo account wakati wa mgogoro. Sasa hapa ndipo nataka kufahamu modalities za liquidator kudhibiti hiyo account wakati kimsingi mgogoro haujamalizika. na sijui kama kweli serikali ilishaweka fedha hizo kwenye account baada ya kugoma kuwalipa IPTL.

Hii account imefunguliwa kutokana na matakwa ya mkataba. Kwa nini liquidator asifanye reference ya mkataba kuhusiana na management ya account na anakwenda mkoja kwa moja kwenye sheria? na sheria yenyewe anatumia kifungu controversial
 
Wakuu,
Na huu ndiyo wakati mwanana wa kujua ECONOMIC RESCUE PACKAGE yetu ambayo nayo imetangazwa hivi karibuni itaelekezwa wapi.

Kama kuna wakati wazalendo tunatakiwa kuwa macho ni sasa - kosa si kosa ila kurudia kosa. Mwizi ni kama aliyeonja damu ya mtu haachi - wazalendo tumenyonywa damu miaka nenda rudi na lazima wakati ufike tuseme sasa basi na wakati huo ni sasa.

Nawaomba watanzania wote wenye uchungu wa kweli na hili taifa letu popote walipo na kwa nafasi zao mbalimbali tuungane pamoja katika hivi vita. Sasa iwe mwiko kukaa kimya ukiona vitu kama hiki alichotuletea Invisible (asante wewe usiyeonekana ingawa macho unayo). Tuchungulie na tuchunguze hadi uvunguni mwa vitanda tujue kulikoni halafu tupeane habari. Hakuna cha nyaraka za siri ya serikali kama lengo ni kutuibia, tusiwaonee haya hiki kigenge cha wezi.

CCM ni Chuo Cha Mafisadi.
 
Kwa mtaji huu tunaitaji kila mpiganaji lazivyo nchi itakuwa mufilisi. Tunawaitaji wapiganaji wa JF, manabii wa uongo(mladi watu wanalipuliwa) na kila mlipa kodi wa nchi hii
 
... Sasa hapa ndipo nataka kufahamu modalities za liquidator kudhibiti hiyo account wakati kimsingi mgogoro haujamalizika.
na sijui kama kweli serikali ilishaweka fedha hizo kwenye account baada ya kugoma kuwalipa IPTL.

Hii account imefunguliwa kutokana na matakwa ya mkataba. Kwa nini liquidator asifanye reference ya mkataba kuhusiana na management ya account na anakwenda mkoja kwa moja kwenye sheria? na sheria yenyewe anatumia kifungu controversial

Mkuu Mpita Njia,

Mgogoro uliosababisha liquidator kuteuliwa hauhusiani kabisa na mkataba kati ya IPTL na TANESCO, isipokuwa ni mgogoro unaofukuta kati ya makampuni mawili yaliyounda IPTL. Lile kubwa, Mechmar Corporation (70%) lilipatikana mahakamani kwamba limefanya ufisadi dhidi ya dogo, VIP Enginering (30%), kwa hivyo wanadaiana. Jaji Katherine Oriyo akaamua kuteua receiver, akisema kampuni hii, IPTL, wengi sana hawajamalizana nayo, ikiwemo TANESCO, kwa hiyo in the public interest ngoja ishikiliwe na third party.

Hiyo escrow akaunti pia inajumuisha guarantee ambayo serikali iliipa IPTL kwa niaba ya TANESCO (liquidity facility) kwa mujibu wa mkataba wa 1995. Kuhusu uamuzi huo wa kuteua receiver, soma zaidi hapa
 
Hee makubwa haya....
Ama kweli Ubepari unakuja na mengi...duh, tutafika kweli?..
 
Lakini Invisible, mbona hii barua haina logo wala muhuri, au ni macho yangu tu? Lol kama ni kweli, basi kumwaga damu ni sawa tu.
 
Jamani.. kinacholiwa ni nini.. Hapa wanagawana hela ambazo mkataba ulisha wagurantee.. so the headline is slightly off. Receivership means the money taken will be used to pay off creditors and the rest divided amongst the share holders.. ie Rwegamarila na wale waindonesia wake (30-70 Respectfully).. they had a falling out and the matter went for arbitration and to court in TZ and the liquidation was ordered by the court due to irreconciliable differences..

BOT hailiwi kina mama ndossi na chenge walisha hakikisha contractual obligation and at the time the govt spilt its ink on the contract.. that money was gone.. NOW its just Delivery.. nothing NEW.

K out
 
Samahani mkuu, ina maana IPTL ndo inaishia? Je aliyeandika si ndo yule mmbongo wao? Mbona barua imekaaa kidesign?

Jamani,

Mimi nadhani huu ndio ushindi mkubwa. IPTL kufilisika maana yake ni vyema kwetu.

Mfilisi wowote lazima atafute mali za hiyo kampuni popote zilipo maana ndio kufungasha virago hivyo ati.

Hata ngeleja amesema issue ya IPTL iko mbioni kuishia.
 
