Tulimsuta Ndugai akaomba radhi na kulazimishwa kujiuzulu. Leo mnalia nini?

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,755
Leo ni michano

Kuna watanzania ni machiriku wa kuongea. Wanaongea bila hata kujua maana ya wanachokiongea.

Desemba 28 2021 Spika wa Bunge Ndugai alikosoa kasi ya ukopaji inayofanywa na serikali akitoa tahadhari kuwa kuna siku nchi itakuja kuuzwa.

Wakali wa verse wakalipuka kuwa anaisaliti na kuipinga serikali. Alisutwa akajaa na kujitokea kuomba radhi kwa maoni yake yale. Ikumbukwe serikali inajinasibu kuheshimu Ibara ya 18 ya uhuru wa maoni lakini shahidi wa Nazareti uhuru wake baada ya maoni ulipigwa roba ya mbao na Utawala Bora. Hatimaye akajiuzulu na kukaa kimya.

Hata kabla hatujakaa sawa tukaanza kuona ishu zinapambamoto huko Loliondo, watu wanahamishwa kwa nguvu huku neno hiyari likitumika kuipaka rangi siasa.

Leo nchi nzima inabembelezwa ilie na wale wale machiriku wakidai bandari inauzwa. Wasichokijua ni kwamba hili suala la nchi kuanza kuuzwa halikuanza jana. Wanajua kuwa Ndugage alikuwa sahihi kwani mkataba huu wa Bandari ni chanzo tu cha kupima kina cha maji.

Mkurugenzi wa TPA anasema nchi zimeshaingia mkataba hivyo gelesha ya kuupeleka bungeni ni hadaa kwa wananchi ionekane wabunge waliridhia. Pia hili limevuja ili tusijadili kupinga sheria mbaya kwa taifa ya kutoa kinga kwa wale jamaa zetu wanaonyooshewa vidole kutumika kuua, kuteka, kutesa na kuhukumu wakosoaji wa serikali. Hayo marekebiaho yatapita na hakuna atakayetapinga. Mkataba utapita na povu tunalolitoa leo tutaenda kufulia nguo kesho.

Tufikirie miaka 100 ijayo wajukuu zetu wataishije. Tuache kuwaza kama hatujui kuna kesho. Akina Livingstone. Carl Peters etc walijitoa mhanga kwa ulaya ya leo. Waliishi ndoto na matumaini ya vizazi vya ulaya ya leo.

Sisi tunapambania matumbo yetu.

Unafiki tuache. Tuisaidie nchi. CCM ni kinara wa rushwa na ufisadi na hivi wanajua wananchi wamewachoka, basi wanaingia mikataba isiyoponyeka maana wao na familia zao wataishi kwenye hayo matendo yao maisha yote
 
Nijuacho suala la bandari ni la tangu awamu 2 zilizopita. Ndugai ni miongoni mwa watu tuliowalaumu kushawishiwa kwa chochote kupitisha maamuzi ya kubinafsisha bandari. Nashangaa leo tunachanganya mafaili
 
Acheni kujitoa ufahamu huyo Ndugai point yake kubwa ilikuwa ni kutetea uanzishwaji wa tozo ambazo sasa hivi zinatutesa sana wananchi wa kipato cha chini Bure kabisa huyo Mzee.
 
Ndugai alitaka kumalizwa ndio mzee malecela akamsanua. Saa hizi angekuwa hayati..ndio ujue hili suala ni zito.
Waliomsuta Ndugai na kumlazimisha kujiuzulu ni ccm wenzake. Kwa wananchi wengine wenye akili zao timamu huo ulikuwa ukiukwaji mkubwa wa katiba ya nchi hii. Pamoja na kwamba Ndugai aliharibu Bunge la nchi hii, kama raia na kiongozi wa mhimili wa dola alitendewa vibaya sana.
 
Siyo bandari tu tena ikiwezekana taasisi zote nyeti wapewe wageni labda tija itapatikana. Watu wetu wengi wamekuwa wezi na mafisadi wakubwa na hawana uchungu na nchi zaidi ya kufikiria maslahi yao binafsi.

Ikiwezekana hata jeshi la polisi wakabidhiwe wageni pengine kuna mabadiliko tutayaona. Kazi yetu kulalamika tu lakini tukipewa nafasi utendaji ni sifuri tu. Angalia kila kitu chetu ni ovyo tu: barabara mbovu, huduma mbovu ili mradi shaghala baghala.
 
Back
Top Bottom