Shida ya kubadili jina la mzazi

buyoya419

JF-Expert Member
Oct 20, 2017
555
416
Naombeni mnipe ushauri nifanye nini

Nilitaka kumweka mzazi kama mtegemezi kwenye bima yangu ya Afya

Walinikatalia nikawauliza wakaniambia jina la mzazi kwenye cheti changu cha kuzaliwa lipo tofauti na NIDA yake na ni kweli kwenye cheti limeandikwa kama hivi Zainabu D/O Mussa na kwenye NIDA yake limeandikwa Zainabu Ombeni Shafii

Nimeenda RITA ofisini kwenye suala la kuchange jina wamenigomea wamesema afatishe la kwenye cheti coz ndio cha kwanza kutengenezwa na Mzazi mwenyewe anasema la kwenye cheti lilikosewa

Nimebaki njia panda hapa coz siwezi nikamuweka kama mtegemezi na mambo mengine

Nisaidieni nifanye nini ili likae sawa la kwenye NIDA ndio lipo sahihi
 
Chukua deedpol chukua form ya kiapo,peleka kwa msajili sijui ndo wa ardhi...baada ya hapo itahitajika ukatangaze kwa gazet la serikali.....baada ya hapo mwambie mama akajisajil upya ...ila Kuna gharama utatumiq mpka kufanikisha
 
Pole sana.

Nenda kwa mwanasheria akuandalie deed poll, ambayo itakana majina uliyoyaweka wewe kwenye cheti cha kuzaliwa/cha kwake cha kuzaliwa na kukubaliana na yale yaliyopo kwenye NIDA ya bi.mkubwa.

Ikishakamilika peleka ofisi ya usajili nyaraka -wizara ya ardhi. Utapatiwa nyaraka ambayo utarudi nayo bima uambatishe na fomu ya bima.

Kila la kheri.
 
Asanteni ngoja nimtafute mwanasheria anifanyie mpango wa deedpoll
 
Back
Top Bottom