Jinsi Eric Shigongo alivyojiunga Chuo Kikuu akiwa na elimu ya msingi

Afanye huo mtihan wa form four anaogopa nn, kama alihonga huko akadhan UD atafanya janja janja aende hukoko alikopata shahada yake
ANAOGOPA KUPIGA ZERO FORM FOUR SIO MCHEZO

Ataibuka na division zero aabishe hiyo degree ya kununua na kufanyiwa research afanye mtihani wa form four kama kweli kichwani zimo

Aende kujisajili vituo vya private afanye tuone
 
Yeye si genius toka la 7 mpk degree afanye tuu masomo saba yale apate hicho cheti. Unajua anag'ang'ania asome UD sbb anataka statasi tuu. UD kazeni alete cheti cha form four tuu tena chenye C tano.
C tano hawezi toboa.MTIHANI WA FORM FOUR HAUIBIWI WALA KUHONGEKA ATARUKA NA DIVISION ZERO HUYO SANA KAJITAHIDI ATAPATA DIVISION FOUR YA MWISHONI

UDSM WAKO SAHIHI AKAFANYE MTIHANI WA FORM FOUR
 
Utakuta asilimia kubwa ya wafanyakazi wa TCU walikuwa UDSM kabla including akina Prof Baregu.
 
Hongera Shigongo.

Uzi huu umejaa mawazo ya kizamani kwamba elimu lazima iwe Darasa la Saba>Sekondari>A-Levo>Digrii. Njia yoyote nyingine mtazamo wa kizamani unaiona ni wa kambo. Sasa ni wakati muafaka kwa serikali kuhuisha mfumo rasmi wa kulinganisha elimu.

Mlenge
 
Hongera Shigongo.

Uzi huu umejaa mawazo ya kizamani kwamba elimu lazima iwe Darasa la Saba>Sekondari>A-Levo>Digrii. Njia yoyote nyingine mtazamo wa kizamani unaiona ni wa kambo. Sasa ni wakati muafaka kwa serikali kuhuisha mfumo rasmi wa kulinganisha elimu.

Mlenge
Elimu haina ujanja ujanja
 
Huu utaratibu hata Ulaya upo, mradi uwe na miaka 21 na unajua kusoma na kuandika. Lakini kuna course unaifanya kwa mwaka mmoja kupata credits za kuingia chuo. Katika hiyo course unafundishwa jinsi ya kuandika essay, kupeleka assignments, hesabu na Lugha ya kufundishia katika nchi uliyopo.
 
Vyuo vikuu vingine ni kichekesho. Utampokeaje mtu wa darasa la 7 chuo kikuu? RPL haisemi hivyo. Kuna gap kubwa sana kutoka darasa la 7 mpaka chuo kikuu. Ni lazima afike Form 4 halafu elimu ya Form 5-6 yaweza kurukwa kwa kutumia RPL au kwa wakati wa zamani kutumia Mature Age Entry processes. Chuo kikuu cha Tumaini kijitafakari kabla ya kujitakafarishwa kwa lazima kwa manufaa ya elimu ya juu wanayoidai kuitoa. TCU toeni ubabaishaji huu wa kitaaluma.
 
Huu utaratibu hata Ulaya upo, mradi uwe na miaka 21 na unajua kusoma na kuandika. Lakini kuna course unaifanya kwa mwaka mmoja kupata credits za kuingia chuo. Katika hiyo course unafundishwa jinsi ya kuandika essay, kupeleka assignments, hesabu na Lugha ya kufundishia katika nchi uliyopo.

New Zealand wana huu utaratibu, lakini mchujo wake si wa kitoto
 
Na hao watu wa kizamani ndio wameshika nafasi nyeti katika maamuzi ya kielimu.

Mimi si muumini wa ujinga huo.
Ila ninachokiona,ni hawa wasomi kutaka kuleta vikwazo ili waendelee kubaki wachache.Wengi wanaogopa changamoto kutoka kwa watu ambao hawakupitia mifumo hiyo
Hongera Shigongo.

Uzi huu umejaa mawazo ya kizamani kwamba elimu lazima iwe Darasa la Saba>Sekondari>A-Levo>Digrii. Njia yoyote nyingine mtazamo wa kizamani unaiona ni wa kambo. Sasa ni wakati muafaka kwa serikali kuhuisha mfumo rasmi wa kulinganisha elimu.

Mlenge
 
Licha ya kufeli darasa la saba, mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo amefanikiwa kuhitimu chuo kikuu akiibuka mwanafunzi bora aliyefaulu kwa kiwango cha juu zaidi.

Kabla ya kwenda chuo kikuu, anasema alijifunza lugha ya Kiingereza mtaani, kama wengine wanavyojifunza lugha ya makabila.

Shigongo aliibuka mwanafunzi bora Chuo Kikuu cha Tumaini alikohitimu shahada yake baada ya kupata GPA ya 4.8.

Akizungumza na gazeti hili kwenye mahojiano maalumu yaliyofanyika nyumbani kwake, Ipagala jijini Dodoma mwishoni mwa wiki, Shigongo alisema alifeli mara mbili darasa la saba na akadhani hiyo itakuwa mwisho wa safari yake kielimu.

