Ndege ya Kwanza kutengenezwa Tanzania yazinduliwa

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,109
49,811
Serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais Samia inazidi kuonesha na kutafsiri mafanikio ya sekta ya Viwanda Kwa vitendo.

Sasa ni zamu ya viwanda vya Kutengeneza ndege ambapo ndege ya Kwanza iliyoundwa ndani ya Nchi skyleader 600 imeoneshwa na kuzinduliwa rasmi kwenye maonesho ya wazalishajo wa bidhaa za viwandani yaani Tanzania international manufacturer expo Dar es Salaam.


My Take: Mafanikio haya ni ushindi mkubwa Kwa Rais Samia ambae Kila kukicha anatandika historia na kuacha alama.

Ikumbukwe kwamba Chuo Cha NIT kimeanza kufundishwa kozi za Urubani na uhandisi wa ndege na tayari Serikali imenunua ndege 6 za Mafunzo.

Haters wa Samia kina "Chadomo, Sukuma gang & Co Watanuna 😁😁😁😁" vumilieni mambo Bado huu ni mtori tuu nyama zinakuja.

===

ndeg.jpeg


Ndege ya kwanza kutengenezwa Tanzania imetambulishwa rasmi na kampuni ya Airplanes Africa Limited (AAL) ya mkoani Morogoro.

Ndege hiyo ilitambulishwa rasmi katika maonyesho ya kimataifa ya wazalishaji wa bidhaa za Viwandani Tanzania yajulikanayo kwa jina la Tanzania International Manufacturers Expo 2023 (TIMEXPO) yaliyomalizika hivi karibuni kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

Bw David Grolig alisema kuwa uamuzi wa kuzalisha ndege hiyo umetokana na mazingira mazuri ya uwekezaji hapa nchini.

Bw Grolig alisema kuwa ndege hiyo aina ya Skyleader 600 ina uwezo wa kubeba abiria wawili (akiwemo rubani) na inakidhi mahitaji ya wafanyabiashara wanaosafiri umbali mrefu.

Alisema kuwa walifanya utafiti wa kina ili kuelewa mahitaji ya wafabiashara ambao mara nyingi hufanya safari za masafa marefu na kutumia muda mwingi njiani.

Alifafanua kuwa kutokana na utafiti huo, waliamua kutengeneza ndege itakayowawezesha wafanyabiashara kusafiri kwa urahisi zaidi na kuhudhuria mikutano mbalimbali nje ya mkoa kabla ya kurejea na kuendelea na shughuli nyingine.

“Tunajivunia kutengeneza ndege ya aina hii ambayo ni muhimu kwa wafanya kibiashara na watu binafsi. Huu ni mwanzo na mwakani tutatengeneza ndege nyingine aina ya Skyleader 500 ambayo ni muhimu kwa matumizi ya kilimo na shughuli zingine.

Ndege zote hizi ni matunda ya ubunifu wa wataalamu wetu wazawa na wa kigeni. Watalaamu wazawa wamepata mafunzo Jamhuri ya Czech na mipango ya kuendelea kutoa mafunzo inaendelea ili kuwa na wataalamu wengi zaidi,” alisema Bw Grolig.

Alisema kuwa umiliki wa ndege hiyo ni rahisi zaidi na wamefanya hivyo ili kuendeleza gurudumu la uchumi kwa Watanzania na wateja wao wan je ya nchi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi mwenza wa kampuni hiyo, Bw. Igor Stratil, alisisitiza kuwa ndege hiyo Na.1 ni matokeo ya utaalamu wa pamoja ya timu ya Tanzania na Czech.

Bw Stratil alisema pia wamefurahi kushiriki katika maonyesho ya TIMEXPO na kuwa washindi wa jumla.

Maonesho hayo yalifunguliwa rasmi na Waziri wa Elimu, Sayansi, na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, na kushirikisha ambapo jumla ya washiriki 138 washiriki na wageni zaid ya 1,000 walikuwa wanatembelea kila siku.

Miongoni mwa waliohudhuria ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw Albert Chalamila, ambaye alifunga maonyesho hayo na kuwapongeza waandaaji na kampuni ya AAL kwa maendeleo ya sekta ya viwanda nchini.

Bw Chalamila alisema kuwa ubunifu wa kutengeneza ndege ni kichochea maendeleo ya teknolojia na nyenzo pekee ya kuvutia wawekezaji wengine na kuchangia ustawi wa jamii.
 
Tulizeni mshono sio ndege tuu Hadi kiwanda Cha kulinda meli kimeanza kujengwa Kila kitu kitapatikana hapa hapa Tanzania 🔥🔥🔥

View: https://twitter.com/east_facts/status/1712127708082082255?t=2iieZ4h3VW_oRu2NB0K-kw&s=19

Inapendeza sana.Hiyo sehemu ya rubani ndio inaitofautisha na ndege nyengine tulizoziwea.Imefanana sana na uso wa FUSO.Ni ubunifu mzuri
Jina tu la hiyo ndege ndio sijalipenda kama vile ni mali ya mzungu fulani mwenye ubia na hicho chuo. ingeitwa Samia 1
 
Twrnde taratibu. Hapa unamaanisha kuanzia injini imepikwa hapo kiwandani ikapozwa na kuwa injini kamili hapohapo tanzani? Au wameunganisha vifaa ambavyo tayari vilisha pikwa kwenye viwanda vya huko nje?
Vyovyote viwanyo Mkuu wewe jua ni ndege imetengenezwa Tanzania,mambo ya parts hata Boeing Kuna vingine wanaagiza.

Mwisho pale Boeing Kuna Mtanzania anahusika na ujenzi wa Moja kwa Moja
 
Vifaa vyote vya ndege hiyo vililetwa kwenye maboksi vikaunganishwa (assembled) nchini na wajinga wa CCM tayari wanasema Tanzania imetengeneza ndege! Kwanini nyie CCM msiwasaidie wale waliotengeneza helicopter pale Arusha Technical College miaka zaidi ya 5 iliyopita ili wafikie viwango vya kimataifa?
Ni hatua kubwa,wapi kwingine Afrika Wana assemble hizo ndege zaidi ya Tanzania?
 
Ni hatua kubwa,wapi kwingine Afrika Wana assemble hizo ndege zaidi ya Tanzania?
Nchi nyingi sana A. Kusini, Namibia, Egypt, Kenya, Mauritius, Ethiopia, etc

Tena Africa Kusini wanatengeneza kabisa:

Sling Aircraft (Pty) Ltd (Previously known as The Airplane Factory or TAF) is a light aircraft development, manufacturing and maintenance organisation. Based in Johannesburg, they design, manufacture and market the highly acclaimed Sling range of light aircraft.
 
Nchi nyingi sana A. Kusini, Namibia, Egypt, Kenya, Mauritius, Ethiopia, etc

Tena Africa Kusini wanatengeneza kabisa:

Sling Aircraft (Pty) Ltd (Previously known as The Airplane Factory or TAF) is a light aircraft development, manufacturing and maintenance organisation. Based in Johannesburg, they design, manufacture and market the highly acclaimed Sling range of light aircraft.
Kazi iendelee 👇

View: https://twitter.com/RashdaZunde/status/1709455595978285184?t=02b2mqUjX3icU_otlNXFrg&s=19

View: https://twitter.com/WizarayaUC/status/1709096148944724449?t=i0qjjtBMPqKAhXVzhGASYg&s=19
 
Back
Top Bottom