Kwanini Waafrika tunapenda sana kuwapa watoto wetu majina ya Ulaya, Asia n.k?

Nsibwene

Senior Member
Mar 2, 2017
198
129
Jina ni neno au maneno anayopewa mtu au kitu au hali Fulani

Nataka kujikita kwenye jina tunalopeana watu.

Kwanini Waafrika tunapenda sana kuwapa watoto wetu majina ya Ulaya, Asia n.k., lakini sisi tuna maneno katika lugha za Kiafrika.

Kwanini usumbuke uingie kwenye mtandao na penginepo.

Tanzania tuna lugha nyingi maana tuna maneno ambayo tungetumia kuwapa watoto wetu.

Hatuwi wa maana ati kwa kuitwa Zebedayo au Hasani au Rebecca au Salha nk

Hatuwi wacha Mungu wazuri kwa majina hayo.

Mtu akiishi au akafuata ya huko nje tunamkandia, vipi kuhusu jina mwanao.

Natamami tubadilike, kama wewe ni Mgogo au Mfipa au Mmakua nk tumia neno ambalo unalijua maana take na unalifurahia.

Tuache ushamba wa kupenda tusivyovijua
 
Mimi niona jina zuri kwa lugha yoyote si kosa kinachomata na maana Tu

Mfano
Happy kingereza

Saeida kiarabu

Furaha Kiswahili

Uwe muislam ao mkiristo sababu ata kwa kimakonde,kizigua n.k halina tofauti kimaaana zaidi ya matamshi na lugha
 
Mimi niona jina zuri kwa lugha yoyote si kosa kinachomata na maana Tu

Mfano
Happy kingereza

Saeida kiarabu

Furaha Kiswahili

Uwe muislam ao mkiristo sababu ata kwa kimakonde,kizigua n.k halina tofauti kimaaana zaidi ya matamshi na lugha
Waarabu Na wazungu Na wao wanaita watoto wao Furaha?
 
Siku hizi tumeenda mbele zaidi ya makabila, hadi vifaa vinahusika. Leo tu taarifa ya habari nimeona majina CHEREHANI (Mbunge mteule na KABATI (Padre).
 
Mbona wewe mkuu unavaa chupi, boxer, jeans, suti pensi. Kwenye jina tu ndo unaona. Kwa nini usindie mizizi na mchwa? Kwanini usiishi chini ya mti na mpango? Kwa nini usitembee uchi
Basi kwakuwa wamekuletea boxa umeamua Kuwaiga Na Kuwa shoga?
 
Back
Top Bottom