Wachambuzi wa Majuma 70 aliyopewa Daniel mchungaji Mastai na Askofu Ngonyani hawajatuambia Yesu alizaliwa mwaka gani. Krismas ni nini?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,137
Nimekuwa nikifuatilia kwa makini Mafundisho ya mchungaji Matsahi wa KKKT Kimara na Askofu Ngonyani wa WAPO kuhusiana na Majuma 70 aliyopewa Daniel kwenye Daniel 9:22-27 na Kipindi cha Dhiki kuu.
.
Wote Wawili wanasema kuna Majuma 7 ya kujenga Yerusalemu mpya.

Wote Wawili wanasema kuna Majuma 62 ya kujenga mahandaki na Miundombinu na Ikifika Juma la 62 Masihi atakatiliwa mbali (atauawa)

Wote Wawili wanasema Masihi wa Mungu Yesu Kristo aliuawa kwenye Juma la 62.

Wanapotofautiana

Mchungaji Matsahi amesema Yesu alizaliwa mwaka 1 na akapiga hesabu zake

Askofu Ngonyani anasema Yesu alizaliwa miaka 5 kabla ya kalenda ya kirumi iliyoanzia na mwaka 1 na Kuanza kujumlisha kutumika

Ikumbukwe kalenda ya kiyunani ilikuwa inahesabu miaka kwa kushuka (-) na hii ya kirumi ya sasa inajumlisha (+)

Swali:

Kama haijulikani tarehe sahihi aliyozaliwa Yesu, sherehe za Krismas zilianzaje?

Bwana Yesu Asifiwe

Jumaa Mubarak

😄
 
Back
Top Bottom