Mwamba wa Tanga
Member
- Apr 4, 2024
- 86
- 290
Habari wakuu natumaini mko salama.
Kisa hiki kilinitokea mwaka 2007
Pala Arusha njiro
Nilikua nachukua ujuzi wa kuchomelea mageti na vitu vingine vya Jamii ya chuma . Nilikua mwaminifu sana na akili nyepesi ya kutambua haraka kazi
Ofisi yetu ilikua nane nane njiro ofisi yetu ilitazamana na Bp.
Siku ya tukio niliwahi sana work shop nikamkuta fundi msaidizi tulizoea kumwita Papaa
Kwanamna nilivyomkuta alikua anaongea na jamaa mmoja sikumfahamu nikawasalimia nikakaa pembeni
Story zao ilikua ni mambo ya starehe tu
Fundi mkuu alivyokuja bwana Mjema wakavutana pembeni wakaongea kwa kirefu mpk wakakubaliana.
Ndipo nikaitwa nikaambiwa niondoke na yule jamaa pamoja na kifaa Ile drill machine Ili jioni akimaliza kazi Mimi nirudi nayo work shop.
Sasa yule jamaa ni fundi rangi na kazi ya kupaka rangi alishamaliza kwahio akaomba kazi ya kuweka gypsum akaambiwa aweke sample Ili boss ajiridhishe
Kazi ya rangi alishalipwa pesa yake yote lkn vijana wake hakuwalipa kawaambia bado nadai.
Sasa kwasababu aliweka sample ya gypsum boss kaja saiti asubuh kawakuta vijana wa fundi akawaambia huyo fundi wenu akija mwambieni aondoke hii kazi haiwezi na kazi ya rangi hanidai
Boss akasepa .. kwahio vijana wakajua wametapeliwa kwahio lzm na wao wafanye Jambo wapate pesa Yao
Tulivyofika saiti nikakuta vijana 4 nje ya geti wakampokea fundi wao Ile mashine
Fundi kajiona mwamba kupokewa mashine vijana wakasepa yeye anaingia ndani anakuta ujumbe kwa Masai tena akamwambia mbona vijana wako wanajua
Dah 😒 fundi ananiambia sasa dogo twende ukachukue mashine urudi kazini kwako nkamwambia poa
Hapo tupo njiro stand njia ya kwenda kambi ya FFU
Tukapanda Hiace mpk mjini
Muda mwingi alikua anaongea na simu kilugha
Mwisho kbs ananiambia twende ngarenaro ofisini kwangu ukapate msosi hlf uchukue mashine urudi
Ndugu zangu wakati huo Mimi nina miaka 16 na ndo naingia Arusha kutokea Tanga kwahio yule jamaa mtoto wa mjini kitambo akawa ananiburuza tu
Tulifika kwenye saloon ya kiume ananiambia nisubiri nje
Akaingia kama dakika 5 akatoka akaniita nikaingia ananiambia sasa dogo nisubiri hapa usiwe na wasiwasi nakuja
Alivyoondoka nimekaa pale kama lisaa limoja hv
Wateja ikawa hamna jamaa wa saloone ndo ananipa pole ananiambia dogo pole bwana yote maisha utawahi tu kuzika kikubwa jamaa apate gari ya mizigo mchana huu .
Dah nikamwambia Mimi sijafiwa
Nikamwambia kisa kizima
Jamaa akasema dogo umetapeliwa
Ikabidi nimpe namba ya fundi wangu nilikua nayo kwenye karatasi akapigiwa akaja mpk pale akanichukua tukarudi mpk kule saiti
Ndo akapata story kumbe yule mwamba alikua anadaiwa mpk kwenye mabucha ya nyama
Basi ndo hivyo drill imeenda na yule Papaa kasema hamjui wamekutana tu pale work shop