Kwanini Waafrika tunapenda sana kuwapa watoto wetu majina ya Ulaya, Asia n.k?

Jambo lingine kujiita majina yenu ya asili hakuna ubaya ila kuyaponda ya kidini ni ujinga ulio pea.

Ndiyo maana leo hii unakuta mtu anaitwa "Anthony Edward" lakini ni Muislamu,cha msingi majina yawe na maana ila kaeni mkijua ya kuwa majina mazuri yapo,na hakuna majina mazuri kuzidi ya mitume na waja wema.
Mubarrid upo sahihi kwa majina ya dini kuyatumia haikwepeki . lakini kulidharau jina lako la kilugha na kushobokea jina la Kizungu au Latino ndio ujinga.

Halafu mtu anajiita jina hata haendani nalo kabisa Yaani unakutana na mwanamke eti anaitwa PRISCILLA au CATHERINE, Subiri umuone sasa.

Siku nilikwenda wilaya ya Rombo ndani kabisa sehemu tukaagiza mbege kumbe tuliwahi kidigo, ndipo Mama muuzaji akasema tusubiri MACDONALD aje kuangalia kama ipo vema(mtaalam). Alipokuja yaani nilichoka nikasema mbona kuna majina mazuri tu ya NDENGERIO au KINABO
 
Wengine hawajitambui wanafikiri jina ni dini wakati majina hayo yalikuwepo kabla yake. Wamewaandika watu walipkuwepo

Jina lo lote ni kuzoea kulitamka, Zoea kulitamka jina litakuwa zuri, dini hazina ubaya ila waliloleta walitufanya tusithamini lo lote la kwetu.
Sasa tuna elimu tunajua historia.
Ni kukuza majina yetu mfano Malecela alimpa mtoto wake Mwele, sasa yuko huko na wazungu na pengine wanatamani wawaite watoto wao hivyo
Hujui kuwa anaweza kuwa maarufu na jina lake likavuma. Kaunda wa Zambia alimpa mtoto wake jina la Kambarage kwa sababu ya Nyerere.
Majina yanakuza utamaduni wa mahali. Wengine utamaduni ni Ngoma, mavazi tu. Lugha ni utamaduni Wanaijeria baadhi yao wengi hutumia majina ya kwao
Huwi Mwislamu mzuri kwa kuitwa Husein au Mohamed au huwi Mkristo mzuri kuitwa Petro au Yohana, la sivyo watu wenye majina hayo wangekuwa bora sana.
Hata ukamwita Ronaldo haimfanyi awe mchezaji mzuri .
Tafuta cha kwako kikuze .
 
Mbona wewe mkuu unavaa chupi, boxer, jeans, suti pensi. Kwenye jina tu ndo unaona. Kwa nini usindie mizizi na mchwa? Kwanini usiishi chini ya mti na mpango? Kwa nini usitembee uchi
Ukienda Ulaya ukaitwa Zamoyoni kuna ubaya gani?
Au akili zako zimeganda!!
 
Kiukweli majinaya kibantu hayavutii masikioni.

Si kitu,tuntufye, kokumanyisa, kigwangala, pinda, tundu, kinabo nk.
Kwako tu sio kwa kila mtu. Majina ya kibantu mazuri sna na yapo tofauti kila ukoo una jina lake kama unadhani wazee wetu hawakuwa na akili basi wewe ndio una tatizo.
Majina ya kibantu yanakoneksheni na DNA. Ukiitwa juma , Saidi mpo maelfu diniani hata google inachanganyikiwa .
Ukiitwa mwanamutapa dunia nzima inajua wewe unatokea wapi.
Nyerere ni watu wa msoma tu hakuna nyerere wengine.
Bantu names are very powerful names.
 
Ushamba. Wazungu wakija watakuwa wanashangaa sana. Ni sawa na mtu leo uende ulaya ukute mtu anaitwa Zamoyoni, utashangaa sana.
Kenya kuna wazungu wamejipa majina ya 'kiluo' na wanazungumza lugha hiyo kwa ufasaha kabisa!

Tanzania pia kuna mtaliano anaitwa masanja huko usukumani.

Yule jamaa wa usangu anajiita 'Mwakabwanga'
 
Jina ni neno au maneno anayopewa mtu au kitu au hali Fulani

Nataka kujikita kwenye jina tunalopeana watu.

