Jinsi ndege ya Rais Habyarimana ilivyotungiliwa

Poppy Hatonn

JF-Expert Member
Apr 9, 2021
2,101
2,711
Naitafsiri kidogo Ile posting ya JF ya Jager Master ya Dec, 2011.

Hii makala ya 2001, imeandikwa na kachero Wayne Madsen. Anasema Marekani Wana kambi Cyangugu, Rwanda karibu na mpaka wa Congo.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani mara nyingi inaàjiri PMC (private military contractors) ambao zamani walikuwa wanaitwa 'mamluki'. Haya mambo yameandikwa 2001.

Hawa Marais waliopo madarakani sasa hivi Uganda, Rwanda, Ethiopia, Angola, Eritrea na DRC wanaongoza nchi nchi zenye vurugu kubwa za kikabila na kisiasa ambazo zinawezesha kampuni za madini za kimataifa kupeana mali za Afrika.

Hizi kampuni nyingine zinashirikiana na PMC zilizotajwa hapo juu. Kwa mfano, American Mineral Fields Inc,ambayo ilishiriki sana katika kumuweka hayati Laurent- Desire Kabila madarakani. Kampuni hiyo inamilikiwa kwa kiasi kikubwa na washirika wa Bill Clinton.

Pia, lengo moja kubwa la RCD, Warwanda wanaopigana Congo dhidi ya Kasbila ni kuwasaidia Barrick Gold kupata madini.

Sasa hivi,Barrick na makumi ya makampuni ya madini yanachochea mgogoro wa Congo.

Vurugu za sasa, Afrika ya Kati zinasababishwa kwa kiasi kikubwa na tukio la Aprili 6,1994, liliporushwa kombora kwa ndege iliyokuwa imembeba Rais wa Rwanda, Mhutu,Juvenal Habyarimana,na mwenzake, Rais wa Burundi, Cyprien Ntaryamira.

Oh, I am dead tired. Nitaendelea kesho. Inatoa ushahidi mwingi, kuliko unaohitajika kuonyesha Kagame kaitungua ile ndege. Pia unasema hawa watu ndio waliomuua Director wa TISS.. Labda, hakuna haha ya kuendelea(kesho). Yaliyoandikwa yanatosha.
 
Baada ya hii ndege kutunguliwa, Serikali ya Rwanda ikaanzisha yale mauaji ya halaiki ambapo watu 800,000 waliuawa. Baadaye RPF wakalipiza kisasi kwa kuua Wahutu 500,000,wengi wao wakiwa wakimbizi waliokuwa Zaire.

Watu walioutungungua Ile ndege mpaka leo hawajulikani ni kina nani,na hawajafikishwa mahakamani.

Umoja wa Mataifa ukifanya uchunguzi ukashindwa kuwapata. OAU ilifanya uchunguzi ikashindwa kuwabaini.

Mwaka 1988,Jaji wa zamani wa Ufaransa ,Jean-Louis Bruguire,alichunguza kushambuliwa kwa Ile ndege. Baada ya kuzungumza na mashahidi Switzerland,Rwanda, Tanzania,na Russia,Bruguire inaelekea ana ushahidi wa kutosha kuamuru hati ya kimataifa itolewe kumkamata Kagame.

Jaji mwingine mstaafu wa Ufaransa, Thiery Jean-Piere,ambaye sàsa ni Mbunge wa Bunge la Ulaya,katika uchunguzi mwingine kabisa wa kibinafsi alifikia uamuzi kwamba Kagame alikuwa nyuma ya shambulizi Hilo.

Wakati shambulizi hilo lilipotokea,RPF ilikuwa inasaidiwa na Marekani na Uganda.
Kabla ya shambulizi, miezi mitatu kabla ya shambulizi Jenerali Kagame alikuwa Fort Leavenworth, Kansas, kwenye General Staff College akipata mafunzo ya kijeshi,pamoja na mafunzo ya SAM( Surface to Air Missiles),katika kambi ya Air Force ya Barry Goldwater, Arizona.
 
Kabla ya shambulizi,miezi mitatu kabla ya shambulizi Jenerali Kagame alikuwa Fort Leavenworth,Kansas, kwenye General Staff College akipata mafunzo ya kijeshi,pamoja na mafunzo ya SAM( Surface to Air Missiles),katika kambi ya Air Force ya Barry Goldwater, Arizona.
Duh...!. Endelea...
P
 
Katika kutoa ushahidi mbele ya Kamati ya uchunguzi ya Ufaransa ( kumbuka Ile ndege ilikuwa inaendeshwa na rubani Wafaransa), Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Ufaransa,Bernard Debre alisisitiza kwamba makombora maeili ya SAM-16 yaliyotumika katika hilo shambulizi yalikuwa yametokea katika Jeshi la Uganda, ambayo probably walipewa na Marekani kutoka katika Vita ya Ghuba.

Aliungwa mkono na wakuu wawili wastaafu wa idara ya ujasusi ya Ufaransa (DFSE) Jacques Dewatre na Claude Silberzahn.

Waziri wa Ulinzi wa Habyarimana, James Gasana, aliyekuwa Waziri wa Ulinzi kuanzia April 1992 mpaka July 1993 alisema hawakuona sababu ya kupoteza fedha kununua SAM,kwa sababu RPF walikuwa hawana ndege. Kwa hiyo siyo sahihi kusema Wahutu waliitungua Ile ndege.

Haya maelezo ya hawa officials wa serikali ya Ufaransa DFSE yanaungwa mkono na majasusi wa zamani wa RPF ambao walitoa ushuhuda kwa U. N.

Hawa wanasema ndege ilitunguliwa na kikosi cha watu kumi cha RPF. Hizi ripoti alipewa Mkuu wa ule uchunguzi, Jaji Louise Arbor wa Canada ambaye hakuufanyia kazi,hasa alipoona Rwanda wanashutumiwa.
 
Back
Top Bottom