SoC02 Jinsi huduma za maktaba zinavyoweza kuinua hali ya maisha ya wa Tanzania

Stories of Change - 2022 Competition

giho

New Member
Jul 26, 2022
1
0
Maktaba ni jengo au sehem yenye mkusanyiko wa vitabu majarida magazeti, tamani, kumbukumu mbalimbali nk vilivyopo kwenye mfumo wa ki electroniki au vilivyochapwa(printed), vyenye tarifa zinazo elimisha na kuburudisha maktaba huwa na rasilimali za kiada na ziada.

Kuna aina tofauti za maktaba ambazo ni maktaba za uma (public library), maktaba za kitaluma(academic library), maktaba za kitaifa (national library) na zingine nyingi kwa lengo la kuhudumia jamii yote leo ninazungumzia maktaba za uma na mchango wake katika kuleta maendeleo.

Maktaba za uma ni pamoja na zile za mitaa/kijii, kata, tarafa, wilaya, mkoa na taifa.

Faida za maktaba kwa jamii
Huchochea elim ya kujitegemea (self centered education) kupitia maktaba hizi watu wanao uwezo wa kujisomea kwa muda wao nakujipatia elim na marifa juu ya kile wanachohitaji. Mfano unahitaji kuwa mwanatehama unaweza kutumia vitabu vinavyo husu TEHAMA na kuwa mtalam wa teehama bila kutafuta mwalim au msimamizi wa elimu hiyo.

Huinua elimu ya watu wazima kwa watu ambao umri wao hauruhusu kwenda shule wanaweza kupata elimu hiyo kwakutumia maktaba jambo hili husaidia wao kuinua kiwango chao ch elimu

Huimarisha tabia ya kusoma bila kikomo (lifelong learning), watu wanasema elimu haina mwisho kutokana na hilo watu wanatumia maktaba ili kujipatia marifa bila kujali umri wao wala hali ya kielimu. uwepo wa maktaba huwasaidia watu wenye kuhitaji kujifunza mambo mengi.

Kuburudisha watu wakati mwingine watu huenda maktaba kwa lengo la kupumzisha akili na kujiburudisha kwa kusoma vitabu vyenye maudhui yanayo burudisha. Mfano uwepo wa vitabu vya hadithi mkusanyiko wa video za burudani au kutoa ufikiaji sahihi kwa mitandao yenye mikusanyiko ya maudhui ya kuburudisha.

Husaidia kugawana marifa (knowledge sharing) baina ya watu inaaminika kuwa njia nzuri ya kujifunza ni kuwafundisha wengine hivyo maktaba nisehem sahihi inayo saidia watu wenye marifa kuongeza marifa yao kwa kuwapa wengine marifa. mfano daktari wa magonjwa ya ndani anweza kuchangia marifa yake kwa kuandika vitabu kitu kinachowafanya wengine wayajue yale anayo yajua. kupitia changamoto na maswali atakayo ulizwa na wasomaji wake mtalam huyo atajifunza zaidi. hivyo marifa yatakuwa yamegawanywa.

Hupunguza pengo la maarifa (knowledge gap) watu wanapo weza kupata uwezo wa kuingia maktaba na kupata vitabu wanavyohitaji, wanaweza kujua mambo ambayo wangefundishwa wakiwa vyuo hivyo pengo la tarifa kati yao hupungua. mfano unaweza kusoma historia ya nchi yako kwakusomavitabu vya historia mfano azzimio la arusha misingi ya tanu nk..

Licha ya kuwa na faida kibao huduma ya maktaba inazo changamoto nyingi mfano kutopewa kipaumbele na wanasiasa walio madarakani, kukosekana kwa sheria inayo tia msukumo juu ya umuhimu wa maktaba kwa taifa.
 
Back
Top Bottom