macho_mdiliko
Platinum Member
- Mar 10, 2008
- 28,277
- 56,963
Utapeli wowote una kanuni moja muhimu: mtu anakuvutia kuwa utapata pato nono kwa kufanya kazi ndogo sana! Ukiishaijua hii kanuni wala hutakaa utapeliwe kirahisi namna hii. Halafu hii aina ya utapeli anayoiongelea mwanzisha thread ni ya siku nyingi mno mno ila version zinabadilika tu! Nakumbuka zamani sana nilishasikia bibi yangu anahadithia babu yangu akiwa kijana alienda mjini akakutana na wale waangusha pochi. Mbele anatangulia mtu anaangusha pochi halafu nyuma anakuja mwenzake ambaye humjui na kukushawishi muichukue mkagawane kilichopo. Matokeo yake ukienda wanakuchenjia uchochoroni na kukunyanganya kila kitu. Sasa mwanzisha thread alifanya kosa kubwa sana kukubali kufuatana nao kwani wangeweza kutumia nguvu kuzichukua zile fedha.Da! Nilikutana na hii kitu mwaka 2013.hawa jamaa wananusa Sana hela.