Jinsi Eric Shigongo alivyojiunga Chuo Kikuu akiwa na elimu ya msingi

sijawahi kuamini usahihishaji wa mitihani ya form four,,labda huenda huko mbeleni nitakuja kuamini... ila kama mwaka nilobahatika kumaliza mimi matokeo yalitoka mara mbili..( ikumbukwe walisema wamesahihisha upya, je walosahihisha mwanzo walifanyaje??? na matokeo yalinifanya niwe tu disappointed)
 
Kwa hiyo mnataka kumaanisha elimu ya sekondari ni ngumu kuliko ya chuo kikuu?

Kama ndivyo basi kuna tatizo kubwa katika elimu yetu

Kama mtu yeyote akijiunga na chuo kikuu anaweza kusoma na kufaulu, mpaka akahitimu, kwa nini pawepo na ubaguzi wa nani adahiliwe na nani asidahiliwe. Waseme, wewe tu na ada yako. Kama nafasi ipo njoo, jilipie, usome.

Ndio maana mpaka leo Chuo Kikuu Huria kinawekewa mikingamo kuishi kama dhima yake inavyotaka: Huria; kila anayetaka kusoma aje. Siyo kwamba hizo digrii zinatolewa kama sandakarawe.
 
Anarisiti vipi wakati hajawahi kusiti? Asiti kwanza akichemka ndio arisiti
Nilimaanisha akae km private candidate asitake tufanane yeye abaki tuu na cheti chake cha GPA 4 8 wambakishe afundishage hapo hapo
 
Hakuna ombwe yoloyote kweli kwenye kichwa cha shigongo! Kuna mambo mengi sana atakuwa anayakosa, vilevile kuna mambo mengi anayajua ambayo hayapo kwenye mfumo wa vyuo ambayo ni ombwe kwa waliopitia mfumo rasmi.
Sekondari kuna mambo mengi unafindishwa ambayo ndio yanajenga utambuzi na ufahamu wa dunia kwa ujumla wake.
Unakuwa general katika kila kitu.
Hata hivyo chuo kikuu kuna kozi unafanya marudio kama 50% ya O level na A level.

Mfano ukisoma physics kuna topic kama mechanics imebeba vitu vya sekondari na Advance mechanics hio ni ya chuo kikuu.
Wave mechanics ina introduction ya sekondari af baadae ina sogea mbele. Je kwa hizo kozi za art kama mass communication ina marudio yoyote ya sekondari?
Kama sivyo mtu huyo lazima awe na ombwe ya mambo mengi sana.
Vyuo vya teknolojia DIT nk walikuwa na kozi ya mature age entry ambayo mtu wa kitaa anafanya mitihani akifaulu ana soma mwaka mmoja kabla ya kujiunga na digrii.

Hivyo basi TCU wangeweka utaratibu wa refresh course kwa mtu ambae hajapitia sekondari walau miaka 2 af aendelee na kozi.

Katika mfumo wa teknolojia wa sasa watu wanaufahamu mkubwa sana wa mambo mbalimbali japo hawajapitia sekondari na chuo hivyo wapewe nafasi ta kijiendekeza.
SWALI,JE SHIGINGO ANA AJILIKA BILA VYETI VYA SEKONDARI ?
 
Huu utaratibu hata Ulaya upo, mradi uwe na miaka 21 na unajua kusoma na kuandika. Lakini kuna course unaifanya kwa mwaka mmoja kupata credits za kuingia chuo. Katika hiyo course unafundishwa jinsi ya kuandika essay, kupeleka assignments, hesabu na Lugha ya kufundishia katika nchi uliyopo.
Hongera kwake Erick Shigongo.

