Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

EPISODE 46

“A TRUE STORY BY INSIDER MAN”

Nilifanya kurequest usafiri kwaajili ya Mary na mimi nilichukua bajaji kwenda Changanyikeni kulala kwa Prisca.

CONTINUE..

Baada ya kuwasili kwa mama kijacho wangu Prisca nilimkuta hajalala na alikuwa bado yuko seblen anaangalia movie. Niligonga mlango na akatoka kunifungulia, muda huu aliishia kunikumbatia na makisi juu. Pale nje kuna jamaa alikuwa anaanika nguo na aliishia kutukodolea macho kwa wivu.

“Baby I have missed you so much.”

“Remember I promised you nitakuja leo.”

“Pole na Msiba hunny, da Mary umemwacha wapi?”

“Tuliachana ubungo pale yeye karudi home.”

“Kaoge kwanza then uje ule sawa?”

“Twende ukaniogeshe bwana au hutaki kuniogesha Baba Kijacho?”

“Mhh sawa honey tangulia nakuja.”

Baada ya kuoga tulikuwa chumbani tukipiga story na muda huu nilikuwa namchezea Prisca tumbo lake na yeye alikuwa ametulia tulii anasikia raha. Kwa upande mwingine Prisca alikuwa kabadilika sana kimaongezi, ule utoto wake ulikuwa umekwisha, kulikuwa na mabadiliko makubwa sana.

Tuliishia kulala tu maana nilikuwa nimechoka na uchovu sana wa safari.

Asubuhi niliamshwa kwaajili ya breakfast na kwenye simu Iryn, Mary, Muajemi, na Mama J walikuwa wamenipigia simu. Ilibidi nianze kumpigia simu Mama J na niliongea naye mbele ya Prisca huku akisikia.

WIFE: “Baba J Unaendeleaje jana ulisema unarudi mbona hujarudi?”

MIMI: “Wife sorry tulichelewa kutoka then tukapata shida njiani, hivyo tulilala Moro na soon tutaanza safari ya kurudi.”

WIFE: “Ok husband, Iryn amesema leo anaondoka jioni kwenda kwake.”

MIMI: “Sawa! Lakini mwambie asiondoke kwanza, mimi mchana nitakuwa hapo, nitampigia simu soon niongee naye.”

Na wakati naongea na mama J kwa simu Prisca alikuwa akinitizama sana na baada ya kumaliza maongezi akaanza kucheka.

“Honey una masters ya uongo inaonekana hata mimi unanidanganya vingi sana.”

“So ulitaka niseme ukweli kwamba niko kwa mchepuko?”

“Nooo! I like the way ulivyomdanganya na ameridhika kabisa hajawa na maswali tena.”

Na mimi nilikwenda zangu kulala tena maana nilikuwa na uchovu muda huu, ukijumlisha kutoka kule Mbweni mpaka Tabora nilikuwa nakosa muda wa kulala kabisa.

Mchana muda wa saa 9 nilipigiwa simu na mama wa2 na akanambia jioni atakuja kwangu kunitembelea, pia alisema ana mazungumzo na mimi kuna jambo anataka kunishirikisha.

Muda huu ilibidi nimuage Prisca na nikaondoka kurudi home Mbezi. Nilitumia bodaboda kurudi nyumbani na ilinichukua dakika 20 kufika pale, na baada ya kushuka na kuingia ndani mama J alikuja akani hug na Iryn akafuatia.

Muda huu tulitumia kuongea kuhusu habari za msiba za kule Tabora na baada ya kumaliza maongezi ya msiba nilimpa mama J taarifa za ujio wa mgeni.

MAMA J: “Vipi kuhusu Iryn tulikuwa tunapanga tuondoke ukirudi wewe.”

MIMI: “Iryn kwanini tusiondoke kesho mummy nikusaidie kutoa na vitu kule Kijitonyama?”

IRYN: “No problem Insider usiwe na wasiwasi, mama J tutakwenda kesho tuandae dina kwaajili ya wageni baadae.”

Saa 12 jioni mama wa2 alikuja nyumbani pamoja na mwanae Rachel lakini nilishangaa kuona haja ongozana na Pili.

“Mama mkwe karibu ndani hapa ndo nyumbani jisikie upo kwako.”

“Ahsante sana mkwe ukweli nimefurahi sana kupajua pia pole sana kwa msiba jamani.”

“Ahsante sana kwakweli Mzee tulijuana kwa muda mfupi na ametangulia mbele za haki, alikuwa kama mzee kwangu. Vipi mke wangu Pili yuko wapi? mbona hujaja nae?.”