Lakini, alipata bahati ya kwenda kusoma kozi ya mwaka mmoja ya unesi msaidizi wilayani Sikonge mkoani Tabora, lakini kutokana na mshahara kuwa mdogo anasema aliacha kazi na kukichana cheti alichokuwa nacho.

Kujifunza Kiingereza


Shigongo anasema alijifunza Kiingereza mtaani. “Kiukweli sikufundishwa, naongea Kiingereza kama lugha ya kikabila, ukiniambia adjective nini sijui, sijui adverb yale mambo mimi siyajui kabisa mimi naongea kama kabila.

“Mimi (Sikonge) nilikutana na kijana anaitwa Jesse alikuwa mtoto wa daktari anaitwa Camstra, ambaye ni surgeon (daktari wa upasuaji) aliyetokea Uholanzi.

Sasa mwanawe Jesse alikuwa hajui Kiswahili akawa rafiki yangu, mimi namfundisha Jesse Kiswahili yeye ananifundisha Kiingereza, kwa hiyo nikashika pale lugha.

“Kwa hiyo nilifundishwa namna ya kuzungumza siyo kujua hii ni adverb au adjective. Baadaye nilipojua Kiingereza nikaanza kuwa nasikiliza redio na kusoma gazeti la Sunday News. “Nikawa najifunza Kiingereza, nikisoma Sunday News na ‘dictionary’ (kamusi) lazima iwe pembeni.

Nilikuwa napenda sana kusoma safu za Wilson Kaigarula. Nimesoma sana ‘articles’ (makala) zake. Nasikiliza BBC English Service, nasikiliza KBC ya Kenya ya Kiin[1]gereza.

“Kama unaweza kujifunza Kisukuma bila kufundishwa darasani ni hivyohivyo, sasa nikaanza kusoma ‘noval’ (riwaya) za Sidney Sheldon, kitabu chake cha ‘The other side of midnight’.

“Sidney akanimeza, yaani ikawa mimi nasoma riwaya za Sidney mpaka nikawa naweza kukesha nasoma kitabu. Yaani sisi tulikuwa vijana wa mwanzo tukitembea na ‘noval’ mtaani. “Nikajenga utamaduni wa usomaji wa vitabu.

Sidney ndiye aliyeniathiri mimi style (mtindo) yake ya kuandika, nikawa napenda anavyoandika ‘flashback style’ anaanzia mwisho wa story, halafu anakuja kukupitisha,” anasema Shigongo.

Kufeli darasa la saba


Shigongo ambaye ni mjasiriamali na mwandishi wa habari anasema alianza darasa la kwanza mwaka 1977 Shule ya Msingi Gembe iliyopo jimbo la Solwa mkoani Shinyanga.

Baadaye anasema familia yao ilihamia mkoani Mwanza, eneo la Nyakato, ambako aliendelea darasa la pili mpaka alipohitimu elimu ya msingi.

“La saba nikafeli na wala sikushangaa kwa sababu nilikuwa sijawahi kufaulu mtihani wowote huko chini, mimi sikuwa mjinga ila mazingira niliyokulia nyumbani maskini, tumezungukwa na matajiri, kila ninakopita najiona kama fukara, hakuna mtu ananithamini, shuleni walimu wananigombeza, kwa hiyo nilikuwa nimejikatia tamaa.

“Hata wakati wa mtihani sifanyi juhudi yoyote ile, yaani kama niliwahi kupata maksi nzuri sana darasani ni asilimia 25, sijawahi kufaulu zaidi ya maksi hizo.

“Siku nilipopata asilimia 25 mwalimu alishangaa. Akaja kaka yangu mmoja akasema lazima usome, akanichukua na kunipeleka Buchosa kule tuliotoka kwenda kurudia shule.

Zamani ulikuwa unaweza kufeli halafu ukarudia.

“Nikaenda kurudia shule moja inaitwa Luhama nikasoma pale la saba nikafeli tena. Nilipofeli nikasema shule itakuwa imeshindikana hapa, la muhimu ni kufanya biashara,” anasema Shigongo.

Baadaye anasema alisikia taarifa kuhusu chuo cha uuguzi kilichopo Sikonge mkoani Tabora, akaamua kwenda kusoma kozi ya mwaka mmoja.

Alipomaliza kozi hiyo, Shigongo anasema alirudi kijijini alikoanza kufanya kazi kwenye moja ya zahanati zilizopo lakini aliokuwa akilipwa akilinganisha na umasikini uliopo kwenye familia yake akaona hautoshi kukidhi mahitaji yake, hivyo akaacha kazi.

“Mimi mshahara ule bwana ulinishinda, nikasema familia yangu ni maskini, wanalala chini na wanalala njaa, wazazi wangu wanadharauliwa na kila mtu na pale tunapokaa matajiri ni wengi wanatupa takataka kwetu kwa sababu kulikuwa na nafasi wanapafanya dampo.

“Nikasema lazima nifanye kitu, kile cheti cha nesi nilikichana nikaamua kwenda machimboni,” anasema Shigongo.