Kwanini Waafrika tunapenda sana kuwapa watoto wetu majina ya Ulaya, Asia n.k., lakini sisi tuna maneno katika lugha za Kiafrika.

Kwanini usumbuke uingie kwenye mtandao na penginepo.

Tanzania tuna lugha nyingi maana tuna maneno ambayo tungetumia kuwapa watoto wetu.

Hatuwi wa maana ati kwa kuitwa Zebedayo au Hasani au Rebecca au Salha nk

Hatuwi wacha Mungu wazuri kwa majina hayo.

Mtu akiishi au akafuata ya huko nje tunamkandia, vipi kuhusu jina mwanao.

Natamami tubadilike, kama wewe ni Mgogo au Mfipa au Mmakua nk tumia neno ambalo unalijua maana take na unalifurahia.

Tuache ushamba wa kupenda tusivyovijua
Majina ya kiafrika yaambatana na mizimu-miungu ambayo ni chukizo mbele za MUNGU.
 
Kwa cc waisilamu huwezi mpa mtoto jina la kibantu, kichina, kihindi, kikorea, kizungu n.k, hayo itaneni wenyewe. Sisi tunaitana majina ya kiarabu/kiisilamu.

Said
Salim
Abdallah
Abdulkareem
Ali
Aisha
Khadija
Raiya
Kulthum
Amiina
N.k
 
Jambo lingine kujiita majina yenu ya asili hakuna ubaya ila kuyaponda ya kidini ni ujinga ulio pea.

Ndiyo maana leo hii unakuta mtu anaitwa "Anthony Edward" lakini ni Muislamu,cha msingi majina yawe na maana ila kaeni mkijua ya kuwa majina mazuri yapo,na hakuna majina mazuri kuzidi ya mitume na waja wema.
Majina asilimia kubwa ni maneno ya lugha ya mahali; yana maana fulani nzuri au mbaya tokana na yule anayetoa. Mfano jina Messi umaarufu wake ndio uliolikuza jina, kiasi cha kwamba watu wameanza kuwaita mtoto Messi.
Mitume au manabii unaowasema walikuwa majina hayo hata kabla hawajawa nabii au mtume. Mfano Muhammad ni jina la Kiquresh (lugha ya Kiarabu) aliitwa hivyo hata kabala hajawa mtume; au Yesu (jina la Kiyahudi -"Jehoshua") yenye maana nzuri. Majina yalikuwepo hata kabla yao. Maana yangu ubora wa mtu hautokani na jina lake. Watoto wanaoitwa Muhamad tungewakuta wote ni manabii lakini sivyo.
Kutunza lugha zetu pia ni kwa njia za majina.
Wengi wanaobeza maneno mazuri ya lugha zetu ambayo tungetumia kuwapa watoto hata atakapokuwa maarufu watu watayafuata. Usibeze lugha yako. Dini ni nzuri na mimi muumini mzuri wa dini ila naheshimu lugha yangu na kuitumia hata kumwomba huyo Mungu wangu.
 
Kwa cc waisilamu huwezi mpa mtoto jina la kibantu, kichina, kihindi, kikorea, kizungu n.k, hayo itaneni wenyewe. Sisi tunaitana majina ya kiarabu/kiisilamu.

Said
Salim
Abdallah
Abdulkareem
Ali
Aisha
Khadija
Raiya
Kulthum
Amiina
N.k
Haya ni majina ya Kiarabu sio ya Kiislamu, uislamu sio jina ni moyo. Walioleta Uislamu huku kwetu ndio wanaoenzi lugha yao na kuona lugha nyingine haina maana. Mungu wa Kiisamu anasikia Kiarabu tu, hasikii mtu anapoomba kwa lugha nyingine. Sidhani kama ni kweli. Mungu ni watu waote husikia lugha yo yote. Mungu ndiye aliyetupa hizo lugha.
 
Haya ni majina ya Kiarabu sio ya Kiislamu, uislamu sio jina ni moyo. Walioleta Uislamu huku kwetu ndio wanaoenzi lugha yao na kuona lugha nyingine haina maana. Mungu wa Kiisamu anasikia Kiarabu tu, hasikii mtu anapoomba kwa lugha nyingine. Sidhani kama ni kweli. Mungu ni watu waote husikia lugha yo yote. Mungu ndiye aliyetupa hizo lugha.

Haya wewe unaejua nipatie majina ya kiislamu
 
Back
Top Bottom