Jinsi gani ya kuchukua sampuli ya udongo wa kupeleka maabara?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,398
Heshima zenu wakuu!

Nataka nianze kuliandaa shamba jipya kwa ajili ya msimu wa kilimo mwaka huu.

Kwa kuwa ni eneo ambalo halijawahi kulimwa, nimeona ni vizuri nikaupime kwanza udongo wake ili nijue afya yake. Ni jinsi gani ya kuchukua sampuli ya udongo?

Je, nichukue wa juu kabisa au wa ndani kidogo?

Unahitajika udongo wa maeneo mangapi? (Shamba lina ukubwa wa eka 20)

Nini cha kuzingatia wakati wa kuchukua sampuli ya udongo?

Nawashukuruni kwa ushauri wenu.
 
Habari ya jioni kufanya sampling ya udongo inatakiwa uchukue sample 3 za sehemu tofatuti tofauti za shamba pia zenye sehemu tatu kwa kila sample kwa maelezo zaidi unaeza nicheck kwa WhatsApp 0765113160
 
Chukua sampo yasehemu tofauti katika shamba ila usichukue sampo ya udongo yasahemu uliyochoma moto(sehemu uliyochoma takataka wakati wa uandaaji wa shamba) na sehemu ambayo ulimwaga samadi yakuingia shambani
 
Heshima zenu wakuu!

Nataka nianze kuliandaa shamba jipya kwa ajili ya msimu wa kilimo mwaka huu.

Kwa kuwa ni eneo ambalo halijawahi kulimwa, nimeona ni vizuri nikaupime kwanza udongo wake ili nijue afya yake. Ni jinsi gani ya kuchukua sampuli ya udongo?

Je, nichukue wa juu kabisa au wa ndani kidogo?

Unahitajika udongo wa maeneo mangapi? (Shamba lina ukubwa wa eka 20)

Nini cha kuzingatia wakati wa kuchukua sampuli ya udongo?

Nawashukuruni kwa ushauri wenu.
-Kwanza kabisa, depth ya kuchukua sample inategemea na zao unalotaka kulima, lakini pia idadi ya sample shambani inategemea mkao wa shamba lako kama ni flat unaweza chukua sample moja tu lakini kama Lina miinuko na mabonde lazima sample ziwe nyingi.
-hatuchukui sample chini ya miti, kwenye vichuguu au kingo za shamba,
- kwahiyo kabla ya kuchukua sample lazima ulitembelee vizuri eneo lako kuangalia tabia mbalimbali kama miinuko, na rangi ya udongo, unatakiwa kuwa makini sana wakati wa kuchukua sample Ili ikuletee majibu sahihi.
 
Uko sawa mkuu
 
Chuo kikuu Cha SOKOINE morogoro (SUA) gharama ya analysis Kwa sample moja ni elf sabini mpaka themanini pia Kuna jamaa wamefungua maabara yao Moshi wao wanafanya 60 mpaka 70k Kwa sample moja
Maabara nyingi katika vituo vya Tari wanapima ila sio kwa lengo la kibiashara lengo ni katika masuala yao ya tafiti ni kama Sua tu.
Mfano wa Tari ni Tengeru,Ukiliguru,Uyole,kuna ile moja ya Chai pale Nyororo nimeisahau na maarufu sana ni TARI-MLINGANO na wadau wengi wanatumia hii.
Taasisi ya SUA haiko kwa lengo la biashara hivyo unaweza kukaa miezi hata mitatu kusubiria majibu kwa kuwa na wao wamebanwa na kazi zao kutoka katika maeneo yao au taasisi zingine za serikali.
Kwa Mashirika wengi wanatumia crop Nuts Arusha au IITA pale mikocheni,hawa mabwana wana maabara mpya na za kisasa na wanafanya pia kwa watu binafsi kama kibiashara.

Soil collection kama alivyoeleza mdau mmoja inategemea na tabia mfanano au mtofautiano wa shamba lako na hata sampuli zinategemea hayo na pia zao na mwisho depth ya ukusanyaji.