Alivyojiunga chuo kikuu

Kuhusu alivyoingia chuo kikuu ilhali yeye ni mhitimu wa darasa la saba, tena aliyefeli, Shigongo anasema hiyo ilitokana na kipaji chake cha kuandika.

“Mwaka 2017 nikasikia hiyo habari ya Recognition of Prior Learning (RPL) kutoka kwa Godwin Gondwe. Na mimi kwa wakati huo nilikuwa nimeshaandika kwa miaka mingi sana.

“Nimeandika kwa zawadi ya Mungu bila kufundishwa na mtu yeyote wala mahali popote.

Sasa nilikuwa nimeandika vitabu vingi sana, na kumiliki kampuni ya habari.

Lakini, wakati wote huo sikuwahi kusoma ‘mass communication’ mahali popote na elimu yangu ikiwa bado ni ya darasa la saba.

“Sijawahi kusoma sekondari mahali popote duniani, mtu ambaye haamini anaweza kwenda kule baraza la mitihani kama kuna mtu anaitwa Shigongo amewahi kusoma sekondari mahali popote.

“Nilipopata taarifa zile mimi nikachukua vitabu vyangu nikaenda pale TCU (Tanzania Commission for Universities) nikamkuta Profesa Mwesiga Baregu na nikaweka vitabu vyangu mezani nikamwambia vitabu vyote hivi nimeviandika mimi bila elimu rasmi, ni vitabu vyenye kurasa 500.

“Akashangaa na akaniambia hapa kwetu kuna mfumo unaitwa RPL unaweza ukafanya mtihani wewe, ukipasi unaingia kusoma shahada chuo kikuu.

“Nikaufanya ule mtihani mwaka wa kwanza nikafeli, ilikuwa 2016, mwaka 2017 nilipofanya ule mtihani nikafaulu. Nilipofaulu nikajiunga na Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es Salaam Turdaco (Tumaini University Dar es Salaam College).

“Nikaanza kusoma shahada ya kwanza ya mawasiliano ya umma, kutoka darasa la saba kwenda chuo kikuu. Nimesoma kwa miaka mitatu. Nimemaliza pale nikiwa ‘one of the best students’ mwenye GPA ya 4.8 yaani nilipata B tatu katika muda wote niliosoma shuleni,” anasema Shigongo.

UDSM yamkataa

Shigongo anasema baada ya kumaliza shahada yake ya kwanza alitamani kusoma shahada ya uzamivu, lakini alipopeleka maombi yake Chuo Kikuu cha Dar es Salaam walimtaka apeleke cheti cha kidato cha nne ambacho hakuwa nacho.

Kiuhalisia hana kabisa cheti hicho. Anasema aliwaambia hakuwahi kusoma sekondari wakamkatalia, akaenda TCU wakamwandikia barua kwenda UDSM wakishauri Shigongo aruhusiwe kuendelea na shahada ya pili licha ya kukosa cheti hicho cha kuhitimu kidato cha nne lakini hawakukubali.

“Yaani mimi nataka nisome masters (shahada ya uzamili). Nataka nisome tu nipate elimu halafu wananiambia lete cheti cha form four, sina hicho cheti.

Nikaenda TCU wakaniandikia barua kwamba huyu mtu amefaulu vizuri, nikapeleka UDSM wakasema hawataki,” anaeleza Shigongo jinsi safari yake ya elimu ilivyokwamia UDSM anakotamani kujiunga.

Chanzo: Mwananchi
Nmebahatika kumsikiliza huyu jamaa. by the time alikuja chuoni kwetu so event ilikuwa ya kingereza.

Ana english nzuri kuliko pHD holders wengi ninaowafahamu.
 
Nmebahatika kumsikiliza huyu jamaa. by the time alikuja chuoni kwetu so event ilikuwa ya kingereza.

Ana english nzuri kuliko pHD holders wengi ninaowafahamu.
Inategemea na Phd ya nini! Kama ni ya sayansi hapo sawa lakini siyo huko kwa malingust
 
ANAOGOPA KUPIGA ZERO FORM FOUR SIO MCHEZO

Ataibuka na division zero aabishe hiyo degree ya kununua na kufanyiwa research afanye mtihani wa form four kama kweli kichwani zimo

Aende kujisajili vituo vya private afanye tuone
Huo mfumo hauwezi ndiyo maana la saba alifeli, Mfumo wa msingi na secondary unapimwa kwa kukariri matakataka mengi sana ambayo kwake siyo kipaumbele,
Anaweza kurudi huko bado watataka kumdahili kwa matokeo ya la saba ambayo hana, alifeli!

Pia hata wakimchukua QT atajikuta anafauli English na kiswahili halafu masomo mengine F, F, ,F kiasi cha kuondoka na zero au div 4, ambapo kwa mliman WATAMKATAA.

Diamond ukimpa mtihani wa kuandika anapata sifuri lakini ukimpima kwa kuimba na kucheza anapata A,
Elimu itambue engo za kuwadahili watu kwa vipaji vyao waache kupimia kipimo kimoja ni kuuwa vipaji
 
Back
Top Bottom