Jinsi nilivyonusurika kutapeliwa!

Jinsi nilivyonusurika kutapeliwa!

Hawafai mkuu, wakiona umesanuka wanatoka nduki kubwa..

Tuwe macho jamani..
Kweli hii dunia tunatofautiana kufikiri. Yaani mtu anafedha za kubadilisha na humjui, anakuja anakuomba umsindikize halafu akugawie milioni 1 na wewe unaona kila kitu kipo sawa!!!!!!! Ujinga ilioje! Kwanza alipokufuata kukuomba eti mambo ya kujaza kwani umeajiriwa benki? Just ungemwambie aone wahusika! Jifanye kuzoea watu haraka haraka kuna siku utafanyiwa kitu kikubwa kuliko hicho!
 
Duh kama mm ilikuwa mwaka 2013 mliman city crdb mm ilibadilika kidogo mwenye pesa dollar alikuwa mmama kiswahili utadhan kashuka kutoka mtwara Leo mm pia nilifika stage zote kama ww nilikuja stuka jamaa ananiambia tukamchukulie lodge huyu mama...!
Nilimuuliza jamaa HV ww haupo nae huyu mama kweli?
Jamaa anashindwa kueleza ukimuungalia usoni mama wa watu anakapua in abnormal way nikawabia mm sitoki nje ya mliman city kama deal bora linishinde.
Sijui kitu gani kilinipush kiukwel sikuaga niliondoka zangu na kurud bank.
Toka siku hivyo nilijifunza kutokuwa na iman na MTU yeyote hasa ninapokuwa na pesa.
Na ungeibiwa ingekuwa vizuri sana kwasababu wewe ndio ulitaka kuiba. Kwa kifupi wewe na huyo mwanzisha thread ni wezi! Mtu atakuja akuambie umwonyeshe sehemu halafu upate malipo makubwa namna hiyo bila kufanya kazi? Eti ametoka shamba! Kwa hiyo wewe ulijiona ni mjanja na utumie ushamba wake kufaidi siyo?
 
Pole na hongera kwa kufuatilia mpaka ukaujua mchezo wote! Naamimi utakuwa umesaidia wengi. Nikishauri tu uitaje hiyo benki ili hata wao watoe tahadhari stahiki kwa wateja wao.
Asanteh mkuu,

Benki yenyewe inapendeleaga rangi ya kijani nadhan utakuwa umeifaham mkuu..!
 
Duh kama mm ilikuwa mwaka 2013 mliman city crdb mm ilibadilika kidogo mwenye pesa dollar alikuwa mmama kiswahili utadhan kashuka kutoka mtwara Leo mm pia nilifika stage zote kama ww nilikuja stuka jamaa ananiambia tukamchukulie lodge huyu mama...!
Nilimuuliza jamaa HV ww haupo nae huyu mama kweli?
Jamaa anashindwa kueleza ukimuungalia usoni mama wa watu anakapua in abnormal way nikawabia mm sitoki nje ya mliman city kama deal bora linishinde.
Sijui kitu gani kilinipush kiukwel sikuaga niliondoka zangu na kurud bank.
Toka siku hivyo nilijifunza kutokuwa na iman na MTU yeyote hasa ninapokuwa na pesa.
Duh! Mkuuu kumbe nawewe walikutoa nje ya benki kama mimi!
 
Kweli hii dunia tunatofautiana kufikiri. Yaani mtu anafedha za kubadilisha na humjui, anakuja anakuomba umsindikize halafu akugawie milioni 1 na wewe unaona kila kitu kipo sawa!!!!!!! Ujinga ilioje! Kwanza alipokufuata kukuomba eti mambo ya kujaza kwani umeajiriwa benki? Just ungemwambie aone wahusika! Jifanye kuzoea watu haraka haraka kuna siku utafanyiwa kitu kikubwa kuliko hicho!
Ni sawa mkuu,
 
Mimi nikiwa bank au kwny ATM huwa sitaki maongezi na mtu nisiyemjua
 
Na ungeibiwa ingekuwa vizuri sana kwasababu wewe ndio ulitaka kuiba. Kwa kifupi wewe na huyo mwanzisha thread ni wezi! Mtu atakuja akuambie umwonyeshe sehemu halafu upate malipo makubwa namna hiyo bila kufanya kazi? Eti ametoka shamba! Kwa hiyo wewe ulijiona ni mjanja na utumie ushamba wake kufaidi siyo?
Futa hiyo kauli yakusema mimi ni MWIZI tafadhari mkuu

Lengo langu ni kuwajuza watu yalonisibu ili wachukue tahadhar sababu haya ni maisha ofcorse hakuna anayejua kila kitu.... ila wewe unajiona much know
...ok it's up to you
 
Mimi nikiwa bank au kwny ATM huwa sitaki maongezi na mtu nisiyemjua
Mkuu uko kama mimi. Dunia ya sasa sio ya kuzoeana na watu kirahisi namna hii. Unakuta mtu anakuambia nina fedha nabadilisha na wewe humjui unaunga tela. Kama ni jambazi ameua na anafuatiliwa mkikamatwa utamwambia hakimu ''alikuokota'' benki wala hamjuani akuelewe?
 