“Pili amekwenda Mwanza kumsalimia Baba yake.”

“Ohh! habari njema hizi ni haki yake.”

Kipindi niko msibani mama wa2 alinijulisha kuwa Pili anafunga shule, hivyo nikamchukue lakini nilishindwa sababu ya kuwa busy na msiba.

Nilitumia muda huu kufanya utambulisho na nilianza na mama J ambaye nilimtambulisha kama mke wangu na nilimtambulisha Iryn kama ndugu yangu. Na baada ya hapo nilimtambulisha mama wa2 kama ndugu yangu wa karibu sana, na muda huu alikuwa amemshika Junior akimchezea.

“Insider una mtoto mzuri hivi napendaje watoto wa kiume mimi, yaani so handsome kama Baba yake.”

“Mama naomba nimshike mtoto na mimi please” ni sauti ya Rachel alikuwa akimwomba mama yake. Na mama wa2 alimpa mtoto Rachel ili amshike.

Saa 1 usiku tulipata dina ya pamoja na baada ya dina akina mama J waliondoka wote pale nyumbani. Waliaga wanatoka out, hivyo nikabaki mimi na mama wa2 pale nyumbani.

Baada ya kuondoka tulikuwa free kufanya maongezi pale kwa kujiachia,

“Insider ukweli nimefurahi sana kufika kwako na kuijua familia yako. Huyo dada umesema ni ndugu yako lakini anaonekana kama sio Mtanzania she’s so beautiful kuna watu walipendelewa kuumbwa.”

“Wazazi wake sio Watanzania kwa kuzaliwa ila wameishi hapa. Nambie ulisema una mazungumzo mengine na mimi.”

“Insider nashukuru Mungu nimepandishwa cheo pale ofisini na sasa nitakwenda HQ na mshahara nitalipwa mara ya 3 ya huu ninaolipwa sasa.”

“Jamani nimefurahi sana kusikia hivyo mama mkwe, mafanikio yako ni yangu. Hongera sana na Mungu akutangulie. Unategemea kuanza lini majukumu mapya?.”

“Mwezi ujao nafikiri, na vipi kuhusu suala lako la kazi nitumie CV yako au hutaki kufanya kazi Bank?”

“Napenda ila kuna deal Marehemu alisema ananitafutia so baada ya kifo chake kuna mtu amemwachia maagizo ambaye tutaonana akirudi kutoka Tabora. Acha nimsikilize afu nitakupa mrejesho mama mkwe.”

“Usiwe na wasiwasi anytime utanambia ili tufanye maarifa.”

“Vipi ni connection au uchapakazi wako tu?”

“Insider ukweli Baba Rachel kanisaidia kupanda cheo.”

“Ndo raha hii ya kuzaa na wakubwa.”

“Hahahah Insider umeanza. Nafikiri tukukimbie sasa ili nikajiandae na ratiba za kesho.”

“Acha niwapeleke ili na mimi niende kule msibani nikaangalie na maendeleo maana toka nirudi jana sijakwenda kabisa.”

Tuliondoka na mama wa2 na nilitumia ile Dualis maana Ist walikuwa wameondoka nayo akina Iryn. Na muda huu nilifanya kuwasiliana na Mary nikamwambia nampitia baada ya dakika 20 ajiandae ili twende Mbweni.

Baada ya kuingia kwa gari Mama wa2 alikuwa akishangaa sana kuona na gari nyingine.

“Insider hii ni gari mpya kabisa umenunua?”

“Hapana hii ni ya Mzee alinununua kwaajili ya mchepuko wake, alisema nisimpe mpaka awe vizuri barabarani, sasa ndo kimetokea kifo chake.”

“Aisee sijui huyo dada anahali gani kwasasa, inaonekana Mzee alikuamini sana, kukuachia gari sio kitu kidogo ujue.”

“Unachoongea ni sahihi Mama mkwe.”

Tulitumia dakika 10 kuwasili pale kwake na niliwashusha na wakati tunaagana Rachel alikuwa akiongea na mimi.

RACHEL: “Uncle Insider utakuwa unakuja kunichukua ili nikacheze na Junior sindio?”

MIMI: “Usijali Rachel nitakuwa nakuja weekend sawa?”

MAMA WA2: “Insider kafunga shule huyu hata katikati ya week sio mbaya.”

MIMI: “Sawa haina shida nitakuwa nakuja kukuchua, wewe ukim-miss nipigie simu tu.”

