Jinsi counter wa baa alivyoibiwa pesa

Jinsi counter wa baa alivyoibiwa pesa

Una 'save' jina boss? Hapo lazima ulie.

Alitakiwa asave kwa jina lake huyo mmiliki.
Tapeli akikuamulia atakutapeli tu. Nilishawahi kukutana na kisha cha hivi miaka kama mitano iliyopita nikiwa kwenye mtandao fulani. Yeye alifika dukani akadai ana shida na bosi apewe namba, akajidai kupiga akadai simu haina salio anaomba ampigie kwenye simu ya huyo mfanyakazi ndipo alipoangalia boss ameseviwa vipi akatoa namba ya boss akaweka yake na kuondoka.
 
Acha kubadili story,umedai yule tapeli alifanya kubadili namba kwenye jina liloseviwa "Boss" na kwakuwa Counter asubuhi alipopokea simu na hatimaye kutakiwa kutuma pesa ya mauzo yeye alikwenda kwa wakala na kumpatia pesa na kumtajia namba za "Boss" na wakala akatuma.
Ndio tunauliza inamaana wakala hakuuliza jina litakalotokea? Sasa unasema Counter alitaja jina,je jina lilotokea ni la Boss halisi au Boss tapeli na kama lilitokea jina la Boss tapeli ilikuwaje Counter hakushtuka kwamba jina lilokuja sio la Boss wake?
Brother ukiwa muongo unahitaji kuwa na kumbukumbu.
wewe hujaelewa soma kwa utulivu , kuna kitu alikiandika bila ufafanuz , so wale slow learners inawachukua muda kuelewa
 
Story yako halisi ni hiyo:
ndege JOHN said:
Alienda mtu kunywa pombe ikumbukwe sio mteja wa pale hafahamiki. Akiendelea kunywa akaanza kumuomba counter amuazime simu ili mpigie mtu amletee hela aendelee kunywa mdada wa counter katika utetezi wake anadai Mara ya kwanza alimnyima kwa madai simu haina salio jamaa akaendelea kusihi apewe tu amtumie meseji.

Haifahamiki Kama ni uchawi ulitumika au sayansi ya kumnyenga mtu kwa kumpa offer za bia ila dakika ya mwisho dada alimpatia simu na jamaa bila kupoteza muda akabadilisha namba ya simu iliyoandika the boss yeye akaeidit ikawa namba yake...za boss Tena zilikuwa Kama tatu akazibadilisha zote akamrudishia simu.wakaendelea kumwagilia moyo..

Asubuhi kufika meseji inaingia ikimtaka amwambie mauzo ya Jana kapata shingapi dada akastaajabu kwanini Leo iwe hivi wakati boss hanaga kawaida ya kuulizia mahesabu huwa anakuja mwenyewe kuyafuatilia Basi kwa Kuwa boss NI boss akaambiwa ipo kiasi fulani laki tano..jamaa(boss) akamuamrisha aende kwa wakali atume fasta pesa ili anunue vinywaji kwa Bei rahisi kwani Kuna mtu anataka afunge bar yake pesa ikatumwa maelezo baadae yanakuja kuwa mengi Ila ndo tayari kesi ya utapeli imeshatokea.

Wale wenye biashara waambieni wanaowauzia wawe makini kuzoeana na mtu haraka maisha ya Sasa sio ya kumsaidia mtu simu yako usimuazime kabisa usije kupata shida ya matukio ya kihalifu.
lengo la jamaa ni kuelimishana na sio kujionesha mjanja
 
Hii ni kamba..
mswahili akimaliza ka degree kake ka ualimu bas anahis kila kitu anakijua , kitu kipya kwake ni kamba , hili ttzo tunalo waswahili ndio maana nchi haipig hatua
 
Hapa kuna jambo...
Ukiwenda kwa wakala uwezi tuma ela lazima atakwambia jina ni nani...
tayari kwenye msg boss amekupa namba ya kuwekea pesa na jina ...kwa kutokuwa na mawasiliano mazuri na tajiri dada akashidwa kuhoji kwann namba nyingine na sio yako kama unavyo juwa za hawa mafamba maswali mawili ashakutukania mpaka nyanya ya nyanya yako.....
 
mi nililizwa kwa mfumo huu kwenye laini ya wakala kosa kumpa mteja smu aweke namba mwenyewe akasave namba yake kweny hiyo simu M PESA alafu akasepa.
Badae kidogo akaja mdingi mwingine anataka kutoa 300000 nikamwambia toa kumbe akafoward msg iliyo editiwa kimambo kwenye ile namba iliyokwisha seviwa kwenye simu yangu mbona nikajaa powa tu nikapeana bingo mzee akatembea nikaja kushtuka badae mtu mwingine alipotoa hela nikaona mbona pesa haijaongezeka kwenye account katika kujitete nikaja kugundua hii ni ngozi nimeshapakaliwa mafuta..
 
Mwingine kapigwa, anakunywa na lidemu bar halijui linaazima lipige simu, lienda pembeni kidogo linasepa na simu, dk 5 badae haipatikan
 
Mdada anamwambia boss amkate 200000 kila mwezi ambakishie 50000 Sasa sijajua itaishiaje hi kesi maana kesho wote na wahudumu wengine wanaitwa polisi wakatoe maelezo...ndo hapo nikapata nafasi pia ya kujua mshahara wa counter kumbe NI laki mbili na nusu
..me Nilikuwa najuaga labda laki moja tu
Inategemea na mauzo ya bar
 
Acha kubadili story,umedai yule tapeli alifanya kubadili namba kwenye jina liloseviwa "Boss" na kwakuwa Counter asubuhi alipopokea simu na hatimaye kutakiwa kutuma pesa ya mauzo yeye alikwenda kwa wakala na kumpatia pesa na kumtajia namba za "Boss" na wakala akatuma.
Ndio tunauliza inamaana wakala hakuuliza jina litakalotokea? Sasa unasema Counter alitaja jina,je jina lilotokea ni la Boss halisi au Boss tapeli na kama lilitokea jina la Boss tapeli ilikuwaje Counter hakushtuka kwamba jina lilokuja sio la Boss wake?
Brother ukiwa muongo unahitaji kuwa na kumbukumbu.
Namba nyingine tofaut na namba ya boss aliyoedit
 
Yqni nyinyi wawili..he u kaeni vizuri msome usie na mtafakali,watu kama nyinyi ndo mnapigwa sana ,mang'ombe
 
Back
Top Bottom