Jina la mwanangu limezua vita ya kifamilia

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
34,679
40,933
Wakuu nipo njia panda ya kuchagua upande. Haya mambo yasikie tu kwa wengine.

Wakati anazaliwa mwanangu huyu mama yake mzazi mwenzangu ndio alisimamia jambo hili ukizingatia kuwa hiyo ndio ilikua taaluma yake.

Sasa jamaa alipozaliwa tu huyu mama akampa jina dogo tuseme jina Y maana ndio alikua mtu wa kwanza kumbeba na kumhudumia wakati mama wa mtoto bado akiwa katika usingizi.

Sasa baada ya hapo tukakaa na Mzazi mwenzangu kujadili official name ya dogo. Tukakubaliana Jina X hili likashika kasi na likakubalika kwetu.

Sasa tunataka kupata cheti cha kuzaliwa. Tangazo la Kuzaliwa linamtambua dogo kwa jina Y ila ipo option ya kubadili.

Sasa upande wangu wakagundua kuwa kuna jina jingine la dogo analotambulika ambalo lipo katika tangazo la kuzaliwa.

Binafsi mimi sina matatizo na jina lolote so long as huyu dogo anabeba DNA yangu either mimi ndio nimempa au mtu mwingine yeyote.

Historically hata mimi mzee wangu hakunipa jina langu familia nzima walipewa karatasi kura nyingi zikaangukia jina langu. So nimepata jina kwa kura.

Ila sasa naona watu wanaanza kununiana tu nani mwenye haki ya kuchagua jina na jina lipi litumike.

Nilichoamua ni kuwa majina x na y yote yaandikwe kwenye cheti. Yaani aitwe YX.

I hope kila upande utaridhika na vita itakwisha.
 
Huku kwetu mwenye jukumu la kutoa jina ni baba wa mtoto peke yake, hao wengine ni washauri tu, ila jina huwa tunatoa sisi baba.

Hata mabibi au mababu huwa wanatulia na unapigiwa simu baba mwenye mtoto kama uko mbali au vipi, utoe jina huko huko.

Sisi wengine huwa tuna majina yetu tayari, na wake zetu huwa wanajua kama tukijaliwa mtoto wa kike au wa kiume ataitwa fulani.
 
Halafu ukute majina yote yanayofarakanisha watu ni ya kigeni!

Ushauri wangu:
1. Jina lina nafasi kubwa sana katika maisha ya mtu. So, kuwa makini kwenye kuchagua jina
2. Jina ni identity, ni asili, ni utamaduni. Zingatia hili, labda kama hutazami mambo kwa jicho la tatu
 
Mimi wa kwangu alikaa wiki bila kupewa jina hadi nilipoambiwa na mama yake kuwa tunasubiria jina la mtoto nikalitamka likawa hilo hadi kesho.

The same kwa mtoto wa kike same same nashangaa huyo mwanamke wako anachogombania nini basi kuna siri nzito usipuuze hakuna kitu mwanamke anachobishania kwenye mahusiano kisichokuwa na sababu za nyuma kwake.
 
Bila shaka uki unganisha ayo majina YX jina litakua baya ilo msi mtese mtoto
Kuna rafk yangu, alipata mtoto nikamuuliza jina nashangaa ni majina mawili, angel Maria sijui..nikamwambia akujibu maana ni mshikaji, kuna mengine eti Rosemarry..

Alafu jina anatoa baba fullstop, ukishaanza bishania jina..safari itakua ndefu sana ndani ya ndoa

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Nilichoamua ni kuwa majina x na y yote yaandikwe kwenye cheti. Yaani aitwe YX ...... I hope kila upande utaridhika na vita itakwisha
Mbona hata WA kwangu nimeunganisha majina? Simple? Maria-Rosa
 
Back
Top Bottom