Hakuna ubishi kwamba sisi wapenzi wa siasa za Amani, umoja, haki na maendeleo ya watu siasa za Tanzania ktk kipindi kilichotajwa hapo juu zilitutia unyonge sana.
Zilitutia unyonge kwa sababu hatukua na mtetezi yeyote wa kututia moyo. Tumaini pekee lilibaki kwa Mungu.
Matajiri na maskini wote hali zao zilikuwa mbaya kila mtu kwa nafasi yake ilifika kipindi hata wazawa wa ndani ya chama pendwa chama tawala na wao walionja joto la jiwe.
Tuyaache hayo. Nini kilifata sasa baada ya hali ngumu?
Basi bwana ikawa tunajifariji tu kwa nyimbo za injili na maneno matukufu ya watumishi wa Mungu. Kama ni kipindi tumeomba na kusali sana basi ni kipindi hiki.
Nitataja watumishi wa Mungu wasio na Mawaaa ambao mimi binafsi kupitia wao nilifarijika na kuimarika kiroho na baadae kimwili.
1. Askofu Aurelian Ngonyani huyu ni askofu wa Kanisa la Truth Bible Fellowship.
Ni mtumishi ambaye kwa kiasi kikubwa anajikita kueleza na kufafanua siasa za Nchi ya Israel na tawala zake, changamoto na mafanikio. Huyu mtumishi alinifurahisha kwa vile anavyodadavua Nchi ya Israel kwa mikoa, majimbo hadi mitaa. Amefanya ziara na tour nyingi nchini humo na kuiva ktk historia yake.
Unaweza kumpata Ktk Youtube channel yake kwa jina hilo hilo.
2. Mwinjilist Godfrey Machota.
Huyu ni kijana mdogo Graduate wa Civil engineering 2016.
Kaka huyu amejikita katika masomo ya unabii na ufunuo.
Huzungumzia kwa kina kuhusu siasa, tawala na falme za dunia zilizopita za kuthibitisha Ufalme wa Mungu wa nyakati zijazo.
Ukimsikiliza kwa makini utafarijika sana hata kwa magumu ambayo Watanzania wanyonge wanapitia kutokana na uongozi mbovu.
Naye anapatikana Youtube channel kwa jina hilo hilo.
3. Maalim Othman Suleiman Mazinge.
Heshima kwako Ustadhi na Amir. Huyu mwamba ni mfano bora kabisa ktk utumishi wa kueneza Daawah kwa waja na ummat Muhammad.
Kupitia yeye nimefarijika sana kipindi ambacho uchumi ulikuwa mgumu lakini watz wakapigwa stop wasilalamike eti vyuma vimekaza.
Anatumia Mfano wa Mwanadamu aliye Mbora ktk wote Mtume Muhammad (s.a.w). Pia ana uzoefu na siasa za Tz na maisha yake ingawa yeye si mwanasiasa kabisa.
4. Dr Sule. Huyu anaonekana sana kwenye Daawah Tv Mtoro. Ni mwalimu mzuri ktk kutoa Elimu ya Dini, siasa na maisha ya watumishi wa Mungu wa kale.
5. Paul Semba
Jamaa huyu akiwa ktk Mkoa wa Arusha( kama sikosei) Njiro Hill huko anafundisha kwa kina masomo ya Utawala hasa ajirejea falme za Kale za Babeli, Uyunani, Umedi na Uajemi na Dola ya Rumi.