RACHEL: “Ok byee Uncle.” Na tuliishia kugonga mikono.

Tuliachana pale na mimi nilikwenda kumchukua Mary pale kwao na tukaanza safari ya kwenda Mbweni. Kwa upande mwingine Mary alishangaa kuona nina gari mpya na mimi sikutaka kumwambia chochote.

“Kumbe siku ile usiku ni wewe uliyemshusha Prisca pale home na hii hii gari.”

“Hahahaa ni mimi ila sikutaka kukupa salamu ile siku maana niliona muda umekwenda.”

“Tabia mbaya hiyo Insider unajua nilimfikiria vibaya sana Prisca ile siku, hata yeye hakutaka kusema ni wewe.”

Tuliwasili pale Mbweni na nilimkuta yule mlinzi pale getini akiendelea na majukumu yake. Niliamua ku-park gari nje kabisa ya geti, sikutaka kuingia nayo ndani.

Tuliingia ndani na nikawakuta baadhi ya ndugu wa Jane na marafiki zake baadhi walikuwepo na wengine walikuwa wanakuja kutoa pole. Pis Kuna baadhi ya ndugu walikuwa wameondoka tayari.

Tuliwasalimia wote na mama yake alikuwa pale sebleni nikamsogelea karibu. Nilisalimiana na mama na aliulizia mazishi yalikwendaje kule Tabora. Kwa upande mwingine mama alikuwa na wasiwasi sana kuhusu mwanae kukosa stahiki zake, maana Jane hakuwa mke halali wa ndoa.

Nilimtoa hofu mama muda huu na nikamwambia Mzee alisoma waraka kuwatambulisha wake zake wote hata Jane ametambulika kama mke wake. Na imani atapata urithi maana Mzee aliandika ameacha barua ya mirathi.

“Na wasiwasi mwanangu wasije mnyang’anya na hii nyumba, Jane akaanza kutaabika.”

“Hamna mama Mzee alisema hii nyumba kamjengea Jane, nafikiri hata hati itakuwa na Jina la Jane naamini hivyo.”

Kwa upande mwingine mama yake alinishukuru sana kwa yote niliyoyafanya pale na kujitoa kwangu kipindi chote cha msiba. Na sisi hatukaa sana bali tuliwaaga tukaondoka pale Mbweni na tulikwenda mpaka “The Wave” ya kule chini Whitesand.

Baada ya kuwasili pale, tuliingia ndani na tulitafuta angle nzuri tukakaa. Tuliagiza wine ambayo tulifanya kushara na Mary na muda huu tulikuwa tukipiga story mbalimbali.

“Insider umejitoa sana kwenye huu msiba Mungu atakulipa hata Mzee huko aliko atakuwa anaona must be proud of you.”

“Hata wewe pia Mary ulijitoa sana sikutegemea ungenipa kampani namna ile, ulijitoa kuliko hata ndugu zake Jane.”

“Insider, unajua Mzee japo nilimwona kwa mara 2, ila kifo chake kilinishtua sana.”

“Unajua mimi mpaka sasa siamini amini kama kweli Mzee ametutoka naona kama ndoto. Nikikumbuka wakati tunaongea na alikuwa akinisisitiza sana kumwangalia Jane.”

“Ni kama alikuwa anaona kifo chake inabidi uwe bega kwa bega na Jane, nafikiri Mzee alikupa Task hakutaka kukwambia ukweli.”

“Hata mimi nahisi hivyo, Mzee alinipa task Mungu asaidie Jane ajifungue salama. Nafikiri hii ndo task nayotakiwa kuhakikisha inafanikiwa.”

“Hiyo ndo point hata hivyo Insider unabahati sana ya kukutana na watu wenye hadhi tukianza na Mzee sikutegemea angekuwa na ukwasi wa namna ile.“

“Unajua sikuwahi kumwuliza Mzee kuhusu personal life yake hata siku moja, ila nilipanga this time angerudi ningemwuliza maana alisema angenitafutia kazi.”

“Nilisikia unaongea na Mzee Juma naamini atakusaidia kama kweli alipewa maagizo kutoka kwa mzee na jinsi ulivyojitoa kwenye huu msiba naamini atafanya jambo.”

“Anyway acha tuone Mzee pekee ndo angelichukulia hili suala kwa uzito sana maana kuna sehemu nilikuwa namgusa, how about Mzee Juma??”

“Ni kweli unayosema ila siamini kama anaweza kukuchinjia baharini.”

