Jinsi nilivyonusurika kuuawa Arusha sababu ya mapenzi

mutu ya momba

New Member
Jan 28, 2016
4
11
Basi bwana siku moja nikiwa Dom, simu ikaita, kuangalia hivi ni 'baby' wangu wa zamani ati anataka niende kumsalimia ati kanikumbuka, mara kakumbuka 'show' za kibabe pamoja na kunibania pua mradi tu nimuelewe.

Nilikuwa natamani kwenda Arusha na kweli nimemkumbuka hatari, nikaona isiwe kesi ngoja nikamwangalie huyu mrembo. Katika mawasiliano akadai kuwa nitafikia kwake kwani anaishi yeye mwenyewe na beki tatu tu.

Hapo nikasita kidogo, nikawaza usintanie wewe lodge ziko kibao tutachagua moja, kwani hela kitu gani? Mtoto akadai ooh hajazoea lodge na sababu zingne kibao za kishua na kilokole humohumo. Kinyoonge nikaona isiwe kesi, nikamwambia kesho mapema natia timu.

Basi bwana nikaamka asubuhi, nikadaka basi la Shabiby, nikafika Chuga mtoto kaja kunifuata stendi na kimkebe (ki IST), amekuwa mkali hatari. Nikasita kidogo hivi, kweli machalii ya R wamemuacha huyu? Basi tukaingia huku na huku nikafika kwake.

Nyumba kali hatari, nikajiuliza mh, huyu anaishije nyumba kali hivi, kodi anapata wapi? Nikiwa najiuliza maswali kichwani nikavutwa chumbani, nikaona bwana wee itafahamika baadaye. Mchezo mdogo mdogo mpaka usiku usiku, mwanamke akanambia twende baa 'tukajiboost' kidogo, nikaona poa.

Tukaenda baa ya jirani tukaanza kupata moja moto moja baridi, ghafla nikahisi kitu, nikamkumbuka 'home boy' wangu mmoja ni polisi kwenye jiji hili, nikamtafuta, nikamwambia niko kipande hiki. Akanambia kuwa makini, hapa siyo Dom kuna vibaka hatari, ikitokea kuna dharura nimtafute anaweza kusaidia, nikamwambia poa.

Basi bwana tukaanza kurudi nyumbani tumelewa kiasi pamoja na mabusu barabarani kama tumeuziwa Dunia hivi. Basi bwana ile kufungua geti tu nakutana na pande la mutu, mbaba kashika silaha mkononi, nikajua hili ni panga, ananifuata kwa nguvu. Nikajua hapa nauwawa, nikirudi nje nitakimbizwa kama mwizi ntauwawa pia.

nkakumbuka karate kombat za kipindi hicho, nikamuhesabia hatua nikamfuata tukakutana katikati, nikamdaka mkono, kumbe halikuwa panga, ilikuwa ni fimbo kubwa. Basi ile kusukumana nikapata upenyo kuna chumba kilikuwa wazi nikaingia nikajifungia.

Yule jamaa akaanza kumpiga yule mwanamke (kumbe ndiyo mlipa kodi pale), mi nikaanza kupiga kelele kuomba msaada, hakuna mtu anayetoka. Yule jamaa akaanza kupiga simu kuita wahuni wenzie, nikajua nauwawa leo, tena nauwawa kishamba sana kwenye mji wa watu.

Ghafla nikakumbuka namba ya 'home boy', yule pot(Don Caro), nikamtafuta, nikamwambia kuwa niko hapa nimefumwa na jamaa anaita wenzie. Dakika tano nyingi nitakuwa tayar kwa Israel. Kama hutawahi utawaambia ndugu zangu nilikufa kifala, fanya hima.

Basi dakika za kuhesabu Don Caro huyu hapa na mapot wa kutosha wakamdaka jamaa, wakamvalisha bangiri, wakanichukua tukaondoka. Nikaenda kulala kwa Don Caro. Asubuh na mapema nikawa narudi Dom, sikuamini kama nimepona.
 
Mshukuru Don Caro la sivyo leo ungekuwa unahadithia mingine jinsi ulivyogeuzwa demu na bwana wa demu wako.

Vyovyote itakavyokuwa, ni marufuku kwa mwanaume kulala nyumba ya mwanamke usiejua anaishije hapo.
 
Cheap is always expensive.

Uliepuka gharama za lodge/hotel kwa kuweka rehani mwili wako

Next time usilale kwenye chumba/nyumba ya mwanamke usiejua analipa je kodi au aliijenga vipi hiyo nyumba.
 
Back
Top Bottom