Jinsi K Vant ilivyomkutanisha rafiki yangu na malaika

Ilikuwa ni jumamosi moja tulivu, nikiwa na watu wangu kadhaa tuliosoma wote shule ya msingi tuliamua twende kwenye pori moja lililo kilometa kadhaa kutoka kwenye kijiji ambacho kwa umoja wetu (tuliomaliza pamoja shule ya msingi) tuna shamba ambalo tulinunua kwa pamoja.

Basi tukanunua vinywaji mbalimbali vikiwemo vya nje ya nchi na vya ndani ya nchi.
View attachment 2025149

Tukaenda porini kuwinda swala na viwanyama vingine vidogodogo kama sungura.

Safari yetu ilikuwa ni nzuri sana, tulikuwa na maguire mawili, na upinde na mishale yake. Pia tulikiwa na mbwa wawili hodari wenye nguvu, mbio na weledi wa hali ya juu kwenye sekta nzima ya uwindaji.

Mbwa hao ni wabobezi mahiri wa kunusa, kukimbiza, kudaka na kudhibiti kitoweo bila kukidhuru ama kukiua.

Siku hiyo neema ilikuwa upande wetu, tukapata mbuni mmoja, swala mmoja na sungura watatu.

Tukawapakia wanyama wetu kwenye pickup na kurudi kijijini.

Kijijini mambo yakawa ni moto, maandalizi ya kitoweo yakapamba moto. Nyama ilikuwa ni nyingi kuliko idadi ya watu. Pombe nazo zikawa ni nyingi mno.

View attachment 2025147

Basi tukapiga mlo pale, nyama choma na vinywaji vya namna namna.

K Vant ilipata bingwa wake ambaye ndani ya nusu saa alikuwa amepiga mitulinga miwili ile ya mls 750.

Aliendelea kuzipiga na kuzitwanga kwa mbwembwe na kwa spidi ya ajabu.

Baada ya lisaa limoja na nusu ndugu bingwa wa K Vant akaanza kupoteza pambano.
Sasa ni dhahiri K Vant zikaanza kupanda ushindi wa kishindo kwa kasi.

Basi bwana bingwa wa K Vant akapoteza rasmi pambano. K Vant ikaibuka na ushindi wa TKO.

Jamaa akawa amelewa chakari sana na wala hajitambui tena. Tukampa nusu saa tukidhani ataamka.

Nusu saa ikapita na hakukuwepo dalili za yeye hata kutingisha kidole. Tukamvua nguo na kuanza kumpepea.


Miongoni mwetu alikuwepo mtaalam wa tiba mbadala, yeye akasema kwamba tumsugue bingwa kwenye nyayo zake kwa vipande vya mabarafu na malimao.

Zikatafutwa barafu hadi zikapatikana. Yakaletwa malimao yenye ujazo mkubwa wa kutosha.

Nyayo zikasuguliwa sana kwa malimao nanmabarafu hadi tukaisikia harufu ya K Vant ikitokea kwenye nyayo lakini bingwa hakujitikisha.

Mtaalam mwingine wa tiba mbadala akasema bingwa awakewe vipande vingi vya barafu kwenye nyeti ZAKE.

Kijiboksa kikatolewa na lundo la mabarafu yenye ubaridi mkali yakamiminwa huko. Lakini bingwa hakuisikia baridi hiyo hata kidogo.

Tupkaona huyu bingwa tutampoteza. Tukamuweka kwenye gari, nduki hadi hospitali ya wilaya.

Tulipofika bingwa akapikelewa, akapimwa presha na pulse rate. Haraka haraka kimbembe cha kutafuta mishipaya damu kikaanza ili awakened drip.

Akalazwa na tukaambiwa turudi kesho yake asubuhi ili tuone maendeleo yake.

Kesho yake tukafika jamaa hana fahamu
Kesho kutwa yake pia hana fahamu.

Daktati wa zamu aliyeingia night shifti akizungukazunguka Woking alishtushwa na sauti kali kuliko ile ya mtu aliaye nyikani.....Niko wapi huku, niko wapi?

Dokta akiwa kwenye clinical coat. Bingwa akaroppka shikamoo kaka malaika
Je hapa ndio mbinguni Penyewe?

Alisikika bingwa akiuliza.
------------------------

K VANT USIINYWE KWA KUTAKA SIFA, YENYEWE HAINYWI POMBE LAKINI INALEWESHA
Tarehe 2/01/2023 hii mada ni ya mwaka juzi ila imenichekesha mwaka huu thanks kaka Bujibuji Simba Nyamaume
 
Pole yake sana, alijitakia mwenyewe...
Hebu sogea bahari beach tupate 1,2,3
We mzeeee.......

Ova
20230101_182341.jpg
 
K vant balaa,hapa nashindwa hata kunywa supu kisa k vant ya jana.

Moto ninao,mpaka nikae sawa itanichukua muda.Mpaka sasa nineshakunywa lita 3 za maji
 
Back
Top Bottom