Tulitumia kama masaa 2 pale “The wave” na tuliamua kuondoka kwenda kulala. Na muda huu niliwaza kumpa pesa kidogo Mary maana nilijua lazima kafulia.

Kipindi niko msibani Tabora niliwasiliana na Muajemi na nilimpa taarifa za msiba na alinitumia milion 1 ya pole. Pia Nilimuahidi nikirudi Dar jumamosi ningemcheki maana alisema anataka tuongee kuhusu sakata la Iryn.

Hivyo, nilikuwa na million 1 kutoka kwa Muajemi, laki 5 kutoka kwa Iryn na laki 3 alizonipa Mzee Juma. Jumla nilikuwa na 1,800,000/= na sikutumia hata cent kwenye hizi pesa.

Nilimpeleka Mary mpaka kwao na wakati tuko nje getini tuliendelea kupiga story na Mary mle ndani ya gari. Baada ya nusu saa hivi tuliagana na nilimpa laki 3 kama shukrani yangu kwake.

******
Jumatatu asubuhi niliondoka pamoja na Iryn kwenda kwenye apartment yake mpya. Na toka alipie alikuwa hajawai kwenda tena maeneo yale. Baada ya kuwasili pale getini kulikuwa na mlinzi, hivyo tukafanya utambulisho kwanza.

“Kaka mimi naitwa Iryn mpangaji mpya niko “Block A” floor ya 1.”

“Karibu sana Bossy na samahani kwa usumbufu.”

“Usijali ni kazi yako hakuna ulichokosea.”

Muda huu tulifunguliwa geti na tulikwenda moja kwa moja mpaka usawa wa apartment ya Iryn ndo nikapark gari.

Baada ya kuingia ndani ya apartment Iryn alikuwa anaangalia vitu vya kununua. Baada ya hapo tuliondoka kwenda Kijitonyama kwanza, kwenda kuchukua vitu vyake.

Baada ya kuwasili pale Kijitonyama tuliingia ndani na Iryn aliingia chumbani kuanza kupanga nguo na kuweka kwenye bag. Mimi muda huu nilikuwa nafungua Home thieta maana ilikuwa inaondoka na baada ya kumaliza nilikwenda kumsaidia kutoa vitu vya chumbani na kupeleka kwenye gari.

Nilifungua drow na nikaanza kutoa vitu vya mle ndani na nilivyofungua drow ambalo lina simu nikaanza kuzitoa na kuzipanga.

IRYN: “Insider hizo simu ulisema utanitafutia mteja uliishia wapi?”

MIMI: “Nilisahau ila leo kuna mtu nitampigia naona ziko 10 idadi ni sawa?”

IRYN: “Ni sawa moja kuna dada nilimpa pale Sinza niliona peke yake hana simu inayoeleweka. Na wewe unaweza kuchukua simu moja hapo utakayoipenda.”

MIMI: “Thank you Bossy, mimi nina chukua hii 13 Pro.”

IRYN: “Kwanini sasa? Chukua hio Pro Max.”

MIMI: “Napenda simu ndogo hiyo Promax hapana.”

IRYN: “Sawa ni wewe tu mimi nimekupa uchague unayotaka kama umeipenda Pro haina shida.”

MIMI: “Na hizi zilizobaki niuzaje?”

IRYN: “Uza hizo 13 Pro Max na hiyo Samsung, hizo 13 Pro ziweke kuna dada tutawapa Saloon. Kwa hizo simu 7 zilizobaki niletee milion 14 cash, ukiuza zaidi ya hapo ni yako.”

MIMI: “Sawa afu nilikuwa nawazo, kwanini ile Saloon ya Sinza isifungwe? Wateja wa pale tukawa direct Mikocheni? Maana nimefanya Research nimegundua wateja wengi hawatoki Sinza pale.”

IRYN: “Wazo lako ni zuri sana nafikiri mwisho wa mwezi huu tuta achana na Sinza. Hata pale Mikocheni tunahama kuna ofisi kubwa niliipata tutaweza hata kupata sehemu ya storage.”

MIMI: “Ooh! hukuwahi kunishirikisha hili kabisa ulianza lini Process?”

IRYN: “Ni muda toka kipindi kile nime-kusimamisha, pia naomba week hii utaorganize kikao kila kitu utapanga wewe. Mimi utanipa ratiba, location na cost zote tutakazo incur. Nataka kuongea na wafanyakazi wangu wote mpaka wa Masaki.”

MIMI: “Sawa haina shida, nitalifanyia kazi then nitakupa mrejesho mapema.”