Hata hivyo, kuna jambo haliko sawasawa, kupata GPA ya 4.8 siyo kitu cha kawaida. Ni wanafunzi wenye uwezo mkubwa sana darasani ndiyo wanafaulu kwa kiwango hicho, Shigongo anasema alikuwa anapata si zaidi ya 25% akiwa shule ya msingi, yeye ni mwanafunzi wa kawaida. Na hii inakinzana sana na matokeo yake ya shahada.
 
huu mfumo wautangeze zaidi hao tcu kuna darasa la7 wengi tu now ukiwaingiza chuo wanatoka na degree nzuri tu kuliko walio kwenye mfumo rasmi..
pia vyuo vyote nchi vinapaswa kujua elimu ni kitu cha muhimu na kama mtu anataka kusoma kujiendeleza zaidi basi wampokee kwa mikono miwili na wamuelimishe ili awe msomi mzuri..

elimu sio dhabi au sio lazima uwe na elimu ya form 4 kama hapa kwetu ndio ujulikane ulisoma isiwe hivyo wanataaluma wa vyuo vikuu mnapaswa kuja na njia tofauti tofauti ili kuhakikisha watu wengi zaidi wanapata fursa ya elimu kama wanauwezo huo.
Inaweza kuchangia watu kukwepa sekondari na kurukia chuo.
Elimu ya chuo kikuu ilibuniwa for Gold people sio kwa kila mtu.
Vocational ndio for iron people.
Bila pyramd dunia haitatawalika.
 
Hongera kwake Erick Shigongo.

Hata hivyo, kuna jambo haliko sawasawa, kupata GPA ya 4.8 siyo kitu cha kawaida. Ni wanafunzi wenye uwezo mkubwa sana darasani ndiyo wanafaulu kwa kiwango hicho, Shigongo anasema alikuwa anapata si zaidi ya 25% akiwa shule ya msingi, yeye ni mwanafunzi wa kawaida. Na hii inakinzana sana na matokeo yake ya shahada.
Ukizingatia lugha ya kufundishia ilimpa shida, kama grammar inampa shida amiwezaje kuandika essays za kumpa GPA 4.8!
 
Kwa hiyo mnataka kumaanisha elimu ya sekondari ni ngumu kuliko ya chuo kikuu?

Kama ndivyo basi kuna tatizo kubwa katika elimu yetu
Ndio! Chuo kikuu una specialize taaluma fulani, unasoma zaidi mambo yanayofanana.
Chuo kikuu unasoma kisha ukifanyia mtihani basi, Chuo kikuu kuna mambo yanajirudia
kutoka msingi na sekondari.
Chuo kikuu kuna course work, assignment, zote zinajazia marks ktk mtihani.
Sekondar mlundikano wa masomo yasio fanana biology,hesabu,jografia ,physics, nk
Sekondari unafanya mtihani wa mwishi baada ya miaka 4.
Sekondari walimu wanabadirika, chuo mwalimu mmoja kwa course.
Sekondari nekta ndio watahini, chuo prof ndio mtahini.
Sekondari hakuna kurudia somo ukifeli
Chuo kuna suplementari.
Wapi kuna ugumu?
 
huu mfumo wautangeze zaidi hao tcu kuna darasa la7 wengi tu now ukiwaingiza chuo wanatoka na degree nzuri tu kuliko walio kwenye mfumo rasmi..
pia vyuo vyote nchi vinapaswa kujua elimu ni kitu cha muhimu na kama mtu anataka kusoma kujiendeleza zaidi basi wampokee kwa mikono miwili na wamuelimishe ili awe msomi mzuri..

elimu sio dhabi au sio lazima uwe na elimu ya form 4 kama hapa kwetu ndio ujulikane ulisoma isiwe hivyo wanataaluma wa vyuo vikuu mnapaswa kuja na njia tofauti tofauti ili kuhakikisha watu wengi zaidi wanapata fursa ya elimu kama wanauwezo huo.
Darasa la Saba umpeleke akasome hayo mambo yao ya journalism Ila vyuo vinavyojitambua haviwezi kumchukua mtu ambae hajapitia mfumo rasmi wa kujiunga na chuo kikuu. Aende udsm akasomee engineering au udaktari wa la Saba hatobi au aende SUA akasomee vet science
 
Nilimaanisha akae km private candidate asitake tufanane yeye abaki tuu na cheti chake cha GPA 4 8 wambakishe afundishage hapo hapo
Mfumo wa kuhakiki vyeti atapenyea wapi? Labda zamani, hio digrii yake ataiweka ndani.
Kwa nini aliamua kupita short cut kwa nini asingekomaa ili awe na cv nzuri, sidhani kama ataweza kupata kazi ya serikali au makampuni makubwa japo sio lengo lake kuajiluwa.
Atabakia tu kusema nina digrii!
 
Back
Top Bottom