Kadi ya chombo cha moto kuendelea kusoma jina la mmiliki wa mwanzo licha ya kubadilisha

Isaac1

Member
Nov 12, 2018
79
70
Habari zenu msaada wenu pls kwa hili.

Miezi mitatu iliyopita nilinunua bajaji kwa mtu kwa ajiri ya kufanyia biashara.

Akanipa kadi na nikaenda TRA (DSM)

Ila kutokana kuwa nilikuwa na haraka na naishi mkoani nikaamua kuwatumia vishoka maana bajaji kadhaa nimewatumia.

Nikarudi mkoani ili waendelee na ubadilishaji na mwisho wa siku wakanitumia control number ya kulipia nikalipia kwa ajiri ya kubadilisha umiliki.

Japo sijapata muda wa kurudi DSM kwahiyo kadi sijachukua mpaka leo.

Ila maelezo yake niliyempa kazi anadai kuwa iko tiyari.

Sasa cha ajabu juzi kati dogo anayeindesha alikamatwa na traffic kwa kosa la kutokuwa na bima, sasa cha kushangaza dogo baada ya kunitumia ile karatasi ya machine ya trafiki naona bado inasoma jina la mmiliki wa mwanzo, kumpigia simu yule anadai kuwa huwa inatokea hivyo kwa upande wa bima je ni kweli au kuna makosa yamefanyika?

Naombeni majibu kwa wajuzi wa haya mambo.

Asanteni.
 
Back
Top Bottom