Baada ya hapo tuliondoka pale Kijitonyama na tulikwenda Mlimani City ambapo alikuwa anafanya shopping ya kununua vitu vya ndani pamoja na chakula. Na baada ya kumaliza shopping tuliondoka na kurudi Kawe kwenye apartment mpya.

Nilishinda pale na Iryn na siku hii nilimpigia Ugali na yeye alikuwa anapika mboga. Na baada ya lunch nilimwaga nakwenda Mbweni kwaajili ya kuangalia maendeleo ya pale.

Nilipitia pale Jambo Supermarket Bahari Beach nikanunua baadhi ya mazaga ya jikoni ya kupika na nilinunua mchele, unga, Nyama ya ng’ombe na Kuku. Nilihisi huenda wakawa wameishiwa vitu vya kupika hivyo nilijiongeza tu kwa upande wangu.

Baada ya kuwasili pale na mazaga dada alikuja kunipokea na nilimsaidia kubeba mpaka jikoni. Nilikuwa nimefaulu ule mtihani maana walikuwa wameishiwa vitu ndani.

“Kaka umejuaje kama vitu vilikuwa vimeisha ndani maana nilikuwa nawaza kukupigia lakini mama akasema niache utakuja.”

“Ungepiga tu hata msiwe na wasiwasi kwa siku nyingine.”

Na muda huu nilikwenda Seblen kuonana na mama na nilimsalimia pia pale kulikuwa na ndugu wengine wa Jane. Mpaka leo walikuwa watu watano tu wamebaki pale kwa Jane.

MAMA: “Mwanangu huyu ni mdogo wake Jane anaitwa Vicky ndo bint yangu wa mwisho. Sikuwai kukutambulisha kipindi kile cha msiba na kila ukija anakuwa ndani.”

MIMI: “Hongera mama naona pia wamefanana sana na Jane, nilikuwa namwona ila nilihisi ni mdogo wake.”

Na mudaa huu nilisalimiana na Vicky, pia alikuwa anasoma chuo hapa Dar na alikuwa 1st year.

VICKY: “Ahsante kaka tunashukuru kwa yote na kujitolea kwako kwenye familia yetu.”

MIMI: “Msijali tuko Pamoja sana ndugu zangu.”

MAMA: “Umewasiliana na Jane? na maendeleo yake yapoje? Mimi simpati kwa simu.”

MIMI: “Nimeongea naye asubuhi na weekend hii ataweza kurudi. Wakati naongea naye alikuwa kidogo kachangamka tuendelee kumwombea.”

MAMA: “Ahsante sana kidogo na amani.”

Na muda huu simu yangu alianza kuita na ile kucheki alikuwa ni Muajemi akipiga na mimi nilipokea simu yake na tukaanza mazungumzo.

Muajemi alikuwa anaomba tuonane jioni ya saa 11 ontime na mimi nilimkubalia sikuwa na pingamizi lolote.

Nilishinda pale Mbweni mpaka saa 10 jioni na niliaga nikaondoka maeneo yale. Njiani nilifanya mawasiliano na Muajemi na akanambia tukutane pale Namanga.

Niliendesha gari mpaka Namanga na mapema nilikuwa nimefika tayari. Baada ya kufika maeneo yale nilimpigia simu na akaniambia yuko showroom ambayo ipo opposite na mataa ya Namanga.

Nilidrive mpaka pale Showroom na nikapark gari nje nikaingia ndani. Baada ya kuingia ndani niliweza kuonana na Muajemi na tukasalimiana kwa kugonga tano. Na muda huu tulianza kuongea na alinipa pole ya Msiba na maongezi mengine mengi yaliendelea.

“Bro! sitaki kukupotezea muda ila nina zawadi kwaajili ya Iryn naomba uipeleke kwa niaba yangu.”

“Ni zawadi gani hiyo Bro?”

“Twende nikuoneshe Bro!.”

Tuliongozana na Muajemi na baada ya mwendo wa hatua 10 hivi alinionesha gari kama zawadi ya Iryn. Mbele yangu ilikuwa inaonekana Mercedes Benz kwa nyuma ikisomeka “S-550” something like that. Na colour yake ni rangi ya maziwa “pearl” na ilikuwa inang’aa sana muda huu.

“Nataka umpelekee Iryn hii gari.”


TO BE CONTINUED
Muajemi ni Dugu moja na Kondeboy kabisaa,ye anahonga ndinga kali tu
 
Back
Top Bottom