Kwa mujibu wa Biblia Mungu hakutaka watu wawe Wanasiasa au wawe viongozi wa Serikali au waajiriwa serikalini au kuwepo Kodi au mali za umma

Shotocan

JF-Expert Member
Nov 21, 2023
2,202
4,614
Kwa mujibu wa Biblia Mungu hakutaka watu wawe Wanasiasa au wawe viongozi wa Serikali au waajiriwa serikalini au kuwepo Kodi au mali za umma

Mwanzo Mungu ndie alikuwa mtawala wa watu Israel ndio waanzilishi wa mifumo hii ya Serikali iliyoko Sasa baada ya kumuasi Mungu

Hii mifumo ya Sasa ilianzia kwenye Biblia kitabu Cha 1 Samweli 8: 4 -22 nasoma

4 Ndipo wazee wote wa Israeli wakakutana pamoja, wakamwendea Samweli huko Rama;

5 wakamwambia, Angalia, wewe umekuwa mzee, na wanao hawaendi katika njia zako; basi, tufanyie mfalme atuamue, mfano wa mataifa yote.

6 Lakini neno hilo likawa baya machoni pa Samweli, waliposema, Tupe mfalme atuamue. Naye Samweli akamwomba Bwana.

7 Bwana akamwambia Samweli, Isikilize sauti ya watu hawa katika kila neno watakalokuambia; kwa maana hawakukukataa wewe, bali wamenikataa mimi, ili nisiwe mfalme juu yao.

8 Kwa kadiri ya matendo yote waliyonitenda tokea siku ile nilipowatoa katika Misri hata leo, kwa kuniacha mimi, na kwa kutumikia miungu mingine, ndivyo wanavyokutenda wewe.

9 Basi sasa, isikilize sauti yao; walakini, uwaonye sana, na kuwaonyesha desturi ya mfalme atakayewamiliki.

10 Naye Samweli akawaambia wale watu waliotaka mfalme maneno yote ya Bwana.

11 Akasema, Mfalme atakayewamiliki ninyi atakuwa na desturi hii; atatwaa wana wenu na kuwaweka kwake, kwa magari yake, na kuwa wapanda farasi wake; nao watapiga mbio mbele ya magari yake.(Escort inayotangulia mbele ya Raisi nk kabla gari yake)

12 Naye atawaweka kwake kuwa maakida juu ya elfu, na maakida juu ya hamsini; na wengine atawaweka walime shamba lake, na kuvuna mavuno yake, na kufanyiza zana zake za vita, na vyombo vya magari yake.( Kuwapa vyeo awatakao wengine mawaziri,wakuu wa mikoa ,wilaya ,mahakama nk anavyojisikia mwenyewe ampe cheo nani)

13 Na binti zenu atawatwaa kuwa wafanyaji wa marhamu, na wapishi, na waokaji.(wafanyakazi serikalini)

14 Atatwaa makonde yenu, na mashamba yenu ya mizabibu, na ya mizeituni, yale yaliyo mazuri sana, ili awape watumishi wake.

15 Naye atawatoza ushuru (ushuru wa bandari,wa mazao ,forodha, miamala ya simu nk ) wa mbegu zenu na wa mizabibu yenu, awape maakida wake, na watumishi Wake.( Ili wapate mishahara na marupurupu manono wa serikalini,bungeni na Mahakamani Kwa wananchi wanayotozwa)

16 Atawatwaa watumishi wenu na wajakazi wenu, na ng'ombe zenu walio wazuri sana, na punda zenu, naye atawatia katika kazi zake mwenyewe.(utaifishaji Mali na kuzifanya za umma na kutoa ajira serikalini) nk

17 Atawatoza fungu la kumi la makundi yenu (asilimia ya Kodi Kila Pato lako); nanyi mtakuwa watumwa wake.(wafanyakazi wa Serikali badala ya watu kujiajiri)

18 Nanyi mtalia siku ile kwa sababu ya mfalme wenu mliyejichagulia; Bwana asiwajibu siku ile.( Kulia Kodi kuwa kubwa ,vifurushi ,mara oh Haki hamna kwenye mihimili liwe bunge ,mahakama au Serikali,ufisadi ,rushwa uwe ya barabarani ya traffic ofisini nk)

19 Walakini hao watu wakakataa kuisikiliza sauti ya Samweli; wakasema, Sivyo hivyo; lakini tunataka kuwa na mfalme juu yetu;

20 ili sisi nasi tufanane na mataifa yote; tena ili mfalme wetu atuamue, tena atoke mbele yetu na kutupigia vita vyetu.

21 Samweli akayasikia maneno yote ya watu, akayanena masikioni mwa Bwana.

22 Bwana akamwambia Samweli, Isikilize sauti yao, ukawafanyie mfalme.
 
Hakuna kisicho na Historia hapa duniani

Ndio hivyo Tena Hata mifumo ya Sasa ya tawala za Serikali Historia ndio hiyo
Hakika. Kipindi fulani niliwahi fuatilia sana kitabu cha Daniel hasa kwanzia sura ya 11 ndipo baadae katika historia nilikutana na scripture fulani zinaelezea tangu kuvunjika kwa utawala wa Alexander mkuu na tawala kuangukia kwa wale generals wake na kuibuka kwa Julius Caesar na the whole story hadi kwa kina Cleopatra na nini hiyo chapter ililenga.
Hivyo hakuna kisicho na historia.
 
Hongera kwa kusoma biblia
 
Sahihi
 
Biblia kuna muda inakuwa na ujinga mwingi,Mungu alijua kuwa watu wake watataka mfalme kipindi fulani,halafu Mungu huyo huyo aseme watu wake wamemkataa?
Halafu soma hapa haya ya tano
5 wakamwambia, Angalia, wewe umekuwa mzee, na wanao hawaendi katika njia zako; basi, tufanyie mfalme atuamue, mfano wa mataifa yote.
Ufalme haukuanzia Israel na ndiyo maana wakaomba awafanyie ufalme kama Mataifa mengine.
Labda useme Mungu alikuwa mfalme wa Israel lakini mataifa mengine yalikuwa na wafalme.
 
Soma kwa kutulia ujifunze kitu, usiwe na haraka kama uharo mkuu
 
Biblia kuna muda inakuwa na ujinga mwingi,Mungu alijua kuwa watu wake watataka mfalme kipindi fulani,halafu Mungu huyo huyo aseme watu wake wamemkataa?
Halafu soma hapa haya ya tano
5 wakamwambia, Angalia, wewe umekuwa mzee, na wanao hawaendi katika njia zako; basi, tufanyie mfalme atuamue, mfano wa mataifa yote.
Ufalme haukuanzia Israel na ndiyo maana wakaomba awafanyie ufalme kama Mataifa mengine.
Labda useme Mungu alikuwa mfalme wa Israel lakini mataifa mengine yalikuwa na wafalme.
Aliyezeeka ni Samuel sio Mungu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom