SoC01 Jinsi dhana ya mfumo dume inavyowatafuna Wanaume

Stories of Change - 2021 Competition

Mseminary Robert

New Member
Sep 18, 2021
1
0
JINSI DHANA YA MFUMO DUME INAVYOWATAFUNA WANAUME

Wahenga walipata kusema kikulacho kinguoni mwako na hivi ndivyo ninavyoweza kuamua na kuhawilisha tafakuri yangu katika maisha ya mfumo tunaoutamania kuishi kwa kuzingatia kuwa binadamu wote ni sawa na tunapoutafuta usawa wa kijinsia ni kwamba bila ya kuwa na walakini na wala mficho wa kimaana tuutafute usawa katika njia ambayo ni yakumnufaisha kila aliye mwanajamii.

Nawasilisha tafakuri hii juu ya dhana ambayo iliyojengeka hususani katika jamii ya Kiafrika kwamba mwanaume ndio kila kitu katika nyanja zote za kijamii, kiuchumi na kisiasa dhana hii ni dhana ya kishamba ambayo katika kujenga na kusimamia haki za usawa wa kijinsia ni dhana pingamizi katika mapambano haya ambayo wanaume wenyewe wanakuwa ni wahanga wa dhana hii pale wakutanapo na unyanyasaji wa kijinsia ambayo ndio nguzo kuu ya kusimamiwa na kukemewa katika jamiii ambayo tunaipigania ustawi wake. Imezoeleka kuona kwamba vitendo vya ubakaji,udhalilishaji wa kingono, utumikishwaji bila hiyari ni vitu ambavyo vinapaswa kukemewa kwa wanawake tuu pindi inapowasibu. Lakini swali kuu la kujiuliza ni kwa kiasi gani wanaume wanatoka kifua mbele na kuamua kuwasilisha matukio ya uvunjifu wa haki za binadamu na sheria na katiba ya nchi pale ambapo wanapokutana na madhira hususani yanayodhalilisha Utu wa jinsia zao na kuwaondolea thamani?.

Mfano; kutokana na maendeleo makubwa ya Sayansi na Tehama wapo baadhi ya watu ambao wameshindwa kutumia vema maendeleo haya na kufanya maendeleo haya ya Sayansi na Tehama kuwa ni mwiba na shubiri kwa baadhi ya watu na hata kudiriki kujikatisha uhai kutokana tuu na kuvuja kwa baadhi ya picha chafu za ulawiti kwa wanaume, utupu wenye kudhalilisha faragha ya mtu bila kuzingatia athari zinazotokana na madhira haya.

Mfano huu ni sehemu ya madhira mengi ambayo leo hii nimeamua kutoa kama sehemu madhara ya dhana potofu na inayoleta mvunjiko wa ustawi wa jamiii. Kutokana na mfano huu tajwa ni wazi kabisa kasumba inayotokana na dhana ya mfumo dume imekuwa kichocheo kikubwa kwa wanaume kuficha yale wanayokutana nayo kutokana na mfumo wa kimaisha tuliojijenjegea kama wanajamii wa kiafrika kwamba mwanaume ndio kila kitu na ni fedheha kwa mwanume kuonekana hadharani akilalamikia juu ya madhira mbalimbali yanayomsibu.

Imeanza kuonekana ni kawaida katika maisha ya mahusiano kwamba mwanaume anapomkuta mke wake na mwanaume mwingine basi mwanaume Yule anaamua kuchukua sheria mkononi na kufanya vitendo vya ulawiti dhidi ya mwanaume mwenzie kama kutoa adhabu juu ya kile kiitwacho fumanizi. Na pindi wanapotekelza fumanizi hili ni kwa njia ya unyama zaidi ambapo zinazuka na kusaambaa kwa picha hizi chafu katika mitandao ya kijamii ambayo baadhi ya sisi kama wanajamii tumekuwa tukiachangia kwa kiasi kikubwa sana kwa kusambaza picha chafu hizo ambazo kwa ujumla ni kinyume kabisa na utunzaji wa Utu wa mtu.na nikwanini tufikie hatua hiyo kama vipo vyombo vinavyopaswa kusimamia na kutekeleza ufuatiliaji wa haya yote lakini jambo la kushangaza zaidi ni imekuwa mwendelezo wa matamko na rai za viongozi ambazo kwa maoni yangu binafsi sioni utekelezwaji bali kuzidi kushamiri kwa matendo haya yanayodhoofisha Utu wa sauti za wasiosikika ambazo zinamezwa na kufifishwa na dhana ya mfumo dume iliyo potofu ambapo mhusika kwa maana ya mnyanyaswaji au mtendewa ni mwanume mwenyewe. Nini mchango wa mamlaka husika kwa maana madawati ya kijinsia, vyombo vya ulinzi na usalama na wote wanaosimamia sheria na mustakabali wa jamii nzima yenye usawa?. Je kwa vitendo hivi ni sawa kuendelea kutendeka?, na nini hatima ya haya yote?. Nini pia mchango wa jamii ambapo watendewa wa matendo haya ikiwemo wao wenyewe katika kupigania uondoshwaji wa dhana ya mfumo dume ambao unasababisha madhira kwa wanaume wenyewe kwa kutendewa vitendo viovu?. Haya ni maswala ambayo katika zama za sasa yanatakiwa kuangaliwa nakujadiliwa kwa makini lakini kwa bahati mbaya yanatazamwa katika upande mmoja tuu wa kijinsia ya kike ambapo mwanamke anatazamwa kama muhanga mkuu na kusahau kabisa kwamba dunia imekuwa tambara bovu.