Ni taaluma za watu zingatia hilo kama ikikugusa uwe na mwongozo wa mtu.
 
Ulichoongea ni kweli mkuu lakini Kwa sasa teknolojia imekuwa sana watu wameanzisha maabara zao na kinachofanyika ni unapeleka sample wao wanafanya full analysis na recommendations
-kazi kubwa ya agronomist hapo ni kukupa muongozo wa namna ya kukusanya sample then kuinterpret majibu baada ya analysis ya sample.
-mimi Nina connection na watu wa SUA pamoja na wale wa Moshi Kwa ambaye atakuwa na uhitaji anaweza kunicheki kwaajili ya field survey na sample collection then tutazipeleka kwaajili ya analysis na kuinterpret majibu yako
 
Heshima zenu wakuu!

Nataka nianze kuliandaa shamba jipya kwa ajili ya msimu wa kilimo mwaka huu.

Kwa kuwa ni eneo ambalo halijawahi kulimwa, nimeona ni vizuri nikaupime kwanza udongo wake ili nijue afya yake. Ni jinsi gani ya kuchukua sampuli ya udongo?

Je, nichukue wa juu kabisa au wa ndani kidogo?

Unahitajika udongo wa maeneo mangapi? (Shamba lina ukubwa wa eka 20)

Nini cha kuzingatia wakati wa kuchukua sampuli ya udongo?

Nawashukuruni kwa ushauri wenu.
Chukua chukua sample NNE.Pembeni kona zote,katikati..

Gawa shamba plot A,B,C na D

Kila plot chukua udongo kidogo

Udongo kutoka plot zote changanya kupata udongo katika chombo kimoja

Udongo uliochanganywa nenda maahabara kapime

In short udongo nyanda za juu kusini
nauhaba virutubisho

soluhisho.lisha udongo kwa mbolea ya samadi au mboji

pia tumia chokaa mazao kuboresha udongo.

nimesema hivyo kwani nimeshiriki upimaji udongo nyanda za juu kusini.Upungufu unafanana kwa mashamba mengi
 
Ulichoongea ni kweli mkuu lakini Kwa sasa teknolojia imekuwa sana watu wameanzisha maabara zao na kinachofanyika ni unapeleka sample wao wanafanya full analysis na recommendations
-kazi kubwa ya agronomist hapo ni kukupa muongozo wa namna ya kukusanya sample then kuinterpret majibu baada ya analysis ya sample.
-mimi Nina connection na watu wa SUA pamoja na wale wa Moshi Kwa ambaye atakuwa na uhitaji anaweza kunicheki kwaajili ya field survey na sample collection then tutazipeleka kwaajili ya analysis na kuinterpret majibu yako
Agronomist kazi yake kubwa kubwa kama ulivyosema ni interpretation japo hata maagronomist wa hizo lab wanafanya vyema.
 
Chukua chukua sample NNE.Pembeni kona zote,katikati..

Gawa shamba plot A,B,C na D

Kila plot chukua udongo kidogo

Udongo kutoka plot zote changanya kupata udongo katika chombo kimoja

Udongo uliochanganywa nenda maahabara kapime

In short udongo nyanda za juu kusini
nauhaba virutubisho

soluhisho.lisha udongo kwa mbolea ya samadi au mboji

pia tumia chokaa mazao kuboresha udongo.

nimesema hivyo kwani nimeshiriki upimaji udongo nyanda za juu kusini.Upungufu unafanana kwa mashamba mengi
Depth please
 
Mfano kama

1)organic matter(Matamahuluku)Chimba centimeter 45

2)Kama whole soil profile chimba mita moja.

Nifafanulie unaitaka ipi?Na upo mkoa gani?
Zao analotaka kulima linamata zaidi kuliko hvo vingine, mfano soil profile description haihitaji kuchukua sampuli ya udongo
 
Back
Top Bottom