Ngoja waje wanitokee mm tena nikiwa bank nawakomalia wasitoke had kwa mapolisi wale wa bank! Hapo ndio watakoma kuingia bank.
Hahaaa
Nooo! Usiweke ukaribu nao hata zero distance sababu wengine sio watu wazuri wana madawa wanakupulizia utatoa bila kupenda....
 
Futa hiyo kauli yakusema mimi ni MWIZI tafadhari mkuu

Lengo langu ni kuwajuza watu yalonisibu ili wachukue tahadhar sababu haya ni maisha ofcorse hakuna anayejua kila kitu.... ila wewe unajiona much know
...ok it's up to you
Mkuu mimi nikuulize swali? Hiyo milioni moja aliyokuahidi na wewe ukakubali kwenda unaona ilikuwa ni haki yako kuipata? Si inaonekana ulimwona jamaa kama ni zoba hivyo uka-take advantage?
 
Wakuu habari

Jana wakati nikiwa benki(jina kapuni) nilifanya taratibu zote, kuandikia form ya kuwekea pesa nikapanga mstari tayari kwa huduma... gafla akaja kaka mmoja hivi na kuniita falagha

" samahani naomba unisaidie kuandika hapa" yule kaka aliongea huku akiwa ameshika payinslip(fomu ya kuweka pesa) huku akitoa bahasha yenye USdollar alidai kuwa kapewa na wachina kwenye sheli flan( jina kapuni) thamani ya USD15000

Sijaanza kumwelekeza mara dada mmoja alikuwa karibu yetu akaingilia" hizo dollar hazi badilishwi hapa, labda benki ya postal"

Basi sababu mi niliitwa nitoe msaada niliamini kuwa jamaa kashapata msaada aende zake benki tajwa..

Ile nataka kuondoka nirudi kwenye line yule kaka mwenye dollars akasema " Naogopa kwenda peke yangu kama vip nisindikizen kisha pesa zitazotoka nitawapa milioni moja moja" mmh! Kusikia hivyo nikahairisha kwenda kwenye line.... nazidi kuingia kwenye mtego

"Nna haraka sana kama inawezekana iwe saivi" aliongea huku akitoka nje ya benki haraka haraka, tukabaki mi na yule dada " twende au tuache pesa ziende tu mm! Nikamwambia twende ila tuwahi maana nna pesa za watu hapa.....

NJIANI
...yule dada akawa anapiga simu " hallow eeeh hivi rate ya kubadili dollar ni shingapi?..... kama dollar 15000 hivi?...... duh haya haya tunakuja saivi(call ended)

Akanivuta pembeni kidogo na kwa sauti ya chini kusudi yule kaka asisikie ( dogo amesema rate siku ya leo ni kubwa hivyo ni milioni 32,000,000)

Kufika sehem jamaa akagoma kwenda eti anaogopa, twende sisi tukamchekie kwa yule mtu aliokuwa akiwasiliana na yule dada akatoa note moja ya dollar50, nakusema chukieni hii mkanichekie....

Tukakubaliana sawa tukaenda tukiwa mimi na yule dada ambaye hata simfaham wala sijawahi muona mayala!

Tulivyorudi
"Dollar iko sawa" yule dada aliongea, na sijui kwanini kila jambo yule dada alianza kuongea yeye( nahisi yule dada na yule kaka lao moja)

"Sasa mimi ngoja niwape mkanibadilishie mimi naogopa kutembea tembea" yule kaka aliongea na nilishindwa kuelewa anamaanisha nini

"Mimi siwaamini naombeni hela zenu mlizonazo na mimi niwape hizi dollar mkisha badili basi nitawapa hela zenu" yule kaka aliongeza .... hapo nilipata wasi wasi sana kwanini tumwachie pesa zetu.

Binasfi nilikuwa nna milion 1 ambayo ilitakiwa nii-deposit ambayo kwa mda huo niliiweka mfukoni, yule dada alikuwa amebeba begi na alisema ana milioni 5.

Kilicho nichanganya ni kumwachia pesa yule kaka kisha sisi twende kubadili pesa..

to be honest
Pesa sikutoa niligoma kata kata, yule dada alikuwa mstari wa mbele kunibembeleza nitoe pesa nilikataa na kuondoka kasiii....

PENDEKEZO
tufanye kazi, tuachee tamaa matapeli wangenizidi akili wangenitapeli...

Nawasilisha...
Da! Nilikutana na hii kitu mwaka 2013.hawa jamaa wananusa Sana hela.