Ni wazi pia bila kuuma maneno kwamba katika mustakabali wa usimamiwaji wa malezi nchi nyingi za kiafrika husuani Tanzania malezi kwa vijana yamelegalega kwa kiasikikubwa sana kwa kile kitazamiwacho kama mabadiliko ya kuendena na dunia itakavyo. Matokeo yake ni kushamiri kwa utamaduni mmbovu wa mapenzi ya jinsia moja yaani ushoga ambapo kwa msimamo wanchi nyingi za kiafrika ikiwamo Tanzania ni kosa kisheria lakini kwa kiasi gani mamlaka zimefanya uchunguzi na kuchukua hatua za kuikomboa jamii dhidi ya janga hili dhalimu. Kiuhalisia vitendo hvi vinazidi kushamiri ikiwemo ushoga na mapezi ya jinsia moja kwa ujumla ambapo mchocheo huu unapeleka kusambaa kwa vitendo vya ulawiti na kuzidi kuongezeka kwa unyanyasaji dhidi ya wanaume kwa kiasi kikubwa ambapo ni wanaume kwa wanaume wenyenye ndio wanafanyiana, jamii ipo kimya kana kwamba jambo hili ni sawa kwa kuwa ahakuna aliyejitolea muhanga wa kulizungumzia. Haya yote yanapaswa kutupa Tahadhari juu ya kuzingatia kufuatilia kwa ukaribu juu ya malezi ya vijana hususani vijana wa kiume nadiriki kusema kwamba katika dunia ya sasa MTOTO WA KIUME ANAPASWA KUCHUNGWA ZAIDI KATIKA MALEZI ZAIDI YA MTOTOWA KIKE (nipo tayari kukosolewa kwa sentensi hii) kwani vitendo vya ulawiti, na kuingiliana kinyume cha maumbile (GUYSIM) ,(LESBIANISM) imekuwa ni kubwa sana hususani katika mashule( pedophilia) na maeneo ambayo watoto na vijana wanaishi.

Kila mmoja wa wanajamii achukulie swala hili kama sio swala la kubezwa au matukio ya unyanyaswaji kwa naume ni machache bali ni vitu ambavyo vinachipuklia kwa kasi sana na nivile hakuna wakuvisemea na wanaume wenyewe wamekuwa hawana mwamko wa kujitokeza na kujisemea kutokana na kile kitwacho kasumba zoelefu ya mfumo dume ambao unatupumbaza kwa kuficha masuala yanayo takiwa kukemewa na kufanyiwa kazi kwa mustakabali wa kujenga jamii zetu,Tanzania yetu na Afrika yetu kwa ujumla

Mjumuisho wa haya yote tunao wajibu wa kila mwanajamii anayetambua thamani na mwenendo wa maadili ya kiafrika kusiamama kidete na kuliongelea swala hili kwa uwazi ikiwemo kupata ushirikiano kutoka kwa watendewa wa masuala haya ambayo ni wanaume wenyewe kuamua kutoka nje ya mfumo tulivu utokanao na dhana ya mfumo dume na kuamua kuweka wazi kwamba mfumo dume ni chanzo cha haya yote ambayo ni chagizo la kuendelea kwa mmomomyoko wa maadili na kuendelea kwa vitendo viovu ambavyo havina tija katika wakati wa sasa ambao ni zama endelevu za mchocheo wa sayansi na tehama ambapo binadamu wote wanahaki ya kutendewa kwa usawa bila ya kuathiri mila zetu na tamaduni zetu za Kiafrika.
MAKALA HII IMEANDALIWA NA ROBERT BEATUS
MSEMINARY KUTOKA TAASISI YA FALSAFA YA SHIRIKA LA ROHO MTAKATIFU
NJIRO -ARUSHA,TANZANIA
 
Back
Top Bottom