Jinsi counter wa baa alivyoibiwa pesa

Jinsi counter wa baa alivyoibiwa pesa

Mwizi ambaye angalau anatumia creativity unaweza ukamtafuta ukamuongezea hata elfu 50 ya ubunifu ila ukamwambia aache mwisho wa siku the Chickens will come home to Roost
 
Una 'save' jina boss? Hapo lazima ulie.

Alitakiwa asave kwa jina lake huyo mmiliki.
Mimi baada ya kupigiwa simu na kampuni ya BRANCH na wakampigia baba angu na mama,walikuwa wananidai pesa yao toka siku hyo nilibadilisha utaratibu wa kusave majina ya wazazi wangu naandika majina yao na siweki kabisa mama au baba
 
Alikosea kutompigia simu bosi wake ili kuhakiki kile alichoambiwa.
Angempigia kwa namba gani wakati namba zishabadilishwa na Kuwa za jambazi na kila alilopiga simu inakata anaambiwa atume meseji yupo kwenye kelele
 
Hapa umetutia Kamba. Aina ya huo utapeli inaweza ikawa kweli upo, ila kusema Counter wa Bar au Muhudumu wa Bar analipwa laki mbili na nusu(250,000/=) huo ni uongo.

Kumbuka vinywaji kama bia, soda, some spirit vina faida ndogo sana. Sasa Boss anatoa wapi jeuri ya kulipa 250k kwa mwezi. Na hapo bado kodi ya jengi au frame hajalipa, umeme kwakuwa mafriji yanakula umeme unamuhusu na vitu vinginevingine.
Hivi mnakunywa hata pombe kweli? Au pombe mnakunywa kwenye vibar mshenzi vichochoroni huka
 
Alienda mtu kunywa pombe ikumbukwe sio mteja wa pale hafahamiki. Akiendelea kunywa akaanza kumuomba counter amuazime simu ili mpigie mtu amletee hela aendelee kunywa mdada wa counter katika utetezi wake anadai Mara ya kwanza alimnyima kwa madai simu haina salio jamaa akaendelea kusihi apewe tu amtumie meseji.

Haifahamiki Kama ni uchawi ulitumika au sayansi ya kumnyenga mtu kwa kumpa offer za bia ila dakika ya mwisho dada alimpatia simu na jamaa bila kupoteza muda akabadilisha namba ya simu iliyoandika the boss yeye akaeidit ikawa namba yake za boss. Tena zilikuwa kama tatu akazibadilisha zote akamrudishia simu. Wakaendelea kumwagilia moyo.

Asubuhi kufika meseji inaingia ikimtaka amwambie mauzo ya jana kapata shingapi dada akastaajabu kwanini leo iwe hivi wakati bosi hanaga kawaida ya kuulizia mahesabu huwa anakuja mwenyewe kuyafuatilia. Basi kwa kuwa bosi ni bosi akaambiwa ipo kiasi fulani laki tano.

Jamaa (boss) akamuamrisha aende kwa wakali atume fasta pesa kwenye namba fulani nyingine 07***** jina litakuja fulani fulani ili anunue vinywaji kwa bei rahisi kwani Kuna mtu anataka afunge bar yake pesa ikatumwa maelezo baadae yanakuja kuwa mengi Ila ndo tayari kesi ya utapeli imeshatokea.

Wale wenye biashara waambieni wanaowauzia wawe makini kuzoeana na mtu haraka maisha ya Sasa sio ya kumsaidia mtu simu yako usimuazime kabisa usije kupata shida ya matukio ya kihalifu.
Ila inataka rehema kuepuka kutapeliwa maishani. Unaweza ruka mikuki mingi sana afu ukaishia kutapeliwa hata uzeeni. Kila mtu ana weak spot ambayo tapeli akiitumia anafanikisha wizi wake
 
Una 'save' jina boss? Hapo lazima ulie.

Alitakiwa asave kwa jina lake huyo mmiliki.
Tapeli hua ana taarifa za kina. Hata jina la boss atakuwa analijua. Anakuja kukutapeli akiwa kesha fanya homework yake
 
Mdada anamwambia boss amkate 200000 kila mwezi ambakishie 50000 Sasa sijajua itaishiaje hi kesi maana kesho wote na wahudumu wengine wanaitwa polisi wakatoe maelezo...ndo hapo nikapata nafasi pia ya kujua mshahara wa counter kumbe NI laki mbili na nusu
..me Nilikuwa najuaga labda laki moja tu
Ukiona hivyo hyo ni bar kubwa, ila mara nyingi huwa si zaidi ya 150,000.
 
Unadhan huyo tapeli alikua hana namba za huyo Boss..? Mtu akitaka kukupiga tukio anafanya research ya kutosha... Hata ungesevu kwa jina la ubatizo, yeye angeingiza namba za huyo boss kujua ameseviwa vipi... All in all ukiona mtu katapeliwa sio kwamba hana akili bali kazidiwa mbinu...
Matapeli wanatapeli wazembe.Ukiwa ni mtu mwenye misingi tako hakuna tapeli anayeweza kukupata.
 
Kuna namba za watu wa karibu sana ambao nikiwagusa tu kwa msg huwa wanatuma hela bila kupiga simu, watu hao huwa sisevu namba zao. Mfano kaka, mama, dada, madogo nk.
Na wao wakigusa tu kwangu kwa msg, nitafanya jitihada hadi nitume.
Kama unaweza kumtumia mtu ela kwa meseji tu iko siku huo uzembe utakugharimu.
 
Back
Top Bottom