Jinsi nilivyonusurika kutapeliwa!

Jinsi nilivyonusurika kutapeliwa!

Hao hawakuwa tofauti na wale wanaotembeaga na pambo la dhahabu halafu mwingine anajifanya eti ni mshamba hajui kama ni dhahabu kuna siku kuna walinifata mitaa ya lumum ba Mwanza niliwatia adabu maana niliwakwanyua mitama ya kutosha,watu wa namna hiyo usiwakubalie hata kuwasikiliza.

Lukwafya
Hahahahahaha ulifanya la mbolea mkuu, afu ni kama ukiendelea kuwasikiliza wanakupumbaza zaidi yani!
 
Dada hii ingekula kwako vibaya sana, inasikitisha na kina mama au dada sasa wamejiingiza kwenye hii michezo michafu, ole wao wakikamatwa uswazi, kule watachomomwa moto tu..
Asanteh Mkuu,

Marekebisho kidogo mimi ni kaka/baba/mwanaume/mkuu
 
Hapo shukuru Mungu ulikua sehemu ya wazi ndio maana uliweza kuondoka sababu hawakua na ujanja wala ucjisifu kama umewashtukia...kitendo cha kukubali kuondoka nao tayari ulishajimaliza...yani hapo inaonekana walijua huwezi kuwasumbua ndio maana wakakupeleka kwenye mazingira ya kawaida next time ukikubali kuondoka na matapeli ujue umekwisha, watatumia diplomatic way kama hyo ya kukuomba uache pesa ukizingua wanachukua kwa nguvu na kipigo juu...the best oprtion ni kuacha tamaa....
 
"Dollar iko sawa" yule dada aliongea, na sijui kwanini kila jambo yule dada alianza kuongea yeye( nahisi yule dada na yule kaka lao moja)
Yaani muda wote huo ulikuwa hujahisi kitu? Yaani mpaka unatia huruma kwa upoyoyo wako. Hongera lakini kwa kusave hii kitu maana ulikuwa unaibiwa kitoto sana.
 
Hapo shukuru Mungu ulikua sehemu ya wazi ndio maana uliweza kuondoka sababu hawakua na ujanja wala ucjisifu kama umewashtukia...kitendo cha kukubali kuondoka nao tayari ulishajimaliza...yani hapo inaonekana walijua huwezi kuwasumbua ndio maana wakakupeleka kwenye mazingira ya kawaida next time ukikubali kuondoka na matapeli ujue umekwisha, watatumia diplomatic way kama hyo ya kukuomba uache pesa ukizingua wanachukua kwa nguvu na kipigo juu...the best oprtion ni kuacha tamaa....
Duuh! Aisee Asanteh sana mkuu

Tamaa mbaya sana...
 
Hakuna hela rahisi hivyo kaa mbali na hao matapeli kwa kweli................ mimi sio muumini wa hela chap chap isiyokuwa na chanzo kamwe..........................
 
Yaani muda wote huo ulikuwa hujahisi kitu? Yaani mpaka unatia huruma kwa upoyoyo wako. Hongera lakini kwa kusave hii kitu maana ulikuwa unaibiwa kitoto sana.
Shukrani mkuu,

Unajua hizi mambo unaweza ziona simpo, lkn ni mambo magumu sana, ukizingatia wengine wanatumia mpaka nguvu za giza kufanikisha utapeli!
 
Mbona wamekusitiri kwani kutoka benki hiyo ya mwazo mlitumia usafiri gani kwenda Posta?
 
Hakuna hela rahisi hivyo kaa mbali na hao matapeli kwa kweli................ mimi sio muumini wa hela chap chap isiyokuwa na chanzo kamwe..........................
Hakika mkuu, chamuhim hapo ni kufanya kazi nasio kutegemea pesa ya chap-chap.. kama nilichokifanya mimi.
 
Mbona wamekusitiri kwani kutoka benki hiyo ya mwazo mlitumia usafiri gani kwenda Posta?
Tulitumia miguu mkuu sababu kutoka benki mpaka posta umba ni mita kadhaa tu..!
 
Mimi watu kama hawa nilikutana nao natoka ndani ya Tanzania Postal Banki. Stori zao ni namna hiyo hiyo hata approach zao ni hivo hivo na mara nyingi wanaviziavizia karibu na mabenki. Mimi niliponea chupuchupu kama huyu jamaa, nilikuwa nishatowa benki tsh 2 455 000/=!!!!
 
Siku zote tapeli anamtafuta mwenye tamaa, kama unaweza kupata hela ya chapchap lazima uingie kingi
 
Ndo maana ulipona wangekupandisha kwenye gari ungetoka kapa mkuu
Mmm! Mmh! Mmmh! Ni kweli kabisa mkuu na hata uhai wangu ungekuwa rehani daah!

Tamaa mbaya!
 
...Una bahati umekutana na matapeli wasio wazoefu, kitendo chako cha kutoka ndani tu na kuwa pamoa nao ungepuliziwa dawa fulani na kukupoteza kabisa fahamu zako, ungezindukia jangwani huku kimilioni chako kikisombwa...
 
Mimi watu kama hawa nilikutana nao natoka ndani ya Tanzania Postal Banki. Stori zao ni namna hiyo hiyo hata approach zao ni hivo hivo na mara nyingi wanaviziavizia karibu na mabenki. Mimi niliponea chupuchupu kama huyu jamaa, nilikuwa nishatowa benki tsh 2 455 000/=!!!!
Hawafai mkuu, wakiona umesanuka wanatoka nduki kubwa..

Tuwe macho jamani..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom