Majina yetu huathiri haiba zetu kwa namna za ajabu kabisa... Unapomchagulia mtoto jina hakikisha unajua vema asili yake hasi na chanya zake na mustakabali wake... Kwani hujawahi kusikia mtu akiambiwa karithi jina na tabia!?
Kuna kinywaji kikali duniani maarufu sana kinaitwa John walker... Inasemekana jina hilo ndio la huyo mvumbuzi ambaye alipenda kutembea mji mmoja hadi mwingine kwa miguu ama kwa gari.. Vitu vya kupaa alipanda kwa lazima sana
JW ni kinywaji kikali kwakweli na ukifanya maskhara unayabanika maini figo na bandama yako bila kupenda! Lakini unajua kiboko ya kilevi kikali ni nini!?
Chuma hakiathiriwi na pombe kali... Chuma adui yake mkuu ni maji... Hapo kutu ni fasta na hiki ndio kiama chake.. Ukiikutanisha pombe kali na chuma... Ni kama kukipiga msasa... Pombe itasizi chuma kitang'aa
Chuma kina majina mbalimbali kutokana na matumizi yake.. Kuna mataruma, kuna flat bar kuna waya kuna Nondo nknk...
Nondo inaweza kuwa na matumizi mengi kwa wakati mmoja lakini kubwa ni ujenzi... Msingi imara wa nguzo kuta au viunganishi kwenye magorofa madaraja na ujenzi mwingine... Nondo hutumika sana... Kwahiyo kiroho jina la Nondo ni kuleta uimara kiunganishi na kushikamanisha..... Ukitaka kuiweza nondo itafutie moto au maji.. Sio tindikali..
Nimemaliza... Mlale salama....