Mkuu hakuna anayepinga wala kuchukizwa na kufilisika kwa IPTL, macho yetu ni hizo 138billion. Hizo si fedha kidogo mkuu, ni nyingi kuliko zilizoibiwa EPA.
 
Mkuu hakuna anayepinga wala kuchukizwa na kufilisika kwa IPTL, macho yetu ni hizo 138billion. Hizo si fedha kidogo mkuu, ni nyingi kuliko zilizoibiwa EPA.

Sasa rafiki yangu wewe ukichaguliwa kuwa mfilisi, utaanza na nini, accounts zote za kampuni husika na asset zake au sio? Au wewe utaanza na kufuatiliwa wadeni wa kampuni husika?

Sasa hizo hela lazima kimahesabu ni za IPTL otherwise Mfilisi asingekurupuka na kusema hivyo.

Alafu kumbuka mara nyingi mfilisi anakuwa mtu aliyekubaliwa na wadau wakubwa wa hiyo kampuni.

This is typical normal procedures za ku-close down business... cha ajabu nini? hela nyingi? sasa unadhani IPTL isikuwa inafanya biashara ya kuuza ukwaju?
 
Based on the scale of business hela wala sio nyingi.. watu wanafikiria in personal terms.. BOT inaliwa vipi sasa.. hizi hela ni mali ya IPTL walionayo kihalali kutokana na mikataba mibovu yakina Mary Ndossi na Chenge.. That is how they became billionaires.. Nothing new here...
 
...good point,watu wanasahau wanaotia hasara Taifa ni hao walio madarakani walafi wa 10% & wasiojua kitu,ukiangalia vizuri hao IPTL hawajavunja sheria yeyote zaidi ya kutumia incompetence ya viongozi wetu,hakuna haja ya kulaumu IPTL dawa ni kuwashughulika hao waliotuingiza kwenye hiyo mikataba!
 
Mwaka huu tutaona mengi, ... Kumbuka tunaelekea 2010 na zinatafutwa pesa mapema.

Hawa jamaa wa sasa hivi ni smart kidogo kulinganisha na watangulizi wao, mwaka 2005 jamaa walichelewa ku-fundraise na pesa ikatoka mwishoni sana na kusbabisha Sumaye & Co. kushindwa kukampeni sawasawa.
 
unauhakika gani kuwa ni 'incompetence' na siyo rushwa? Kama IPTL walitoa rushwa ili waingie mkataba unaoifilisi nchi kwanini wasipigiwe kelele? Hii si sawa na issue ya rada?
 
Sasa rafiki yangu wewe ukichaguliwa kuwa mfilisi, utaanza na nini, accounts zote za kampuni husika na asset zake au sio? Au wewe utaanza na kufuatiliwa wadeni wa kampuni husika?

Sasa hizo hela lazima kimahesabu ni za IPTL otherwise Mfilisi asingekurupuka na kusema hivyo.

Alafu kumbuka mara nyingi mfilisi anakuwa mtu aliyekubaliwa na wadau wakubwa wa hiyo kampuni.

This is typical normal procedures za ku-close down business... cha ajabu nini? hela nyingi? sasa unadhani IPTL isikuwa inafanya biashara ya kuuza ukwaju?

biashara ya ukwaju? lol, well, turidhike, tusihoji, tusitafute ufafanuzi wa sh. 138 billion kwa sababu IPTL walikuwa wanafanya biashara isiyo ya ukwaju! Mkuu soma thread ya IPTL ujue Serikali ilikuwa inalipa kiasi gani kwa mwaka na sasa inatakiwa kulipa 138bil. Kama ni biashara tu basi hata jamaa wa rada waachwe bila kuhojiwa.
 
Mwaka huu tutaona mengi, ... Kumbuka tunaelekea 2010 na zinatafutwa pesa mapema.

Hawa jamaa wa sasa hivi ni smart kidogo kulinganisha na watangulizi wao, mwaka 2005 jamaa walichelewa ku-fundraise na pesa ikatoka mwishoni sana na kusbabisha Sumaye & Co. kushindwa kukampeni sawasawa.

Nakubaliana na wewe huenda ni fund raising ya uchaguzi 2010.
 
Mikataba mibovu si matokeo ya incompetency ya viongozi wetu. Hata kidogo. Ni matokeo ya tabia ya wizi ya baadhi ya waliopewa dhamana. Ni ujambazi hakuna lingine. Ni wizi unaoachwa kufanyika kwa sababu ya kukosekana kwa mtu wa kusimamia utekelezaji wa maadili ya kazi. Ni tabia inayoachwa kuendelea na viongozi wetu wa juu kabisa wa nchi, rais akiwemo. Haiingii akilini kwa mfano mikataba nyeti ikazuiwa isijadiliwe bungeni hata kupitia kamati tu.

Viongozi wetu wa juu ndio sababu ya mikataba mibovu. Wameshindwa kuisimamia na kuwawajibisha wanaoisababisha. Mikata mibovu ni wizi wa wazi wa viongozi wetu na si kingine.
 
Back
Top Bottom