Jinsi mabenki yanavyowaibia watumishi wa umma kupitia mikopo

Yaani mkopo wa milioni 6 kwa miaka 8 huyo jamaa ni mpuuzi si achukue miaka miwili atakatwa kila mwezi 285,251 kwa miaka miwili na riba itakuwa 846,024 sawa na 6,846,024 kwa riba ya 13% huyo itakuwa mwalimu ndo wanapenda shida
Swala la mikopo weng hawajui na weng wanafikiri kukatwa kidogo kwa muda mrefu ndio nafuu kumbe anaumizwa pasipo kujua.

Wengi wanakopa pasipo kupata ushauri toka kwa wataalamunwa fedha na benk walio huru(nje na taasisi alolenga kukopa)
 
Kabla ya kuomba mkopo tunawatumia wao kutupatia ushauri wa nini nifanye, sio kila mmoja amesoma uchumi.

Cha ajabu ushauri wanaonipatia hata mimi nisiesoma uchumi siwezi kumshauri mtu afanye.

Actually riba ilikua 16% plus hiyo processing fee ilikua almost 4 Million.

Hizi benki zinatakiwa kuwa msaada kwa watumishi kwasababu ndio kundi kubwa zaidi linalozifanya ziwe hai, maana yake zilitakiwa kuweka mikopo isiyoumiza sana, angalau riba 11% per annual.
Kuna benki moja wana 13%.

Ila nikushauri ktk maisha kuwa na marafiki wa kada mbalimbali hutojutia.
 
Shida ipo kwenye top up, ukifanya top up kwenye mil 6, wanakupa mil 2. Hiyo mil 2 itasababisha ulipe mil 16. Hivyo kama ulikopa mil 10 watachukua mil 4+16= 20 mil. Chanzo chao Cha biashara ni mil 12 tu.
NA. (Not Applicable )


Hadithi
 
Mie nashauri Kwa mwenye malengo kopa fanya malengo hatuna bima za maisha unaweza ajiriwa ukafa ndani ya miaka miwili na hujafanya kitu

Kujichanga mdogo mdogo ni ngumu sanaa hasa hasa ukitaka kujenga huwezi toboa kirahisi lazima ukope tu
Issue siyo kukopa.

Mkopeshaji ni nani na ana masharti yapi? Mkopaji una masharti yapi? Acha kwenda kwa Lender na expectations za kijinga kichwani.
 
Benbulugu usifanye Top up.

Riba ikiwa flat au inayopungua.

Haina athari yeyote coz utapata kiasi unachotaka. Ila kuna gharama utalipia.

AKILI BANDIA TUPITE MFANO WA 6M LOAN.

Kaselele amekopa 6M kwa 2yrs, monthly repayments (mr) ni almost 285k. Profit ya benki ni 846k. Loan fee tuseme ni 2.5% yaani 150K.

Akafanya marejesho ya 1yr. Ambayo ni almost 3.423M (kiasi cha mkopo kilicholipwa ni 3M faida ya benki ni 423k)

TAMAA ZA BANDIA.
Kaselele anapata ushawishi wa kijinga kutoka kwa watumishi wenzio anatamani top up, baada ya kupandishwa daraja kazini. Anakuja tufanye top up.

NDANI YA KUMI NA NANE
Benki yangu inamdai #Kaselele 3M haijarejeshwa. Kaselele anataka top up ya 6M.

NOTE: [Kazi ya Credit Officer ni kufanya biashara, masuala ya FL //Financial Literacy kalipie ada ukasome huko kwenye makongamano ya KIDINI. Hope TUGHE, CWT etc waichukue FL kama compulsory kwa wanachama wao].

TUENDELEE.
Mkopo mpya wa Kaselele utakua ni 3M + 6M = 9M.

TUPIGE HESABU KIDOGO ya miaka 3.
Loan ni 9M kwa 3yrs
Mr itakua 303k
Profit ni almost 1.917M
Fees itakua ni 225k

*****TAFUTA UHALISIA
A) KWENYE MKOPO WA 12M kwa madirisha mawili ya miaka miwilimiwili bila top up, gharama zake zilikua ni (Fees 300k + Benki profit ya almost 1.68M= JUMLA NI 1.98M). Halafu rejesho lilikua 285k jepesi kidogo siyo.

B)KWENYE MKOPO WA 12M wa madirisha mawili yenye top up ndani yake wa miaka 4. Gharama zitakua ni fees (150k+225k= 375K) + Profit 423k + 1.917M = 2.35M JUMLA NI 2.725M. Halafu kuna rejesho la 303K zito kidogo kulinganisha na 285k.

Halafu 1.98M na 2.725M kuna tofauti ya almost 700k.

Niishie hapo kuhusu top up.


Kwa leo inatosha.
Kwahyo kuliko kufanya top up bora ukope benki ingine incase umebanana nashida??asante kwa ushauri lkn mkuu.
 
Habari za jioni GT...Niende moja kwa moja kwenye mada.

Mabenki nchini wanawaibia sana watumishi wa umma kupitia kinachoitwa mikopo ya watumishi. Nina rafiki yangu anafanya kazi serikalini. Juzi alienda kukopa pesa benki (NMB)...sasa shida ilianza juu ya mchanganuo wa mkopo, duh, ni hatari.

Kwa kiasi cha Tsh mfano 6M, unatakiwa urudishe almost zaidi ya 10M. Bado kwenye hiyo 6M uliyoomba, wanakata 8% kama processing fee. Hivyo, unajikuta unachukua net take home 5.4M. Kumbuka mkopo huu unakatwa kwa muda wa miezi 96. Yaani, unapewa 5.4M, unarudisha 10.6M. Hii ni sawa na riba ya 100%.

5.4M * 2 = 10.8M. Kwanini wasikopeshwe bure kama walivyo wafanyakazi wa BOT, NMB, NK ambao hawatozwi riba kwenye mikopo yao? Serikali ipo wapi kwenye wizi huu wa mchana?
Wafanyakazi wasipo kopa mabenk yanafungwa.
Au waje na njia nyingine ya kupata hela
 
Jamaa yangu amefungiwa huduma ya salary advance na NMB kisa amekopa benki nyingine tofauti na NMB ...ILA mshahara wake unapita NMB...
wakuu hii imekaaje?
 
Back
Top Bottom