Jamaa alikua Anatokea stendi kashika Bahasha akanisimamisha,baada ya salamu, "samahani unaifahamu hoteli(akaitaja) nikamjibu ndio, akaniambia yeye ni Mgeni anaenda kukutana na mtu hapo ampe mzigo(akafungua kidogo ile bahasha) mamaaaaaaaaaaaa vitu vinang'aa hatari. Akasema hizi ni dhahabu natakiwa kwenda kumkabidhi anipe hela,naomba unipeleke.KICHWANI ZIKAWA ZISHACHAJI MDA MREFU NIKAWA NA MCHORA TU! Nikamwambia,me nna kazi zangu saizi ntakuelekeza hutapotea.
Akatokea jamaa mwingine akawa kama anatupita hivi(mwenzake) akamsimamisha,akamuuliza kama ana ijua hiyo hotel, akasema haifahamu, jamaa akasema huyu anapafahamu ila anasema hana muda,akamwambia kama alivoniambia Mimi na akamwonesha madini hewa. Jamaa akatuahidi hela nzuri tukimpeleka. Basi jamaa akaanza kunishawishi balaa.. Kimoyo moyo nikawa nawacheka tu.nikawambia sasa hizo hela utatoa kweli, jamaa akasema ndio, nikawambia sasa nisubirini kidogo(dakika sifuri) niweke huu mzigo (nilikua nimeshika spea ya gari naelekea garage.
Wakanambia poa, SIJUI KAMA BADO WANANISUBIRI MPAKA LEO, mfukoni nilikua na hela moja hivi! Wale jamaa sio watu wazuri,ukiingia Tamaa tu umelia
POLE MKUU KWA USUMBUFU WALIOKUSABABISHIA NA HONGERA KWA KUWATAMBUA
 
Mimi nikiwa bank au kwny ATM huwa sitaki maongezi na mtu nisiyemjua
Yah pengine inaweza kuwa ni dawa but i think it not enough mhimu hapo kuacha tamaa ya pesa tu umeshinda kila kitu
 
Mkuu mimi nikuulize swali? Hiyo milioni moja aliyokuahidi na wewe ukakubali kwenda unaona ilikuwa ni haki yako kuipata? Si inaonekana ulimwona jamaa kama ni zoba hivyo uka-take advantage?
Ni sawa mkuu lakini sio fair kuniita MWIZI

Mwizi anachukua mali ya mtu bila ruksa sasa mimi nilikuwa naiba nini?
 
Hongera ulichomoka blocker hakuwa mzuri ndicho kilicho kuokoa vinginevyo ungelia kwenye biashara yoyote mwangalie sana yule anayeongezeka huyo ni bloke's akikusa umeshinda mchezo
 
Da! Nilikutana na hii kitu mwaka 2013.hawa jamaa wananusa Sana hela.

Jamaa alikua Anatokea stendi kashika Bahasha akanisimamisha,baada ya salamu, "samahani unaifahamu hoteli(akaitaja) nikamjibu ndio, akaniambia yeye ni Mgeni anaenda kukutana na mtu hapo ampe mzigo(akafungua kidogo ile bahasha) mamaaaaaaaaaaaa vitu vinang'aa hatari. Akasema hizi ni dhahabu natakiwa kwenda kumkabidhi anipe hela,naomba unipeleke.KICHWANI ZIKAWA ZISHACHAJI MDA MREFU NIKAWA NA MCHORA TU! Nikamwambia,me nna kazi zangu saizi ntakuelekeza hutapotea.
Akatokea jamaa mwingine akawa kama anatupita hivi(mwenzake) akamsimamisha,akamuuliza kama ana ijua hiyo hotel, akasema haifahamu, jamaa akasema huyu anapafahamu ila anasema hana muda,akamwambia kama alivoniambia Mimi na akamwonesha madini hewa. Jamaa akatuahidi hela nzuri tukimpeleka. Basi jamaa akaanza kunishawishi balaa.. Kimoyo moyo nikawa nawacheka tu.nikawambia sasa hizo hela utatoa kweli, jamaa akasema ndio, nikawambia sasa nisubirini kidogo(dakika sifuri) niweke huu mzigo (nilikua nimeshika spea ya gari naelekea garage.
Wakanambia poa, SIJUI KAMA BADO WANANISUBIRI MPAKA LEO, mfukoni nilikua na hela moja hivi! Wale jamaa sio watu wazuri,ukiingia Tamaa tu umelia
POLE MKUU KWA USUMBUFU WALIOKUSABABISHIA NA HONGERA KWA KUWATAMBUA
Asanteh mkuu,

.. hata mwanzo wazo la kuwa hawa ni matapeli lilinijia lakin nilikuwa nikiwachora tu... nijue wataishia wapi lkn kimoyo moyo niliapa sitawapa hata thumuni yangu shenz zao wale....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom